Kuamini kuwa hakuna historia ya Mwaafrika zaidi ya kuwa ni mtumwa ni mpangilio wa kum "brainwash" Mwaafrika na kumfanya ajione duni (inferior) siku zote.
Naamini kuwa historia ya Mwafrika ni zaidi ya utumwa ambao tunaaminishwa kuwa ni historia pekee iliopo na kwa ujuha wa wengi wetu tunaamini hilo kabisa (ushahidi, tazama kwa makini hii nyuzi). Mfumo wetu wa elimu tumeurithi kwa hao hao wanaotaka kutuaminisha kuwa Mwaafrika si lolote si chochote hadi hii leo.
Fungukeni muijuwe historia ya ukweli na mtaelewa kwamba hata watawala wa Kiafrika wa zamani walikuwa wana watumwa.
Ukiiingia historia kwa umakini utabaini kuwa ustaarabu wa awali duniani ulikuwa Afrika, mahekalu na majumba makubwa makubwa yalikuwa Afrika na watawala walikuwa Waafrika na watumwa walikuwa Waafrika na wengineo pia hapa hapa Afrika.
Waafrika walitawala mpaka baadhi ya Asia kwa miaka na miongo kadhaa na kuwa na watumwa wa kila aina (Soma kisa cha Queen of Sheba).
Soma vizuri historia ya Vasco Da Gama alipokuja, msafara wake uliikuta Kilwa imeendelea, ina majumba ya ghorofa yenye rangi, wakati Uropa walikuwa hawajui rangi ni nini, walikuta Waafrika wanatawala na wanafanya biashara mpaka China, wakati Uropa hata njia ya kwenda India tu walikuwa hawaijui.
Walikuta tayari Kilwa mpaka Sofala utawala wa Kiafrika wanatumia sarafu za dhahabu wakati wao hawakutegemea hilo. Walikuta Kilwa watu wanavaa hariri wakati wao walikuwa hawajui hariri ni nini! Isitoshe walikuta watu wanatumia sahani za kauri kutoka China (chinaware) wakati wao ndio mara ya kwanza wamezionea kauri Kilwa.
Walikuta majumba yanapambwa kwa tiles za vigae, kuanzia sakafu mpaka kuta mpaka dari ushahidi ni mabaki ya majumba Kilwa, (Kilwa ruins) ambayo mabaki hayo yamewekwa, yamefanywa kuwa kumbukumbu za kihistoria duniani (world historical heritage).
Yote hayo hatuyaoni wala hatuna haja ya kuyaona wala kuyachunguza zaidi kwa kuwa mrengo wa elimu tuliowachiwa na wakoloni (wazungu) na ndiyo tunayoiendeleza, umetufunika vichwa vyetu na kutujaza ujinga tujione kuwa Waafrika ni duni.
Bila kufunguwa vichwa vyetu na kuisaka na kuitafuta historia ya zaidi ya Mwaafrika kuwa ni mtumwa tu, hatutafunguka na tutaendelea kuwa Watumwa.
Nionavyo, utumwa wa Mwaafrika uko ndani ya vichwa zaidi, vilivyorubuniwa kuwa duni kwa kuaminishwa kuwa historia pekee iliopo ya Mwaafrika ni mtumwa. Naamini Afrika kuna historia kubwa zaidi ya utumwa.
Sijui kwanini mnaingizwa mkenge na wazungu ili mjione kuwa Waafrika siku zote ni duni na nyie mnaingia kichwa kichwa!
Miafrika Ndivyo Tulivyo -
Nyani Ngabu