The Worst
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 8,855
- 28,752
Fungus katikati ya mapaja nadhani siyo kitu kigeni wala cha aibu kwa sisi wanaume nimeipitia hiyo hali japo siyo kwa kiwango chako,nilikuwa na ile ya kutoa unga unga unaotoa harufu mwanzo nikawa natumia limao na ndimu inaisha kwa muda ukipita mwezi inarudi.Tiba yake ni nin
Sasa nimejibunia dawa so far inanisaidia muda mrefu sana sijapata ile hali nadhani hata wewe itakusaidia au yeyote mwenye hili tatizo,njia ninazotumia ni
-Usafi wa mwili na nguo za ndani ni marufuku kurudia boxer.
-Nanyoa mavoozi kila baada ya siku kumi hii nimei-set sawa na siku ninazonyoa nywele sehemu nyengine za mwili.
-Chukua mafuta ya nazi yale ya watoto Minara changanya na Grislin ile wanayotumia kinamama kujipaka miguuni ili ilainike jizoeze kuyatumia baada ya kuoga asubuhi na jioni kila siku.
-Kuwa na vitaulo vya kujifuta maji huko chini ukitoka kuoga usitumie zaidi ya siku mbili viwe vimefuliwa,yaani ukitumia leo na kesho kifuliwe.
-Nyembe unazotumia kujinyoa usizirudie mara mbili pia unapooga jisuuze na maji safi hakikisha sabuni yote imeondoka maeneo hayo.
Nilichogundua ku-maintain usafi wa pumbu siyo kazi rahisi unaweza ukafanya yote kwa usahihi ila ukikosea kimoja tu inakuwa kazi bure,hizo dawa za tubes sijui cream sikushauri kutumia nadhani hizo ni kwa ajili ya wanawake labda na wazungu tu tumia njia niliyokupa itakusaidia.