Swali langu ni jee wanafamilia wa Mswiga walikabidhi hizo pesa kwa Chadema au walilipa mojamoja kwa moja serikalini? Kama walikabidhi kwa Chadema, Chadema wanaweza kusema zilikuwa ni mchango wa pamoja wa kuwalipia faini wanachama wao na si mwanachama mmoja in particular. Ombi la Chadema lilikuwa ni kwa wanachama wao kwa ujumla wao na kila aliyechangia alijua hivyo. Kama ni hivyo Chadema watakuwa na haki ya kuzitumia kwa namna ambavyo wataona ina manufaa kwa chama. Ila wanafamilia wakidai warudishiwe basi bila shaka watawajibika kuwarudhia.
Lakini naona hapa tumeenda mbio sana. Wakina Yohana Mbatizaji wanataka watu waamini pesa zimeishatoka kama ilivyokuwa kwenye suala la ruzuku. Ni safari ndefu mpaka pesa zitoke. Na kuna uwezekano wasirudishiwe kabisa kama vile watumishi wanaoidai serikali wanavyofanyiwa. Wanataka tu kumwaga sumu.
Amandla....
..nilichokiona ni Gerson Msigwa toka Ikulu na kaka yake Mchungaji Msigwa wakiwa wameambatana na mpiga video Issa Michuzi walikwenda mahakama ya Kisuti na risiti waliyodai ni malipo ya familia kumtoa ndugu yao.
..pia ilidaiwa kwamba Magufuli kama mwanafamilia amechangia sehemu ya fedha hizo.
NB:
..hili ni jambo la AIBU sana kwamba dhuluma za kisiasa za Magufuli zimepelekea mpaka mkwe wake kutiwa jela. Na zaidi yeye mwenyewe kulazimika kumtoa jela mkwe wake.