Utofauti wa mishahara katika Utumishi wa umma, kunavunja moyo na kusababisha watu kubeza kusoma sana

Technically unachosema ni kwamba yule wa 2mil ashushwe ili awe anaipata 1.4m.

Kwa ufupi ni kwamba unasema mwenye mshahara wa 2mil ASHUSHWE.

Hiyo ndio roho mbaya ninayozungumzia hapa sasa. Sasa huyo akishushwa inakuwa imekusaidia nini wewe kwa mfano.
0.9MX2=1.8M
0.9MX2.5=2.25M bado hajamfikia wa 2.4M

Kwamba watu wawili wanafanya kazi za serikali moja ,level ya elimu/utaalam ni ile ile. Mmoja akiwa analipwa mshahara wa watu wawili wa watu wengine Na chenji 600k. Kwako wewe roho nzuri ni 900k abaki hapo hapo na 2.4M abakie hapo hapo. Mimi nimesema 2.4 ashuke hadi 1.4M ili 0.9M apande hadi 1.4. Au mmoja 1.6M kwa 1.6. Roho mbaya ni mmoja kulipwa zaidi ya Mara mbili ya mwenzie.

NB: nimechukulia kwamba serikali inawezakataa kuongeza 0.9M afike 2.4M kwa vile itajitetea kuwa itabidi itafute itoe more money badala take izigawanye inazotoa sasa
 
Suti atanunuliwa Na serikali. Huwezi mzidi mwenzio 1M kila mwezi ambayo ni 12M per year ambayo ni 60M kwa miaka mitano ambayo ni bonge la nyumba au bonge la mtaji au bonge la gari kwa kisingizio cha suti,na unadhifu wa mavazi.
Kutaka watumishi wote serikalini wafanane mishahara ni ujinga,
Mtu lazima alipwe kutokana na unyeti wa taasisi aliyopo,Dereva wa jaji mkuu,awezi kulipwa sawa na dereva wa Tanesco anayepereka mafundi site,
Dereva wa jaji lazima awe na mavazi stahiki,suti,huyu anatunza siri,ukipata hii nafasi lazima ulipwe vzr Ili uendsne na boss na ofisi unsyoihudumia,dereva wa Tanesco,dawasa,muruwasa,Hawa ni kuvaa overlol tu,
 
Lets say Serikali haina uwezo wa kupandisha mishahara ya Electrical engineers wote iwe 2mil.

Kwa hiyo Solution ni huyo Electrical Engineer wa 2mil ashuke ili naye alipwe laki 9 ili hao wafanyakazi wa serikali wawe sawa?

Hebu nijibu hili swali directly bila kupindisha pindisha maneno.

Ikiwa Serikali haiwezi kuwalipa wote 2m hilo ni tatizo la serikali, mimi ningeshauri serikali itafute namna ya kufanya mishahara hiyo iwe sawa iwe ni kupandisha walingane au kushusha walingane whatever the case lakini haki iwepo.

Ni jambo la ajabu sana mmesoma wote elimu sawa, ujuzi sawa lakini mishahara tofauti katika serikali ile ile.
Hali hii inashusha morale ya kazi, inapelekea watu kutaka kuhama daily kiukweli hakuna aliyesoma alaf apate kazi kupoteza muda kila mmoja anahitaji fedha ili mambo yake yaende, nadhani serikali iwe na chombo kimoja cha kuratibu masuala ya mishahara.

Kama wewe ndio unapata 2m na mwenzio laki 9 basi kumbuka hata yeye hakusoma kupoteza muda, serikali iweke usawa kwa watu wa fani zinazofanana, ukiona unaumia hiyo ndiyo haki vumilia acha ubinafsi mzee
 
Ninakuuliza swali na ninaomba unijibu hapa directly bila kuzunguka.

Dereva wa tanesko anayepeleka nguzo kwa wateja anatakiwa alipwe sawa na dereva wa mkuu wa nchi ikiwa wote wana elimu sawa?

Let's say dereva wa tanesko analipwa laki 5,unamaanisha na dereva wa rais alipwe laki 5?
Hebu jibu hapa.
 
Na wa Tanesco alipwe 3mln ndo inavyotakiwa uwe umesoma elimu moja nk suala ni mazingira ya kazi ni tofauti na mashirika hayo yanatakiwa kuzalisha na kiasi wanachozalisha na kikupwa kuliko services za salary zao but nyie wa Halmashauri kwanza hata kujiendesha hamuwezi lakini pia unyeti wa kazi.

Ukimlipa Tbs vihela vya huko Halmashauri atahongwa mpate bidhaa feki afu mufe tuu kama mizogo

Katika kuchangia kwako umejua kabisa mimi natoka Halmashauri?
Watu mnapenda kujimwambafai sana humu ilihali tunatumia fake id.

Jikite kwenye hoja, unyeti wa taasisi ni kutokana na majukumu yaliyopangwa, mishahara inaweza kuratibiwa na serikali kuu na wote wakalingana wakabaki kutofautiana posho za mazingira ya kazi.

Suala la mshahara ni muhimu sana lina impact kwenye kikokotoo ni vema serikali ikafanya harmomization mapema
 
Ipo siku mtakuja kusema Magu ni nafuu kama leo mnaona Kikwete alikuwa bora.

Utawala wa Kikwete ndio umeasisi mambo mengi ya hovyo kama haya ya kutekana na kunyanyasa wapinzani hivyo ndio wa kulaumiwa leo na hata kesho.

Halafu usitutoe kwenye mada.
 
Technically unachosema ni kwamba yule wa 2mil ashushwe ili awe anaipata 1.4m.

Kwa ufupi ni kwamba unasema mwenye mshahara wa 2mil ASHUSHWE.

Hiyo ndio roho mbaya ninayozungumzia hapa sasa. Sasa huyo akishushwa inakuwa imekusaidia nini wewe kwa mfano.

Hata kukataa mwenzio kupandishwa mlingane au kutafuta average mlingane nayo ni roho mbaya
 
Ninakuuliza swali na ninaomba unijibu hapa directly bila kuzunguka.

Dereva wa tanesko anayepeleka nguzo kwa wateja anatakiwa alipwe sawa na dereva wa mkuu wa nchi ikiwa wote wana elimu sawa?

Let's say dereva wa tanesko analipwa laki 5,unamaanisha na dereva wa rais alipwe laki 5?
Hebu jibu hapa.
Tatizo hili swali hawataki kulijibu wao wanang'ang'ania kusoma course sawa Ila hawazungumzii majukumu kuwa sawa au siyo sawa
Sasa Kama dereva wa rais analipwa sawa na dereva wa halmashauri, Nani ataenda kumuendesha raisi wakati anajua majukumu yatakuwa makubwa Sana kuliko akikaa halmashauri
 
Umeambiwa dereva wa Tanesco sio mtu muhimu kwakuwa anapeleka nguzo site? Kwahiyo dereva wa Tanesco akipewa kumuendesha rais hataweza?
Huyo dereva wa rais ana kitu gani exclusive sana ambacho wenzake hawawezi kufanya?
Hizi ni branding tu.
Serikali ilinganishe mishahara alaf posho za huko kwenye taasisi zibaki kama zilivyo, kumbuka mishahara ina impact kwenye vikokotoo
 
Tatizo hili swali hawataki kulijibu wao wanang'ang'ania kusoma course sawa Ila hawazungumzii majukumu kuwa sawa au siyo sawa
Sasa Kama dereva wa rais analipwa sawa na dereva wa halmashauri, Nani ataenda kumuendesha raisi wakati anajua majukumu yatakuwa makubwa Sana kuliko akikaa halmashauri

Hakuna swali la msingi hapo.
Kulinganisha mishahara hakuna shida yoyote, huko kwenye taasisi kuna posho waendelee kulipana tofauti ila mishahara ambayo ina impact kwenye kikokotoo ni vema ikalingana.
 
0.9MX2=1.8M
0.9MX2.5=2.25M bado hajamfikia wa 2.4M

Kwamba watu wawili wanafanya kazi za serikali moja ,level ya elimu/utaalam ni ile ile. Mmoja akiwa analipwa mshahara wa watu wawili wa watu wengine Na chenji 600k. Kwako wewe roho nzuri ni 900k abaki hapo hapo na 2.4M abakie hapo hapo. Mimi nimesema 2.4 ashuke hadi 1.4M ili 0.9M apande hadi 1.4. Au mmoja 1.6M kwa 1.6. Roho mbaya ni mmoja kulipwa zaidi ya Mara mbili ya mwenzie.

NB: nimechukulia kwamba serikali inawezakataa kuongeza 0.9M afike 2.4M kwa vile itajitetea kuwa itabidi itafute itoe more money badala take izigawanye inazotoa sasa
Kwa nini huyo wa 0.9 asihamie huko wanapolipwa 2.4 ili naye awe na mshahara mkubwa?

Huyo wa 2.4 akishushwa inamsaidia mini huyo wa chini?

Hizi ndio mentality za roho mbaya ninazozizungumzia.

Kama unalipwa 0.9 na unaona haitoshi, acha kazi nenda hapo wanapolipwa 2.4...its as simple as that.
 
Roho mbaya ni pamoja na kufurahia ubaguzi wa mishahara unaofanya wengine waishi kama wafalme na wengine waishe kama vijakazi wa mfalme ili hali wote wana elimu inayofanana.
 
Tuna tatizo la kufukiria kama watanzania.
Mleta mada ameleta hoja inayotakiwa kujadiliwa lakini watu mnahamisha mada na kuanza kumshambulia.

Hii fact mbona iko wazi sana, Electrical engineer wa Halmashauri alipwe laki 9 na electrical engineer wa TBS alipwe 2m ilihali wote wamesoma taaluma moja na wameajiriwa na serikali na sisi kama watanzania bado hatuoni kuna tatizo hapo? Majibu yanatoka kwa jazba tu kama vipi nayeye aende huko TBS akapate mshahara mnono, kwahiyo halmashauri hawahitaji electrical engineer?

Ni kweli hayo majibu ni majibu sahihi kwa wasomi mlioko humu jamvini au kwakuwa mwafrika ni mbinafsi zaidi regardless anafanya nini na wapi?
Hio ndio shida, mishahara inatakiwa iwe standardized! Hiki ndicho wazungu wametuzidi na ndio maana ni rahisi hata ku regulate sheria za kodi kule kwao. Earnings za mtu wa mtaani unakuta ni usd 15 per hour...wa ofisini wana range kwenye 20-23 na hapo hamna BOT wala halmashauri.

Ila imagine kwetu std 7 wanalipwa 12M kwa mwezi ila wenye cheti mpaka PhD ni 350K - 4M halafu mnategemea yule anaelipwa 12M awatetee nyie wa less than 4M ambao mko million kadhaa kikatiba kwa kupigania sera nzuri za kodi. Never!
 
Hakuna swali la msingi hapo.
Kulinganisha mishahara hakuna shida yoyote, huko kwenye taasisi kuna posho waendelee kulipana tofauti ila mishahara ambayo ina impact kwenye kikokotoo ni vema ikalingana.
Mtu analipwa kutokana na majukumu yake , faida anayoiingizia serikali, unyeti wa kazi yake n.k Siyo effect za kikokotoo.

Ni jukumu la Kila mmoja wetu kuzitafuta hizo kazi zenye mishahara unayoamini kuwa ni mikubwa na siyo kulazimisha watu tufanane mishahara wakati majukumu yetu ni tofauti eti kwa sababu tu tuna level moja ya elimu.
 
Kwa nini huyo wa 0.9 asihamie huko wanapolipwa 2.4 ili naye awe na mshahara mkubwa?

Huyo wa 2.4 akishushwa inamsaidia mini huyo wa chini?

Hizi ndio mentality za roho mbaya ninazozizungumzia.

Kama unalipwa 0.9 na unaona haitoshi, acha kazi nenda hapo wanapolipwa 2.4...its as simple as that.
Its as simple as that wakati unajua wazi kuna ufinyu wa nafasi...be real hata kidogo! I don't believe you are this dumb.

Au unafikiri kwenda huko ni kama kwenda maliwatoni!?
 
Ndiyo maana Kuna mishahara mikubwa kwa sababu nafasi ni chache, na ukipata nafasi hiyo unaiingizia serikali pesa nyingi sana( mfano Tanapa) tofauti na halmashauri ambako mnaweza kuwa wengi lakini pesa mnayoingiza ni kidogo Sana
 
Back
Top Bottom