Kuna kipindi (The Medieval Age/ Dark Ages), wakati Asia iko kwenye mwanga, Ulaya ilikuwa ni sehemu iliyojaa uchawi, magonjwa na vita. Wazungu walikuwa ndiyo watumwa wakubwa wa kifikra, kama ambavyo Afrika ipo leo hii. Walipenda sana dini na ushirikina.......
Kipindi hicho walioifanyia dunia mambo makubwa ya kisayansi walikuwa ni waarabu wa Baghdad (The Abbasid Caliphate). Ambao wao ndiyo walianzisha mbinu ya kisayansi (The Scientific Method) ambayo dunia hii inatumia mpaka leo.
Wasomi wa kiislamu ndiyo walianzisha mfumo mzima wa kuweka sifuri kabla ya namba, wakiitoa hii mbinu kul India, tofauti kabisa na walichofanya Wagiriki. Falsafa zilizopotea kwenye maktaba ya Alexandria (The Museon) zilikuwepo zikifundishwa kule Baghdad.
Lakini, leo hii ukiambiwa kwamba waarabu ndiyo walioanzisha vitu muhimu kama Algebra, nadhani huwezi kukubali hata kidogo. Hii ndiyo historia ilivyo (It's never linear).....
Tatizo naloliona kwetu Waafrika ni kutaka kuruka hatua za maendeleo na kutaka kuishi kama watu wa Magharibi. Hamtafanikiwa na mtaishia kupiga mbizi kwenye lami tu.
Ulaya kufika hapa ilipo, iliwachukua miaka isiyopungua 1500, iliyokuwa imejaa giza, magonjwa, vita, mauaji makubwa, udikteta, ufisadi na mengineyo. Hivyo, haya mnayopitoa Waafrika siyo mapya, na lazima myapitie kwasababu hamuwezi kuruka hatua za kimaendeleo....
Yaani Tanzania imekuwa taifa mwaka 1964, haina hata miaka 100, halafu leo hii mtake kuwa kama Waingereza wenye taifa lenye miaka zaidi ya 800 kweli ????
Mbaya zaidi wajama kama Mwalimu Nyerere waliwaaminisha waafrika wengi kwamba maendeleo ni uchumi tu (Materialism), wakisahau kwamba manedeleo ya binadamu pia yako kijamii na kisiasa. Ndiyo maana utashangaa nchi za fulani zimepiga hatua kubwa kiuchumi lakini watu wake wanaishi kwa hofu kubwa na bado hawajastaarabika........
NB: Huwezi kuruka hatua za maendeleo. Nchi za Afrika (As political entities) ni changa mno bado.....