Uungwana ni vitendo: Je, CHADEMA watarudisha Tsh. 38 milioni zilizotolewa na hayati Magufuli kumtoa Msigwa jela?


..nilichokiona ni Gerson Msigwa toka Ikulu na kaka yake Mchungaji Msigwa wakiwa wameambatana na mpiga video Issa Michuzi walikwenda mahakama ya Kisuti na risiti waliyodai ni malipo ya familia kumtoa ndugu yao.

..pia ilidaiwa kwamba Magufuli kama mwanafamilia amechangia sehemu ya fedha hizo.

NB:

..hili ni jambo la AIBU sana kwamba dhuluma za kisiasa za Magufuli zimepelekea mpaka mkwe wake kutiwa jela. Na zaidi yeye mwenyewe kulazimika kumtoa jela mkwe wake.
 
Magufuli hakuwa na fedha waliotoa ni wananchi kupitia mkono wa Magufuli.
 
Wakirejesha 38M, na mimi wanirejeshee 500K zangu.

Otherwise, 350M zote zitakaporejeshwa zielekezwe mahsusi katika gharama zinazohusiana na kampeni ya kudai katiba mpya.
 
Mahakama ndiyo inawajibika kumrudishia magufuli hela zake siyo chadema.

Tumia akili angalau kidogo kufikiri.
 
Haikuwa pesa yake au mshahara wake. Alijichotea hazina pesa ya walipa kodi kwa hivi itarudi kwa walipa kodi aka wananchi
 
Kama ni hivyo pesa si atarudishiwa Gerson Msigwa kwa niaba ya familia? Tatizo analoliona Yohana Mbatizaji liko wapi kama hakulipiwa kabisa na Chadema. Ila nakumbuka kama vile wakina Msigwa walipoenda kulipa walikuta Chadema wameishalipa. Kama itakuwa hivi, hela yao itakuwa ilirudishwa zamani sana.

Amandla...
 
Muongo sana wewe. Fedha walipewa CHADEMA au zililipwa mahakamani? Kama zililipwa aliyelipiwa si Mbowe, mtafute aliyelipa na aliyelipiwa akueleze vizuri. Uhakika ni kweli Msigwa alizikataa pesa za Magufuli kwa kisingizio cha undugu. Kama aliyelengwa alizikataa, kamuulize mwendazake alimlipia Mbowe kwa sababu gani?
Ila Mungu ni fundi sana kumuondoa mtu asiendelee na upuuzi wake.
 
Afadhali ungesema uDED

Enzi za Nyerere uDC walipewa madereva wastaafu wa CCM.

Hahahaaaa....... hahahaaaa...... hahahaaaa....... Lijualikali oyeeee!
Usitutajie kabisa huyo mtu, Uvccm hatuna hamu...nguvu, pesa na muda tuliotumia kukijenga na kupigania chama, leo mtu anaibuka tu anakuja kupewa udc, Uvccm tumepigwa....
 
Kwani hizo fedha zilikabidhiwa nani? Mahakama au CHADEMA?
 
Katika vitu vya kijinga ambavyo mtoa post huwa hutumii akili ni pamoja na hiyo post iliyojaa ushenzi wa kila aina,mjadala huu ukiufikiria kwa makini unatonesha vidonda kwa wanademokrasia,na hili ni jipu ambalo kutibika kwake ni kazi labda Yesu aje.
 
Ni waungwana

Watampa mjane wa marehemu
 
Haziwezi kurudishwa kwani ile ilikuwa rushwa ya kumrubuni Mch. Msigwa aisaliti Chadema. Kwetu ile tunaihesabu kuwa ni nyara tuliyoiteka uwanja wa vita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…