Wanasiasa, wanaharakati, wanateolojia, wanafalsafa and so on ni change agents ktk mchakato wa kujenga nchi; kujenga nchi ni mradi wenye majukumu mengi, kila mmoja akianzia upande wake; hivyo, hakuna mwenye monopoly juu ya kila jukumu ktk mradi huu.
This being the case, can you reframe your point?
Sawa wote wanashiriki lakini hoja ipo kwa yupi anayeshika bendera ya badiliko likaleta tija kwa taifa.
Tazama leo na tangu 1993 imeonekana tume huru ni hoja ya kipinzani na si ya kinchi, sikatai maelezo yako mazuri ya awali lkn bado hayaonekani kuungwa mkono na wananchi wengi, achilia mbali sisi tunaojua
Ebu tueleze mtu mtambaswala, mpeta vvawa anajua tume tuliyonayo si huru kwa muktadha tunaojadili hapa?
Hoja ya kinchi ingeelezwa vizuri na watu wote katika kila pembe ya nchi, utasema sheria mpya ya azaki na kuzuia mikutano sawa, wanaharakati wengi hawajaiona hii kama ajenda ya kuitetea, wasomi hawajaona kama inamsingi kwa maisha yetu hivyo kugubikwa kuwa ya wanasiasa ambao Leo wanataka kuwaambukiza wanaharakati, wanAtaaluma, wanafalsafa na theologist ambapo inachukua muda kuungwa mkono hivyo kuchelewesha mchakato badala ya wanasiasa wangeichukua Leo ili kutekeleza
Na ndiyo maana nabaki na hoja yangu kuwa wanasiasa hutumiwa na wote hao kwa maslahi ya wengi kwani mwanasiasa akiianzisha tunatazama mengi na hasa maslahi yao zaidi badala ya umma, hivyo tunaamini hata Leo Mkipata nafasi ya kuunda tume mtaiunda kwa maslahi ya vyama vya siasa badala ya nchi na umma kwa kuwa wananchi hawajui wanataka chombo cha namna gani kutokana na ufinyu WA maarifa tume bora ya uchaguzi.
Kama jambo hili haliko kisiasa kwa nini marekebisho haya yaje Leo mkiacha marekebisho mengine muhimu kabisa hasa Muundo na uendeshaji WA bunge ambao ndiyo roho ya nchi?
Mkilitengeneza bunge likawa bora tutapata organs nzuri ya nchi na serikali.
Bunge letu ni LA hovyo kuliko hats hiyo tume ya uchaguzi. Tume bora tukiipata itatuletea tena wanasiasa tunaowabeza Leo na CCM dola itakuja kwa jina lingine kupitia chama kingine inaweza kuwa CDM dola hivyo kwangu sioni msingi WA ubatizo WA maji WA MTU mzima bila kitubio ongeza ubatizo WA roho.
Kiufupi, in kuwa, ninyi wanasiasa hamjaamua kuitengeneza Tanzania bora. Hivyo hata huu mkwamo uliopo Leo nahofu unaweza kutokea chini ya chama kingine na ndiyo maana nasema mabadiliko mnayotaka ni ya kisiasa bila wananchi.
We we kumbuka chadema ilipotumiwa na wasomi 2005-2015 ilikuwa matawi yapi? Hoja zilikuwa zinatoka ndani zinapata backup ya wananchi achilia mikutano lkn hoja nzito zenye maslahi ya wengi.
Kama kweli mnataka mngeamua basi kwa kuwatumia hao watu wakati ninyi mnaileta hoja hii basi kila pembe napo ikalipuka kupitia azaki, wanataaluma na theologist achilia muunganiko mficho WA maaskofu WA kilatini
Sent using
Jamii Forums mobile app