Habari Mkuu
Mimi nitaitumia 50000/= katika mchanganuo ufuatao kupitia biashara ya mahindi ya kuchoma
Naishi temeke stereo jirani na soko hapo wanauza mahindi mabichi nami ndiyo biashara niliyowah kuifanya Tandika sokoni
Mchanganuo
Mahindi 50@300= 15000
Usafiri = 500
Mkaa. = 1500
Chumvi. = 300
Ndimu. = 300
Ushuru. = 500
Pilipili. = 300
JUMLA. 18900
MAUZO
Nitauza mhindi 1 kwa shilingi 800 hiyo kwa mahindi 50 kwa siku n shilingi ( 50×800= 40000)
jiko ninalo hivyo sihitaji kununua
JUMLA YA MAUZO - JUMLA YA MCHANGANUO.
40000 - 18900= 21100
kwa hyo ninauhakika wa kurudi na elfu 21100 kila siku kumbuka situmii nauli kurudi nyumbani
Ninauwezo wa kuuza mahindi 50 kwa sababu Tandika n sehemu ambayo inawatu wengi ni soko kubwa hvyo mwingiliano wa watu ni Mkubwa
Baada ya siku 7 ninauwezo wa kuwa na shilingi 147700
Pia kumbuka katika elfu 50 ya mtaji baada ya matumizi ya siku ya kwanza ilibaki (50000-18900= 31100) itabaki shilingi 31100 nitaitumia kuongeza mtaji taratibu kwa siku zinazofuata maana biashara sio siku zote huwa nzuri.
Sent using
Jamii Forums mobile app