Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli

MFANO MGUNGA MWAMNYENYELWA, ALIAMUA KUBADILI MAJINA YAKE NA KUTUMIA HAYA REAL AFRICAN NAMES,
 
Mkuu Isanga Family, kuna issues mbili zinazojitegemea. Uhakiki wa vyeti bandia ndio hoja iliyopo mezani na sio uhakiki wa majina.

Jina la Mwigulu Mchemba ndilo jina bandia, lakini aliyesoma ndio huyo Mwigulu, aliyehudhuria darasani ndiye huyo Mwigulu, mwenye akili ndani ya kicwa chake, ndio huyo Mwigulu, aliyehitimu, ndio huyo Mwigulu, hivyo vyeti vyake vyote ni bonafide genuine, na jina pia ni lake ila ni just a given name. Hakuna jinao yoyote kwa mtu yoyote kutmia jina lolote, popote.

Pasco
 
Sasa si alishasema kuwa alikaa nyumbani miaka miwili kuchunga ngombe?
Ina maana aliporudi aliendelea na jina la mtu mwingine

Kwa mtazamo wangu, hicho ndio kilichotokea asingeweza kurudi tena darasa la tano akaendelea kwa jina lake, kimsingi jina lake halikua tena kwenye orodha ya wanafunzi halali wa shule. Hapo ndio ilibidi apatiwe jina la mtu mwingine. Kama nnachosema sio kweli, taarifa za tarehe yake ya kuzaliwa zitakua na mushkel eneo flan, unaweza kukuta ana tarehe mbili za kuzaliwa, ya kwake na ya yule mwenye jina.

Pasco ameshanikataza kusema ukweli, naamini ukweli halisi unaweza usiwe huu lakini utakua unakaribiana na haya maelezo.
 
MFANO MGUNGA MWAMNYENYELWA, ALIAMUA KUBADILI MAJINA YAKE NA KUTUMIA HAYA REAL AFRICAN NAMES,
Tena sasa huyu ni Dr. wa Ph.D!, ndiye aliyemuibua Mpoto.
Tunawauliza watu humu kwani majina ndio nini, hawana majibu!.
Pasco
 

Pasco, naomba muulize mheshimiwa aweke hapa tarehe yake ya kuzaliwa ilinganishwe na zilizopo kwenye nyaraka za kisheria kama hati ya kusafiria, cheti cha kuzaliwa na habari zilizopo kwenye taasisi za elimu alikosoma kama zinafanana.
Hapo ntakua upande wako.
 
Mkuu Msamaria, sijakataza watu kusema ukweli, nimesema "he who allege must prove".

Pasco
 
Mkuu Msamaria, hizo zinaitwa personal details ni confidential info za mtu, zinapatikani zikihitajika tuu, jf haijazihitaji ila wenye nazo pia wamo humu na wamezikalia.

Pasco
 
Kuna watu wameshindwa elewa kuwa hayo majina "feki" ya Nchemba ndo aliyofanyia mitihani yote na kupata vyeti vyake, ni nini kigumu hapa kuelewa? Sioni tatizo lolote maana vyeti vyote ni halali yake kwa jina alilotumia.
Kwahiyo ukichukuwa jina la mtu alie faulu vizuri darasa la saba ukaenda kusomea then form four ukafaulu vizuri, hapo hakuna shida?
 
Pasco
Nimemkumbuka sana marehemu Peter Kinyanjui ambae sisi tuliambiwa ni Alhaj Omar Juma na pia alikuwa na a.k.a. ya Mark Twist mpaka tukampa na ofisi kubwa kabisa nchini humu. Kumbe jamaa alikuwa ni alien kabisa.
Mkuu Safari, mambo mengine yaache hivyo hivyo kama yalivyo, tukianza na uchunguzi wa nani ni nani na asili yake ni wapi, patakuwa hapatoshi humu, haswa data za jamaa yangu mmoja aitwae Kotto, sikishuka humu, jf yenyenyewe itakuwa kwenye hati hati.

Pasco
 
Sheria inakutaka ukibadilisha jina kwa mambo rasmi (official) inakutaka uende mahakamani ukaape hivyo
Sijaona mahali Comrade amefanya hivyo na kwa Unyeramba ya wakati ule sidhani hata kulikuwa na mahakama karibu
Pana kosa mahali hapa.
 
Mkuu pasco lisemwalo lipo muda ndio utakaozungumza usitumie nguvu kutetea jiulize kwa nini iwe yeye tuu na hiyo imetokea baada ya kutaka kugombea Urais siasa zinaleta uozo uliojificha nakumbuka kihiyo alikua mhandisi wa Temeke kwa muda mrefu tuu bila shida na hakuna aliehoji vyeti vyake na alifanya ukaguzi wa bara bara za Temeke kipindi hicho ilikua Wilaya kama mhandisi wa wilaya alipokuja kwenye siasa za ubunge ndio madudu ya kufoji vyeti yakajulikana kwa hiyo hata huyu unaemtetea leo muda ndio utaongea usitumie nguvu kuniaminsha unachosema wakati najua kuna ujanja ujanja hapo,..
 
Kuna Nafasi fulani mtu anapaswa kuwa na Majina hata 3 tofauti tofauti na sa zingine sahihi hata 4 tofauti.
 
Mkuu Msamaria, hizo zinaitwa personal details ni confidential info za mtu, zinapatikani zikihitajika tuu, jf haijazihitaji ila wenye nazo pia wamo humu na wamezikalia.

Pasco

Mie naishia hapa, nnachoamini majibu ya mheshimiwa yataibua wachunguzi wengi sana kuchunguza na kufuatilia hili jambo undani wake. Ni maombi yangu matokeo yaendane na alichokisema ndugu yangu nnayemheshimu sana Mwigulu Nchemba vinginevyo itakua ni fedheha.
 
si sahihi. Hii ni mtu kacheza na photoshop tu. wala gazeti halina makosa hapo!

angalia namba iliyopo kulia chini ndipo utagundua. Kama gazeti wangerudia basi nafasi hiyo ingekuwa na namba mpya!
Likirudiwa ndio linakuwa na namba ile ile, likiwekwa namba mpya inabidi lirudiwe tena, hizo ni accounting number za mapato.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…