Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

mkuu umeshinda upewe tu hii hela
 
Mkuu hongera kwa wazo zuri,, kama ukikosa hii pesa nicheki PM tufanye kitu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Nini wazo lako usiliimarishe zaidi na kuwapa HUDUMA wamiliki wa gesti kwa HUDUMA zote za chap na za kupumzika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BIASHARA YA KUUZA CHIPS ZA KUPIMA KWA WANAFUNZI

Mahitaji :

Kuni : 10,000 (Hizi kuni nitanunua kwa siku ya kwanza tu kwasababu ndio naanza biashara,siku zinazofata sitonunua kuni za 10k nitakua nazunguka kwa mafundi Seremala nachukua mbao mbao,zitanifaa)

Matofali 3 @ 1500 (haya ni mafiga ya jiko langu)
Karai la chips : 9000
Ndoo ndogo mbili : 5000
Mafuta ya kula liter 3 : 9000
Deli la kuwekea chipsi zangu : 4000
tomato: 1500
kachumbari : 3000
viazi:8000
magazeti : 2000
visosi/visahani:5000
Vifaa vingine vidogo vidogo : ninavyo nyumbani (kisu,chumvi,nknk)
Total : 48,000 ( 50,000 - 48,000 = 2000 hii itakua yangu ya kula siku ya kwanza nipo kazini)

Kwenye kuuza nitakua napima chipsi kuanzia za sh.200 mpk 1000,nina uwezo wakuingiza Faida kwenye hii biashara zaidi ya 10,000 per day x 30 = 300,000

itakapofika mwisho wa mwezi nitaweza kukurudishia ile 50,000 yako mkuu,hiyo ni uhakika Kama tu Shetani hatocheza na Afya yangu, Na Kwa Jina la YESU hatoweza.
 
10000 × 30 = 300000

hao wanafunz utawauzia chips mpaka jmosi na jumapili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Nini wazo lako usiliimarishe zaidi na kuwapa HUDUMA wamiliki wa gesti kwa HUDUMA zote za chap na za kupumzika

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli ila wazo langu limelenga zaidi kutatua kero za makazi hasa katika miji mikubwa kwa kuhakikisha kwamba mtu anao uwezo wa kupata taarifa ya eneo lolote lile kabla ya kuhamia na kufahamu iwapo sehemu husika itamfaa kwa kutumia mbinu za kitaalam.
 
Ni Beer pure na lengo langu ni kuibrand na kutengeneza vifungashio vya brandi yangu, kupanua production na kuongeza wigo wa supply kufikia mikoa mingine.
Hata TBL hawakuanza maeneo yote!
Hata Banana Walianzia K'njaro na Chuga tu leo wanabamba kila kona.
Wazo zuri ,hivi wanzuki SI Ni jamii ya beer ile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…