Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Hapa kila mtu atatoa wazo lake kutokana na mazingira aliyopo, kwa mfano mimi ukinipa hiyo pesa nitafanya hivi:
1. Ngano kg25 @31000
2.Mafuta ya kupikia lita 3 @11000
3.Amira kipimo cha 1000
4.Baking powder pakti 1@500
5. Bicarbonate pakti 1@500
6.sukari kilo1@2600
7.Iriki pakti 1@1000
8.Kuni mzigo 2000
Hadi hapo itakuwa nimemaliza mahitaji yangu,kwa hiyo nina uhakika wa kutengeneza kila baada ya siku mbili
Halfcake 100@20000
Maandazi 100@10000
Ndani ya huo mwezi hela yako nairudisha na nabakiwa na mtaji wangu mkubwa tu.
NOTE:Nimesema wazo linategemea na eneo ulilopo kwa hiyo kwa eneo langu mimi hili jambo linawezekana kwa kiasi kikubwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitaigawa hio 50,000 mara 50 ili nipate elfu 1..

Kwakua hii week ninya Uefa na Europa nitaweka mikeka 25 kwa umakini mkubwa na uchambuzi wa hali ya juu.. mwisho wa week nitakuwa na pesa ambayo sio chini ya 150k.

Ile 25k iliyobaki ambayo sikuweka mkeka itakuwa kama plan B incase mikeka ikifeli yoote..
Hii 25k nitanunua unga wa ngano na mafuta nitengeneze maandazi na chapati (nina hiki kipaji cha kupika) nitayapeleka haya maandazi na chapati weekend kwenye hostel za wanachuo (weekend wengi wanaona uvivu kuamka asubuhi kununua chai ) .. nitawasambazia maandazi hayo hadi saa 6 mchana na pesa yangu itakuwa imerudi.
 
Hili wazo lenye uhalisia sana na ndio ninaloliendea sasahivi, labda uwe umejikita kwenye biashara za kuzalisha si zakutoa Huduma maana wote naona wanaleta mawazo yakuzalisha.

Hii ni FREE CARWASH
_Naoshea maeneo ya posta hiyo 50,000/= inafikishwaa kwa siku 2 cash as profit na siku kama ya leo na kesho magari yapo full packed na wengi wametoka kuuatumia siku za weekend hata kwasiku moja if Odds in my side that day.

MCHANGANUO
_Hii biashara ipo hivi gari unaosha kwa 2000/= mpaka 10,000/= inategemea umemuoshea nani maana wanaosha mpaka ma Range Rover, V8 sasa mtu ukimuoshea anakupa tu “chukua hii 8000/= Nipigie maji” unajikuta kwa siku mbaya 30,000/= kawaida.

ENEO LA BIASHARA
_Posta maeneo ya Golden jebelee tower, kuna ofisi nyingi kubwa maeneo ya nje ndio inapofanyika Huduma hii ubaazi wa SERENA HOTEL unaosha magari non-stop kutwa mzima.

MTAJI
_Hii biashara haitaji Mtaji mkubwa kwasababu unahitaji vifaa ambayo madumu na vitambaa ILA kwenye inabidi ujiunge kwenye kikundi kwa 70,000/= hili uwe mwanachama nishawapa 20,000/= ndio nahaso iyo 50,000/= niwakamilishie.
_kwa kuongeza thamani ya Huduma nanunua matauro meupe, mafuta Air freshener, Polish ya dash board n.k ili kumfurahisha zaidi mteja hii itafanya niweze kumpandishia bei mteja na kupata faida maradufu.

UHALISIA
_Leo ndio natoka kuwapa 20,000/= nakupeleka dumu zangu asubui tu hata SAA 2 bado wakaamua wanipe nauri yakurudi kwakupewa gari moja nioshe nimekula 5000/= cash hiyo kabla ya saa 2 ijafika imagine kutwa nzima.

So, kwahuwo Mtaji wa 50,000/= ambao kwangu ni mtaji wa kujiunga uwanachama na kuonheza matauro na mafuta siku 2 tu naitengeneza.

NB: hii dunia ya leo mawazo ya kutoa Huduma yanapesa hata ukianza chini.

IDEA IN PROGRESS...NEED BACKUP CAPITAL


Faida kabla saa 2 leo.
IMG_20200217_105132.jpeg


Vifaa vya kazi
IMG_20200212_092045.jpeg


Portfolio | 2020
 
50000.

1.elfu 50000 naigawa kwa 6000 = ambapo nitapata 6000×8
- naenda natafuta kuku majumban kwa watu kwa 6000 , = na kuku nane , ambapo nitaenda kuwauza kwenye mabanda yakuuzia kuku kwa 7000-8000
-ambapo kwa Siku na uakika wa kufanya mizunguko miwili ,ambapo faida kwa kila kuku kukadilia ni 1000 ×8=8000,ambapo nikifanya mizunguko hiyo 2 kwa siku napata 16000 ambapo kwa mwezi nikizunguka napata 480000-380000 kutokana na mzunguko kwa mwezi adi kurudisha marejesho,
-
-
ASANTE MKUU NIPE MKOPO ,NIKO SERIOUS
-
-
0694424169

ASANTE
 
Back
Top Bottom