Slobodan Mirosovich
Member
- Jan 9, 2026
- 40
- 196
Katika uchumi wa dunia akiba ya dhahabu ya nchi (National Gold Reserves) inatazamwa kama ngao ya mwisho ya uhuru wa kiuchumi. Taarifa kuwa nchi yangu Tanzania inapanga kuuza sehemu ya hazina yake ya dhahabu ili kufadhili miradi ya miundombinu imenistua sana.
Ni jambo linalopaswa kutafakariwa kwa kina na kila mzalendo , imekuwaje uzalishaji wa kila siku wa dhahabu nchini unashindwa kukidhi mahitaji ya ukwasi (Current Liquidity Needs), mpaka nchi ilazimike kugusa akiba ya kimkakati (Strategic Reserves) . Hatua hii si tu uamuzi wa kifedha, bali ni ishara tosha ya kupungua kwa uwezo wa serikali katika kusimamia uzani wa mapato na matumizi (Fiscal Deficit).
Dhahabu ni rasilimali inayoweza kugeuzwa kuwa fedha wakati wowote (Liquid Asset) na thamani yake haishuki kirahisi kama haya makaratasi mengine. Tunapouza akiba hii wakati sarafu yetu (Shilingi) ikiwa inapoteza nguvu dhidi ya dola ya Marekani, Kitaalamu, uamuzi huu unashusha uaminifu wa nchi mbele ya wakopeshaji wa kimataifa (Sovereign Creditworthiness) jambo ambalo linaweza kuifanya nchi ionekane inaelekea kufilisika (Insolvency)
Serikali inasema inauza dhahabu ili kujenga miundombinu. Hapa kuna fumbo kubwa la kiuchumi(opportunity cost). Miundombinu kama reli na barabara ni uwekezaji wa muda mrefu ambao unachukua miongo kadhaa kurudisha faida (Long term gestation period). Kwa upande mwingine, dhahabu inazidi kupanda thamani duniani kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi za Magharibi. Kuuza dhahabu inayopanda thamani ili kuwekeza kwenye long term investiments ni sawa na kutumia kiinua mgongo cha mafao kununua hiace ya biashara ambayo huna uhakika wa abiria hapa namaanisha hivi miundombinu mfano barabara na reli, ingawa ni muhimu, zinaanza kuchakaa (depreciate) siku ile tu zinapomalizika kujengwa. Zinahitaji mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo (maintenance costs). Pia, reli au barabara haianzi kuleta faida kesho inachukua miaka 20 hadi 30 kurudisha hata ile gharama ya ujenzi. Maana yake ni kwamba tunauza kitu ambacho kingetulinda dhidi ya mfumuko wa bei (dhahabu), ili tujenge kitu ambacho kitatugharimu pesa zaidi kukitunza (Reli/Barabara). Kwa lugha rahisi ni hivi Ikitokea dharura ya kitaifa kesho kama njaa(nimesema njaa maana mvua zimegoma) au vita, huwezi kuing'oa reli au barabara na kuiuza ili upate dola za kununua chakula au silaha. Lakini dhahabu unaiuza ndani ya dakika tano na kupata fedha. Tunapoteza uwezo wa kuwa na fedha mkononi (Liquidity) na kubaki na majengo/barabara ambazo haziwezi kutusaidia wakati wa dharura ya haraka.
Katika mazingira ya ukata wa fedha za kigeni (Forex Crunch), mara nyingi serikali hufanya maamuzi ya dharura chini ya shinikizo unajua serikali ya sasa kuna uwezakano wajanja washasoma gap la kupiga na kwakua Rais anaonekana kutokujali mambo basi anapenyezewa mkakati naye anaubaliki kama ulivyo.Swali la msingi ni je, uuzaji huu utafanyika kwa uwazi (Open Market Tender) au ni mikataba ya chini ya meza inayohusisha madalali (Middlemen)? Historia ya nchii hii inaonyesha kuwa rasilimali za taifa zinapouzwa kwa dharura kama wale twiga waliopanda ndege, nchi hupata hasara kubwa kupitia bei za michongo (Underpricing) huku kundi dogo la watu likinufaika na kamisheni nono si mnajua tena wanaomuongoza mheshimiwa ni watu wa aina gani?
Pindi hazina ya dhahabu inapopungua, imani ya soko kwa sarafu ya ndani huporomoka. Hii itapelekea kushuka zaidi kwa thamani ya Shilingi (Currency Devaluation). Kwa nchi inayotegemea kuingiza bidhaa nyingi kutoka nje kama yetu hii, bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya petroli, mitambo na dawa itapanda maradufu. Huu ni mnyororo unaosababisha mfumuko wa bei (Hyperinflation) ambao utamuumiza zaidi mwananchi wa hali ya chini tutarajie hili mda si mrefu
Uuzaji wa hazina ya dhahabu unapaswa kuwa hatua ya mwisho kabisa baada ya vyanzo vingine vyote kufeli. Badala ya kugusa akiba ya vizazi vijavyo. Serikali inapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (Austerity Measures) kama maposho ya kufuru safari za nje zisizo na maana magari ya anasa nk. Najua hapa hawapataki pia mtindo wa maisha wa ufahari usio na tija; kama Rais kuigiza sinema ni matumizi ya hovyo maana hakuna return yoyote kwenye utalii matokeo yake tunagusa hazina, kudhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia fedha za kigeni.
Kama wachumi na wazalendo wa Taifa hili, hatuwezi kukaa kimya wakati kibubu cha Taifa kikivunjwa ili kuziba mapengo yaliyosababishwa na usimamizi mbovu wa uchumi.Tunauza dhahabu maana yake vyanzo vingine vya Forex (Utalii, Mauzo ya mazao, Mikopo ya nje) vimeshindwa kukidhi mahitaji yetu kama kulipa madeni ya nje na kuagiza bidhaa na yote ni sababu ya uongozi mbovu na ulafi wa watu.KAMWENE