Utofauti wa Mwafrika na watu wengine hauko kwenye rangi tu, hata akili. Mtu mweusi kapunjwa akili

Ndio maana wakasema mtu mweusi ametokana na Sokwe, je unajikubari wewe ni Sokwe?
 
Nakuunga mkono.
Nina mfano mwepesi.

Nikiwa shule advance kulikuwa na shida ya chakula yaani kupata mboga za majani ilikuwa ni tabu na wote mnajua kerocya maharage kila siku.

Nilipropose kwa mwalimu mkuu kwamba kwa kuwa hatua 20 toka eneo la shule pana kijito kikubwa kinachotiririsha maji miezi 10 kwa mwaka na pia pembeni pana ardhi yenye rutuba basi tunaomba atupe ruhusa ili tulime pasiwe na shida ya mboga.

Nasikitika ya kuwa alinisikiliza halafu huyo akaenda zake.
 
Hujafanya tafiti za kutosha ndugu yangu, na pia unanisikitisha sana ambavyo unajiona duni mbele ya jamii nyingine. Huwa nikiwasoma watu wengi kama ninyi, huwa ndiyo napata kufahamu kwamba mzungu alifanikiwa kwa asilimia 100% kumtawala mtu mweusi, kwasababu ameshikilia fikra zetu. Kiufupi mimi nakukubali sana Nankumene japo katika hili naomba niendelee kukukusoa na kama kuna kitu nakosea naomba niambie nifahamu. Niko tayari kujifunza vitu vipya:

Mosi, bila ubishi wowote ule Misri ya kale (Kemet) ilikuwa ni dola la watu weusi. Ushahidi wa kutosha wa hili ninalosema uko kwenye The Egyptian Hieroglyphs. Nafurahi sana kuona umemzungumzia mwana-mahesabu wa Kigiriki Pythagoras. Hivi unafahamu kwamba Pythagoras kama Plato aliwahi kusoma elimu yake ya juu kule Misri ya kale ??? Kiufupi mpaka kufika vita ya Kalkemish (The Battle of Carchemish), vita baina ya Misri na Babeli, Misri ilikuwa inatawaliwa na mafarao waliotoka Sudan (Nubia). Farao Necho II alikuwa ni mnubi wa Sudan. Hili nalo utataka kulipinga ndugu yangu ???

Pili, narudia tena kuhusu Berbers (The Amazigh People). Hii jamii ya kiafrika ndiyo walikuwa wanajeshi wa muhimu wa kalifeti ya Ummay (The Umayyad Caliphate), ambapo walisaidia kwenye uvamizi wa Uhispania. Hata neno GILBRALTAR limetokana na neno la kiarabu Jabal Tarid (The Mountain of Tariq), ambapo walimuenzi kamanda wa kiislamu aliyeongoza uvamizi huo aliyeitwa Tariq Ibn Ziyad. Hawa waafrika (Berbers) ndiyo waliotengeneza falme imara kama Numidia ambazo zilishirikiana na ufalme wa Karthago (Carthage) katika kupambana na Rumi kwa miaka zaidi ya 100 (The Punic Wars).

Baada ya Warumi kumshinda Hannibal mwaka 146 BCE (The Third Punic War), Scipio Africanus aliamuru dola la Karthago lichomwe moto lote na watu wake kuuzwa utumwani. Walifanya sawa na kile ambacho Mongols chini ya Monghke Khan walikifanya kule Baghdad mwaka 1258 (The Siege of Baghdad) ambako kulikuwa na maktaba kubwa na vyuo bora kabisa duniani kwa wakati huo. Leo hii historia ya haya madola hazipo. Lakini, hata kama hazipo, basi tuseme kwamba waafrika wana akili ndogo kuliko jamii nyingine ???

Tatu na mwisho kabisa, waafrika wana historia ambayo haijazungumzwa na kufanyiwa tafiti vilivyo. Wenzetu wazungu wamefanikiwa sana katika kuaminisha weusi kwamba hawana historia. Wengi wetu hili tumelibeba kama lilivyo bila kulipa tafakuri za kina. Naomba nikupe mifano ya mwisho: Kipindi Roma iko chini ya Kaisari Augustus, vilitokea vita vikubwa baina ya Ethiopia (Nubia) na dola la Mrumi mwaka 24 BCE ambapo waliishia kufanya makubaliano ya amani. Hivi mtu mjinga asiye na akili anaweza kuingia kwenye makubaliano ya kidiplomasia na taifa kama Roma kweli ???

Haya, wazungu wamefika zimbabwe (The Great Zimbabwe), wakaandika kwamba ule mji ulijengwa na wazungu kwasababu weusi wasingeweza kufanya hivyo. Kuna watu wanaamini mpaka leo hii kwamba The Great Zimbabwe haukujengwa na watu weusi. Mara ya kwanza Vasco Da Gama anaona rangi iliyopakwa ukutani (Colour Paint) ilikuwa ni kule Kilwa (The Kingdom of Kilwa), hapa nchini kwetu. Ifahamike kwamba Kilwa ilitengeneza hadi sarafu yake ambayo ipo kwenye makumbusho yake, lakini pia ilianzisha mahusiano ya kidiplomasia na Uchina (The Ming Dynasty) mnamo karne ya 14. Hivi watu wasio na akili wanaweza kutengeneza sarafu yao kweli, pamoja na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia ???

Aidha kuna kitu kimefichika, au waafrika mnajiona ni mapanzi kama ambavyo wapelelezi wa kihebrani walimwambia Nabii Mussa baada ya kutoka kule Kaanani.....Yote, tisa mzungu kafanikiwa sana kushika akili za mwafrika. Katika hili, alifanikiwa mno....
 
Tatizo liko kwenye culture na mind-set. Hivi vitu kuvibadilisha ni ngumu mno.
Tutabalishaje hiyo mind set? Tunakua na Rais mwenye PHD, anaongoza serikali nzima, na wananchi kwenda kupokea ndege airport karne ya leo! Wasted hours, wengine wanatoka Dodoma na magari ya serikali just kuja pokea ndege! Sasa huoni tu kuna vichwani mwetu haviko sawa!
 
Yote hayo sawa! Now what really happened? Hizo nadharia usizimeze nzima nzima! Hali tuliyonayo huwezi kusema ilisababishwa na ukoloni tu! Kuna la ziada ndani ya akili zetu.
 
Africa ina vituko sana, kuanzia juu mpaka chini
 
Usimkufuru Muumba wako, na wala usimdhihaki Mungu......
Lakini pia usiangalie historia ya dunia katika kurunzi ya karne za 17-21, huwezi kupata majibu sahihi.
Nina mengi sana ya kusema, lakini nadhani hatutaelewana kwasababu umeshaamini kwamba wewe ni duni.
 
Yote hayo sawa! Now what really happened? Hizo nadharia usizimeze nzima nzima! Hali tuliyonayo huwezi kusema ilisababishwa na ukoloni tu! Kuna la ziada ndani ya akili zetu.
Nakubaliana kabisa na wewe, kwamba matatizo ya Afrika, siyo ukoloni peke yake.....
Matatizo ya Afrika ni mengi mno, zaidi ya yale ya kiuchumi na kisiasa, japo sisi tunayazingatia tu haya mawili...
 
Siamini kabisa mimi ni duni! Ukweli unaonyesha sisi ni duni! Hizo elimu za waamisri! Na kina Mwanamutapa Zimbambwe zilienda wapi! Tumekutwa kwenye mapango ! Tumenunulia kwa gololi! Tumebadilishiwa culture etc.
Utasemaje? Are we superio?
 
Hizo Mwene Mutapa, Songhai, Mali Empire n.k kuzilinganisha na British Empire, Spanish au Mongol Empire ni sawa na kulinganisha kichuguu na mlima Kilimanjaro.

Angalia Legacy ya British na Spanish Empire duniani; Kingereza ni Lugha ya Kwanza, ikifuatia na Kihispania kuzungumzwa na jamii nyingi zaidi tofauti duniani. Wamesambaza dini ya Ukristo kote duniani, Wamesambaza mfumo wa sheria, uongozi, mavazi, mazao.

Nitajie hata legasi moja ya hizo himaya za Ki Africa hata kwetu watu weusi wenyewe.
 
teamWest vs teamEast , teamKobaz vs teamUpendo , teamUrusi vs TeamUkraine , team2Pac vs TeamBIG , hizi timu zote zipo miongon mwetu ila kiuhalisia hazituhusu ila kosa letu hatupendi vya ndani , the only smart race is ethiopians , those guys are royal to their ethnicity and race
 
Sidhani hata kama viongozi na walimu wengi wana ufahamu au uelewa wa umuhimu wa mlo bora kwa wanafunzi mashuleni. Wao watakuwa wanafahamu wanafunzi wanatakiwa wale wajaze tumbo tu.
 
personal priority na sio kigezo cha akili.
Na kwenye swala la mtu kuwa na mlin
Hii ipo Africa mno mkuu. Jaribu kuongea na watu walioishi nje kidogo ukienda kazini hujui boss Ni Nani wote wako on time Ila Sasa sie kidogo kacheo unataka uwe recognized. Huu Ni kweli usiopingika. Huwazi namna ya kuwekeza kwa kizazi chako Cha tano Ila unawaza hotel Kali,gari Kali, suti ya 10M ,wapambe wote Hawa unatoa hela na sio kuwa unaingiza.naona unakataa ukweli
 
Siamini kabisa mimi ni duni! Ukweli unaonyesha sisi ni duni! Hizo elimu za waamisri! Na kina Mwanamutapa Zimbambwe zilienda wapi! Tumekutwa kwenye mapango ! Tumenunulia kwa gololi! Tumebadilishiwa culture etc.
Utasemaje? Are we superio?
Waarabu walifanya haya yafuatayo katika historia yao:
1. Walianzisha hesabu za Algebra (Uniting broken parts)
2. Wao ndiyo walianzisha namba hasi (Negative Numbers), mtafute Omar Khayyam.
3. Wao ndiyo walianzisha mfumo wa tumia desimali kurekodi Sehemu (Decimal in recording fractions)
4. Wao ndiyo walianzisha hesabu za mchemraba (Cubic Equations), mtafute Omar Khayyam.
5. Wao ndiyo walifanikiwa kurekodi jamii 200 za mazao (Classification), mtafute Ibin Bassal.

Lakini nikuulize, hivi leo hii hawa waarabu ambao wameisaidia dunia hivi, wameweza kutengeneza hata gari au ndege yoyote ile zaidi ya kuuana ??? Tatizo ni nini ??? Utasema hawana akili ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…