Habari!
Mpaka leo natafakari hivi ni sababu za Kijiografia ndizo zimepelekea utofauti huu mkubwa wa akili baina ya Mwafrika na mtu mweupe?
Sometimes nahisi ni sababu za kibaiolojia (genetic factors) ndizo zimeweka mstari wa akili kati ya Mwafrika na mtu mweupe?
Narudi mezani napata jibu ni Mungu tu kwasababu zake mwenyewe ameamua kumpunja Mwafrika akili maana hata Waaafrika ambao wangezaliwa na kuishi huko Amerika na Asia hawaishiwi ulimbukeni na ushamba.
Nimewahi kufanya kazi na Wazungu Acacia, General manager alikuwa analipwa zaidi ya milioni 60 za Kitanzania kwa mwezi lakini alikuwa hataki kuitwa boss, alikuwa hana dereva wala body guard.
Nimewahi kufanya kazi na Wazungu pia huko Serengeti hotel moja ya gharama na nzuri sana. Ambayo 24 hrs gharama ya chini ilikuwa milioni 1.4 na sasa imepanda nasikia maana mimi niliacha baada ya kupata kibarua Serikalini. Hotel ambayo watu maarufu kama Bush, Beckham n.k hukosi kuwaona kule. Kule hakuna mtalii Mchina, Mhindi wala Mwafrika. Kule madoni walikuwa wanatumia mpaka milioni 20 per day.
General manager alikuwa analipwa pesa nyingi sana ila hakuwa na mlinzi kwake, alikuwa hataki kabisa kumuita boss.
Tukio la juzi la kuapishwa King Charles wa Uingereza mmeoana, hakuwa na mpambe wa kumsogezea daftari la mikataba, kiti alikisogeza mwenyewe.
Turudi Afrika sasa
•Kila mwanamuziki ambaye yuko kwenye chati tu mabody guards kama wote.
•Leo kazini msimamizi wako acha kumwita boss, muite jina lake la kawaida uone kama hutapewa kesi ya wizi wa mali za umma.
•Ufisadi na urasimu.
Afrika huwezi kusajili biashara siku moja, urasimu ni mwingi.
•Kesi inakaa mpaka miaka 7 ndo inatolewa hukumu hasa kesi ya mauaji. Baadaye mtuhumiwa anaachiwa huru kuwa hana hatia huku tayari kakaa mahabusu miaka 7. Mlipeni basi mabilioni ya kumfidia. Maana kumweka mtu ndani miaka saba si uuaji kabisa.
•Huku Afrika karibu kila Kiongozi wa nchi kila anaposimama au kukaa nyuma yake kuna AD kavaa nguo za kijeshi. Aibu sana.
Hatuja punjwa Akili mzee..ila tulizidiwa Akili wakati waarabu na wakoloni wanakuja kuchunguza Bara letu tukadhani wamekuja kwa nia njema bila kutafakari kwa kina ujio wao..Wazee na mababu zetu niseme na kuwaita walikuwa VILAZA, wapumbavu, wajinga na wakakosa umoja waka anza kusalitiana wao kwa wao...yani Machief wetu walishiriki kutoa taarifa nyingi sana na kuwapa wakoloni Kama taarifa za kiulinzi, majeshi,imani zao, walitoa taarifa zote muhimu na kuwa ambia waarabu na wazungu.
Sasa baada ya waarabu na wazungu kupata taarifa zote muhimu wakarudi kujipanga sasa kwa Uvamizi..wakajua udhaifu wetu ni kukosa umoja hivyo wakazidi kutugawa na kutugombanisha na kuchochea chuki baina yetu...Mfano mdogo tu Mangi mandara wa wachaga alishirikiana na wajerumani ili tu amzidi Mangi Meli kiutawala ..Huu si ujinga huu.!!!...
Wazungu wao ni wajanja sana toka zamani waliweka tofauti zao pembeni wakaungana kwenye kila nyanja kiuchumi, kiulinzi, kifedha..ndio maana leo hii kuna Umoja wa Nchi za Ulaya (EU),wana umoja wa kujihami NATO,makao yote makuu ya nchi zote yapo kwao United Nations (UN),Benki kuu ya dunia(WB), mashirika makubwa yote ya kielimu, kiafya yapo kwao....
Waafrika wenye Akili walikuwepo kina Muammar Gadaffi, Nkurumah, wanaharakati weusi kina Malcolm x, Martin Luther king Jr, Muhammad Ali, walitoa michango mikubwa sana kutaka AFRICA iungane tuwe kitu kimoja, sema kutokana na Akili za waafrika wengi zilivyo za kijinga, kimaskini, zenye chuki binafsi,ukabila,uchu wa madaraka Zinachangia kuzima na kukatisha tamaa za Waafrika wachache wenye Akili na upeo kuendeleza mapambano ya Afrika kuungana...mfano ni sisi wenyewe watanzania tulimpinga sana Magufuli kisa tu ali ingilia uhuru wa wahujumu uchumi,ajira hewa.. vibaraka wa wazungu.
Kwa ufupi ni kwamba mchawi wa Mwafrika ni mwafrika mwenyewe tangu zamani.