Uuzaji wa Akiba ya Dhahabu ni dalili mbaya ya kushindwa kwa dola

Uuzaji wa Akiba ya Dhahabu ni dalili mbaya ya kushindwa kwa dola

Dhahabu yenyewe kaanza Samia kununua mwaka 2023, bado mnamponda wakati kabla yake mlikuwa na Tani SUFURI. Hivi sasa ziko Tani 15, kuna ubaya gani kuuza kiasi wakati soko liko juu ili kuepuka kukopa kwenye commercial banks kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa miundombinu??
BOT ilianza kununua dhahabu tangu enzi za Mwinyi na Magufuli ndio aliweka misingi thabiti ya udhibiti wa madini ! sasa huyu kahaba amenunua nini ?
 
Katika uchumi wa dunia akiba ya dhahabu ya nchi (National Gold Reserves) inatazamwa kama ngao ya mwisho ya uhuru wa kiuchumi. Taarifa kuwa nchi yangu Tanzania inapanga kuuza sehemu ya hazina yake ya dhahabu ili kufadhili miradi ya miundombinu imenistua sana.

Ni jambo linalopaswa kutafakariwa kwa kina na kila mzalendo , imekuwaje uzalishaji wa kila siku wa dhahabu nchini unashindwa kukidhi mahitaji ya ukwasi (Current Liquidity Needs), mpaka nchi ilazimike kugusa akiba ya kimkakati (Strategic Reserves) . Hatua hii si tu uamuzi wa kifedha, bali ni ishara tosha ya kupungua kwa uwezo wa serikali katika kusimamia uzani wa mapato na matumizi (Fiscal Deficit).

Dhahabu ni rasilimali inayoweza kugeuzwa kuwa fedha wakati wowote (Liquid Asset) na thamani yake haishuki kirahisi kama haya makaratasi mengine. Tunapouza akiba hii wakati sarafu yetu (Shilingi) ikiwa inapoteza nguvu dhidi ya dola ya Marekani, Kitaalamu, uamuzi huu unashusha uaminifu wa nchi mbele ya wakopeshaji wa kimataifa (Sovereign Creditworthiness) jambo ambalo linaweza kuifanya nchi ionekane inaelekea kufilisika (Insolvency)

Serikali inasema inauza dhahabu ili kujenga miundombinu. Hapa kuna fumbo kubwa la kiuchumi(opportunity cost). Miundombinu kama reli na barabara ni uwekezaji wa muda mrefu ambao unachukua miongo kadhaa kurudisha faida (Long term gestation period). Kwa upande mwingine, dhahabu inazidi kupanda thamani duniani kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi za Magharibi. Kuuza dhahabu inayopanda thamani ili kuwekeza kwenye long term investiments ni sawa na kutumia kiinua mgongo cha mafao kununua hiace ya biashara ambayo huna uhakika wa abiria hapa namaanisha hivi miundombinu mfano barabara na reli, ingawa ni muhimu, zinaanza kuchakaa (depreciate) siku ile tu zinapomalizika kujengwa.

Zinahitaji mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo (maintenance costs). Pia, reli au barabara haianzi kuleta faida kesho inachukua miaka 20 hadi 30 kurudisha hata ile gharama ya ujenzi. Maana yake ni kwamba tunauza kitu ambacho kingetulinda dhidi ya mfumuko wa bei (dhahabu), ili tujenge kitu ambacho kitatugharimu pesa zaidi kukitunza (Reli/Barabara).

Kwa lugha rahisi ni hivi Ikitokea dharura ya kitaifa kesho kama njaa(nimesema njaa maana mvua zimegoma) au vita, huwezi kuing'oa reli au barabara na kuiuza ili upate dola za kununua chakula au silaha. Lakini dhahabu unaiuza ndani ya dakika tano na kupata fedha. Tunapoteza uwezo wa kuwa na fedha mkononi (Liquidity) na kubaki na majengo/barabara ambazo haziwezi kutusaidia wakati wa dharura ya haraka.

Katika mazingira ya ukata wa fedha za kigeni (Forex Crunch), mara nyingi serikali hufanya maamuzi ya dharura chini ya shinikizo unajua serikali ya sasa kuna uwezakano wajanja washasoma gap la kupiga na kwakua Rais anaonekana kutokujali mambo basi anapenyezewa mkakati naye anaubaliki kama ulivyo.

Swali la msingi ni je, uuzaji huu utafanyika kwa uwazi (Open Market Tender) au ni mikataba ya chini ya meza inayohusisha madalali (Middlemen)? Historia ya nchii hii inaonyesha kuwa rasilimali za taifa zinapouzwa kwa dharura kama wale twiga waliopanda ndege, nchi hupata hasara kubwa kupitia bei za michongo (Underpricing) huku kundi dogo la watu likinufaika na kamisheni nono si mnajua tena wanaomuongoza mheshimiwa ni watu wa aina gani?

Pindi hazina ya dhahabu inapopungua, imani ya soko kwa sarafu ya ndani huporomoka. Hii itapelekea kushuka zaidi kwa thamani ya Shilingi (Currency Devaluation). Kwa nchi inayotegemea kuingiza bidhaa nyingi kutoka nje kama yetu hii, bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya petroli, mitambo na dawa itapanda maradufu. Huu ni mnyororo unaosababisha mfumuko wa bei (Hyperinflation) ambao utamuumiza zaidi mwananchi wa hali ya chini tutarajie hili mda si mrefu

Uuzaji wa hazina ya dhahabu unapaswa kuwa hatua ya mwisho kabisa baada ya vyanzo vingine vyote kufeli. Badala ya kugusa akiba ya vizazi vijavyo. Serikali inapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (Austerity Measures) kama maposho ya kufuru safari za nje zisizo na maana magari ya anasa nk. Najua hapa hawapataki pia mtindo wa maisha wa ufahari usio na tija; kama Rais kuigiza sinema ni matumizi ya hovyo maana hakuna return yoyote kwenye utalii matokeo yake tunagusa hazina, kudhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia fedha za kigeni.

Kama wachumi na wazalendo wa Taifa hili, hatuwezi kukaa kimya wakati kibubu cha Taifa kikivunjwa ili kuziba mapengo yaliyosababishwa na usimamizi mbovu wa uchumi.Tunauza dhahabu maana yake vyanzo vingine vya Forex (Utalii, Mauzo ya mazao, Mikopo ya nje) vimeshindwa kukidhi mahitaji yetu kama kulipa madeni ya nje na kuagiza bidhaa na yote ni sababu ya uongozi mbovu na ulafi wa watu.KAMWENE
Kwani si tunachimba hizi dhahabu wenyewe? Tuweke nguvu kwenye uchimbaji wa dhahabu Mungu katujaalia kuwa hii dhahabu inapatikana kwenye ardhi yetu, ikiwa inatufaa basi tuitumie kwani kimfaacho mtu chake.
 
Ndugu jibu hoja acha uchawa. Hii kitu ina dalili kubwa ya ufisadi kutokana na ukweli kuwa hazina ya dhahabu ipo kwa ajili ya matukio makubwa amabayo yanaweza kuiingiza nchi katika anguko la uchumi.

Sasa katika hali ya utulivu nchi inafikia hatua ya kuuza rasilimali zake muhimu kama dhahabu. Je hiyo sio dalili tunaongozwa na watu wasiolitakia mema taifa? Labda nikutafsirie, huu ni wakati sahihi wa kuuza hiyo bidhaa muhimu ya taifa? Ndugu chawa usikurupuke uelewe kwanza
Mi naona wewe ndo umekurupuka sababu una elimu ya jf tu ambamo waelimishaji wake wakubwa ni haters wa Samia 🤣🤣🤣
 
Pengo la lawrence Mafuru limeanza kuonekana. Mleta mada umemaliza kila kitu.

Ipo shida kwenye matumizi pia ya.fedha inayopatikana kama inaliwa na.matask.force ya kuteka critics.

Mwigulu akiongea anakwambia nchi yetu ni tajiri sana. Na raisi aliyeongeza Gold reserve ni JPM sababu alikuwa anajua na.anapenda kufanya hivyo.
 
BOT ilianza kununua dhahabu tangu enzi za Mwinyi na Magufuli ndio aliweka misingi thabiti ya udhibiti wa madini ! sasa huyu kahaba amenunua nini ?
Enzi za Mwinyi kweli walianzisha, lakini walifeli kwa kuwa mifumo haikuwa mizuri. Wenye nia mbaya waliuza dhahabu feki. Magufuli alianzisha masoko ya ndani ambapo wachimbaji wadogo wadogo wanauza kwenye masoko ya Serikali. Mpaka Magufuli anakufa hatukuwa na hata kilo moja ya dhahabu
 
Ipo tu siku taifa zima tutakuja kuelewa kuwa hatukuwa na usalama wa taifa tulikuwa na genge la wahuni tu la kuiibia nchi huku hicho kikundi kikiwalinda wezi wa rasilimali za nchi.
Hiyo taasis inafaidika indirectly na mpango huo. Is why watafanya lolote ili wabaki madarakani

But one day watoto wetu wats wonder ilikuwaje tuka ruhusu serikali aina hii
 
Sababu ya kuuza ni moja tuu, hatuna dollar za kuagiza petrol na vyakula, petrol tunaagiza 100% , ngano tunaagiza karibu tani milioni moja kila mwaka, vikikosekana hivyo vitu nchi haitakalika, kwa sasa beberu na utalii vimekata hakuna dollar na treasury imekauka, only solution ni kuuza dhahabu tuu, kwa wiki mbili tuu shilingi imeanguka kutoka 2400 installers 2600, na madeni lazima yalipwe mengi in dollars na huwezi default la sivyo tutageuka Zimbabwe soon, na kuuza dhahabu ni temporary solution tuu akiba ni ndogo, only permanent solution ni kukaa chini na wapinzani na beberu ili dollar na utalii virudi, trillion 3 za TRA ni mashilingi tuu huwezi fanyia kitu na hakuna nchi inaweza kukuuzia chochote
Mkuu, mbona kama unataka kutuaminisha kuwa zile tuzo tatu za kimataifa alizopokea Rais ni feki'? Kama Tanzania ni kitovu cha utalii na Royal Tour ilifungua milango ya watalii rundo hizo dola zimeenda mfukoni mwa nani mpaka tukauze dhahabu yetu?
 
Katika uchumi wa dunia akiba ya dhahabu ya nchi (National Gold Reserves) inatazamwa kama ngao ya mwisho ya uhuru wa kiuchumi. Taarifa kuwa nchi yangu Tanzania inapanga kuuza sehemu ya hazina yake ya dhahabu ili kufadhili miradi ya miundombinu imenistua sana.

Ni jambo linalopaswa kutafakariwa kwa kina na kila mzalendo , imekuwaje uzalishaji wa kila siku wa dhahabu nchini unashindwa kukidhi mahitaji ya ukwasi (Current Liquidity Needs), mpaka nchi ilazimike kugusa akiba ya kimkakati (Strategic Reserves) . Hatua hii si tu uamuzi wa kifedha, bali ni ishara tosha ya kupungua kwa uwezo wa serikali katika kusimamia uzani wa mapato na matumizi (Fiscal Deficit).

Dhahabu ni rasilimali inayoweza kugeuzwa kuwa fedha wakati wowote (Liquid Asset) na thamani yake haishuki kirahisi kama haya makaratasi mengine. Tunapouza akiba hii wakati sarafu yetu (Shilingi) ikiwa inapoteza nguvu dhidi ya dola ya Marekani, Kitaalamu, uamuzi huu unashusha uaminifu wa nchi mbele ya wakopeshaji wa kimataifa (Sovereign Creditworthiness) jambo ambalo linaweza kuifanya nchi ionekane inaelekea kufilisika (Insolvency)

Serikali inasema inauza dhahabu ili kujenga miundombinu. Hapa kuna fumbo kubwa la kiuchumi(opportunity cost). Miundombinu kama reli na barabara ni uwekezaji wa muda mrefu ambao unachukua miongo kadhaa kurudisha faida (Long term gestation period). Kwa upande mwingine, dhahabu inazidi kupanda thamani duniani kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi za Magharibi. Kuuza dhahabu inayopanda thamani ili kuwekeza kwenye long term investiments ni sawa na kutumia kiinua mgongo cha mafao kununua hiace ya biashara ambayo huna uhakika wa abiria hapa namaanisha hivi miundombinu mfano barabara na reli, ingawa ni muhimu, zinaanza kuchakaa (depreciate) siku ile tu zinapomalizika kujengwa. Zinahitaji mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo (maintenance costs). Pia, reli au barabara haianzi kuleta faida kesho inachukua miaka 20 hadi 30 kurudisha hata ile gharama ya ujenzi. Maana yake ni kwamba tunauza kitu ambacho kingetulinda dhidi ya mfumuko wa bei (dhahabu), ili tujenge kitu ambacho kitatugharimu pesa zaidi kukitunza (Reli/Barabara). Kwa lugha rahisi ni hivi Ikitokea dharura ya kitaifa kesho kama njaa(nimesema njaa maana mvua zimegoma) au vita, huwezi kuing'oa reli au barabara na kuiuza ili upate dola za kununua chakula au silaha. Lakini dhahabu unaiuza ndani ya dakika tano na kupata fedha. Tunapoteza uwezo wa kuwa na fedha mkononi (Liquidity) na kubaki na majengo/barabara ambazo haziwezi kutusaidia wakati wa dharura ya haraka.

Katika mazingira ya ukata wa fedha za kigeni (Forex Crunch), mara nyingi serikali hufanya maamuzi ya dharura chini ya shinikizo unajua serikali ya sasa kuna uwezakano wajanja washasoma gap la kupiga na kwakua Rais anaonekana kutokujali mambo basi anapenyezewa mkakati naye anaubaliki kama ulivyo.Swali la msingi ni je, uuzaji huu utafanyika kwa uwazi (Open Market Tender) au ni mikataba ya chini ya meza inayohusisha madalali (Middlemen)? Historia ya nchii hii inaonyesha kuwa rasilimali za taifa zinapouzwa kwa dharura kama wale twiga waliopanda ndege, nchi hupata hasara kubwa kupitia bei za michongo (Underpricing) huku kundi dogo la watu likinufaika na kamisheni nono si mnajua tena wanaomuongoza mheshimiwa ni watu wa aina gani?

Pindi hazina ya dhahabu inapopungua, imani ya soko kwa sarafu ya ndani huporomoka. Hii itapelekea kushuka zaidi kwa thamani ya Shilingi (Currency Devaluation). Kwa nchi inayotegemea kuingiza bidhaa nyingi kutoka nje kama yetu hii, bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya petroli, mitambo na dawa itapanda maradufu. Huu ni mnyororo unaosababisha mfumuko wa bei (Hyperinflation) ambao utamuumiza zaidi mwananchi wa hali ya chini tutarajie hili mda si mrefu

Uuzaji wa hazina ya dhahabu unapaswa kuwa hatua ya mwisho kabisa baada ya vyanzo vingine vyote kufeli. Badala ya kugusa akiba ya vizazi vijavyo. Serikali inapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (Austerity Measures) kama maposho ya kufuru safari za nje zisizo na maana magari ya anasa nk. Najua hapa hawapataki pia mtindo wa maisha wa ufahari usio na tija; kama Rais kuigiza sinema ni matumizi ya hovyo maana hakuna return yoyote kwenye utalii matokeo yake tunagusa hazina, kudhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia fedha za kigeni.

Kama wachumi na wazalendo wa Taifa hili, hatuwezi kukaa kimya wakati kibubu cha Taifa kikivunjwa ili kuziba mapengo yaliyosababishwa na usimamizi mbovu wa uchumi.Tunauza dhahabu maana yake vyanzo vingine vya Forex (Utalii, Mauzo ya mazao, Mikopo ya nje) vimeshindwa kukidhi mahitaji yetu kama kulipa madeni ya nje na kuagiza bidhaa na yote ni sababu ya uongozi mbovu na ulafi wa watu.KAMWENE
ROSTAM AZIZI NI MSHENZI SANA
 
mada nzuri here are your answers:
1) Dhahabu ziliwekwa kama akiba, na akiba kazi yake kutumika wakati wa majanga, but uzuri ni hio hio dhahabu inachimbwa ndan sio kwamba tunaenda kununua

2) Miradi lazima iendelee, kuna competition kali sana ya biashara kwenye region yetu tukizubaa basi inakula kwetu,
3) Alternative ingine ni kukopa, ukitaka kujua madhara yake nenda kenya apo
Ona kenge hili! Kwa hiyo kwa kuwa dhahabu inachimbwa hapa Tanzania serikali hainunui inachukuwa bure?

Shithole!
 
Kukosa gavana wa benki sahihi, mwenye uzoefu na kutoa ushauri sahihi kwa serikali inaweza kuwa sababu ya upigaji mnada hifadhi ya dhahabu ifanyike.

Pengine uteuzi wa gavana dhaifu asiye na uzoefu ilikuwa ni mpango mkakati wa mamlaka za uteuzi kufanya dili zao

Pengine Idara muhimu, wizara, idara maalumu zina ugonjwa wa kupoteza Kumbukumbu za Kitaasisi, kwa kubadilisha wakuu wenye maamuzi kila mara na hivyo kumbukumbu za Kitaasisi kupotea na hivyo ufisadi au maamuzi yasiyo sahihi kuweza kupata nafasi ya kufanyika kwa makusudi ah kimkakati :

Thamani ya kumbukumbu ya kitaasisi​

Mei 15, 2025​

Mnamo 1978, genge la wasafishaji mfereji mkubwa (canal) lililofanya kazi ya mkandarasi kampuni ya British Waterways lilikuwa likipambana na tatizo. Walikuwa wakijaribu kuondoa vikwazo kwenye Mfereji wa Chesterfield ili waweze kuimarisha ukuta wa zege — haikuwa kazi rahisi ya siku moja. Lakini kilichowakwamisha hasa ni mnyororo mzito wa chuma ukijikita chini ya mfereji. Baada ya majaribio mbalimbali, waliunganisha mnyororo huo kwenye mashine yao ya kusafisha mfereji mkubwa. Hilo lilifanikiwa. Kwa kuvuta kwa nguvu mnyororo huo na kipande cha mbao kilichokuwa mwisho wake viliondolewa. Genge hilo baada ya kufanikiwa kupambana kuondoa mnyororo huo wa chuma lilichukua kujipongeza kwa mapumziko mazuri kwa ajili ya chai.

Kipindi chao cha mapumziko ya chai kilikatizwa kwa yowe kali kutoka kwa polisi aliyekuwa katika hali ya taharuki kubws. Polisi huyo kwa bahati tu alikuwa akipita kwenye njia ya maji ambayo kwa kawaida ilikuwa tulivu aliposhindwa kujizuia kuona kidimbwi kikubwa cha maji yanayozunguka kwa kasi kubwa. Wakati wafanyakazi waliporudi eneo la tukio kwa spidi kubwa, wakakuta mfereji ulikuwa umetoweka. "Hatukujua kulikuwa na plagi," mfanyakazi mmoja alilalamika kwa kujitetea. Na, kwa haki, mfereji ulikuwa na umri wa karne mbili, na plagi pia.

Kumbukumbu zozote zilizokuwepo za mfereji huo zilikuwa zimeharibiwa katika mashambulizi vita kuu ya pili ya dunia (Blitz).

Maadili ya hadithi: kumbukumbu ya kitaasisi ni muhimu (institutional memory), na ikiwa shirika litaanza kusahau mambo muhimu (kama vile uwepo wa plagi), mambo mabaya hutokea. Utaalamu hupungua kwa kasi ya kutisha ikiwa hautaboreshwa na kuwa re-set.

Hata hivyo, si rahisi. Hivi majuzi nilichukuliwa kwenye ziara ya mkusanyiko wa picha za Maktaba ya Bodleian, na nilishangazwa na jinsi waongozaji wetu wa watalii walivyolazimika kufanya kazi kwa bidii ili kupata taarifa za msingi kuhusu mlezi na msanii, hata katika picha zenye umri wa miongo michache tu.

Hili halingekuwa la kushangaza sana, isipokuwa kwamba sababu nzima ya Maktaba ya Bodleian kuwepo ni kuhifadhi taarifa katika mfumo unaoweza kufikiwa. (Mkutubi wa Bodley, Richard Ovenden, ameandika Burning the Books: A History of the Deliberate Destruction of Knowledge na ni rais wa Muungano wa Uhifadhi wa Kidijitali.) Lakini Bodleian ni maktaba, si jumba la makumbusho la picha, na bila uangalifu wa mara kwa mara kutuza kubukumbu au historia, mpangilio wa asili wa mambo kwa watu si wa kukumbuka mambo, bali wa kusahau.

Hilo linamaanisha shida. Fikiria kashfa mbaya ya Volkswagen VW, ambapo kampuni ilibuni magari yake ili kupumbaza vipimo vya uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa wasimamizi. Hapana, si kashfa ya 2015, ambayo iliigharimu kampuni sifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wake kutimuliwa na zaidi ya euro bilioni 30 katika faini, kulipa madai na faini za kisheria.

Namaanisha kashfa ya 1973, ambapo VW ilishutumiwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Mazingira la Marekani kwa kubuni magari yake ili kupumbaza vipimo vya uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa wasimamizi. Mwaka 1973 VW ilikubaliana kulioa fidia nje ya mahakama na, inaonekana, baadaye tena 2015 ilitumia miongo iliyofuata ikarudia kosa lile la 1973 ambalo kama Kumbukumbu za Kitaasisi zisinge sahauliwa, uzoefu wa adhabu VW iliyopewa 1973 ungeweza kuiokoa VW na kosa la 2015.

Mfano wa kusikitisha zaidi ni milipuko miwili mibaya ya Space Shuttle, Challenger mwaka wa 1986 na Columbia mwaka wa 2003. Ajali hizi zinaonekana tofauti sana. Moja ilikuwa mlipuko muda mfupi baada ya kupaa, nyingine ilikuwa kuvunjika kwa chombo hicho kilipokuwa kinarejea kutoa anga za juu kuingia anga ya dunia. Lakini makosa ya msingi yaliyowezesha yanaonekana kufanana sana. Ripoti ya Bodi ya Uchunguzi wa Ajali za Columbia ilibainisha kuwa maswali yaleyale ya msingi yaliibuka: kwa nini shuttle zote mbili ziliendelea kuruka zikiwa na matatizo yanayojulikana? Na kwa nini mameneja wa Nasa waliamua kwamba ilikuwa salama kuruka licha ya maonyo kutoka kwa wahandisi wao? Ili kuandaa mazingira ya Columbia, NASA ilibidi isahau masomo yote ya Challenger na hilo ni moja ya kupotea kwa Kumbukumbu za Kitaasisi.

Kuna zaidi ya kusahau taasisi kuliko kusahau jambo moja kubwa, iwe ni "ukiidanganya EPA, wanaweza kuigundua" au "mfereji una shimo la kuziba". Mashirika yanaweza pia kusahau jinsi ya kufanya mambo.

Thamani ya kumbukumbu ya kitaasisi
Mei 15, 2025
Mnamo 1978, genge la wachimbaji madini lililofanya kazi kwa British Waterways lilikuwa likipambana na tatizo. Walikuwa wakijaribu kuondoa vikwazo kwenye Mfereji wa Chesterfield ili waweze kuimarisha ukuta wa zege — haikuwa kazi rahisi ya siku moja. Lakini kilichowakwamisha hasa ni mnyororo mzito wa chuma chini ya mfereji. Baada ya majaribio mbalimbali, waliunganisha mnyororo huo kwenye mashine yao ya kuchimba madini. Hilo lilifanikiwa. Kwa kuvuta kwa nguvu mnyororo huo na kipande cha mbao kilichokuwa mwisho wake viliondolewa. Genge hilo lilichukua mapumziko mazuri kwa ajili ya chai.

Kipindi cha chai kilikatizwa kwa ukali na polisi akiwa katika hali ya msisimko. Alikuwa akipita kwenye njia ya maji ambayo kwa kawaida ilikuwa tulivu aliposhindwa kujizuia kuona kidimbwi kikubwa cha maji. Kufikia wakati wafanyakazi waliporudi eneo la tukio, mfereji ulikuwa umetoweka. "Hatukujua kulikuwa na plagi," mfanyakazi mmoja alilalamika. Na, kwa haki, mfereji ulikuwa na umri wa karne mbili, na plagi pia. Kumbukumbu zozote zilizokuwepo zilikuwa zimeharibiwa katika Blitz. Maadili ya hadithi: kumbukumbu ya kitaasisi ni muhimu, na ikiwa shirika litaanza kusahau mambo muhimu (kama vile uwepo wa plagi), mambo mabaya hutokea. Utaalamu hupungua kwa kasi ya kutisha ikiwa hautaboreshwa na shughuli.

Hata hivyo, si rahisi. Hivi majuzi nilichukuliwa kwenye ziara ya mkusanyiko wa picha za Maktaba ya Bodleian, na nilishangazwa na jinsi waongozaji wetu wa watalii walivyolazimika kufanya kazi kwa bidii ili kupata taarifa za msingi kuhusu mlezi na msanii, hata katika picha zenye umri wa miongo michache tu. Hili halingekuwa la kushangaza sana, isipokuwa kwamba sababu nzima ya Maktaba ya Bodleian kuwepo ni kuhifadhi taarifa katika mfumo unaoweza kufikiwa. (Mkutubi wa Bodley, Richard Ovenden, ameandika Burning the Books: A History of the Deliberate Destruction of Knowledge na ni rais wa Muungano wa Uhifadhi wa Kidijitali.) Lakini Bodleian ni maktaba, si jumba la makumbusho la picha, na bila uangalifu wa mara kwa mara, mpangilio wa asili wa mambo si wa kukumbuka, bali wa kusahau.

Hilo linamaanisha shida. Fikiria kashfa mbaya ya Volkswagen, ambapo kampuni ilibuni magari yake ili kupumbaza vipimo vya uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa wasimamizi. Hapana, si kashfa ya 2015, ambayo iliigharimu kampuni sifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wake na zaidi ya euro bilioni 30 katika faini, suluhu na ada za kisheria. Namaanisha kashfa ya 1973, ambapo VW ilishutumiwa na Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani kwa kubuni magari yake ili kupumbaza vipimo vya uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa wasimamizi. VW ilikubaliana nje ya mahakama na, inaonekana, ilitumia miongo iliyofuata ikisahau kile ambacho kingekuwa uzoefu wa adhabu.

Mfano wa kusikitisha zaidi ni milipuko miwili mibaya ya Space Shuttle, Challenger mwaka wa 1986 na Columbia mwaka wa 2003. Ajali hizi zinaonekana tofauti sana. Moja ilikuwa mlipuko muda mfupi baada ya kupaa, nyingine ilikuwa kuvunjika kwa kuingia tena. Lakini makosa ya msingi yaliyowezesha yanaonekana kufanana sana. Ripoti ya Bodi ya Uchunguzi wa Ajali za Columbia ilibainisha kuwa maswali yaleyale ya msingi yaliibuka: kwa nini shuttle zote mbili ziliendelea kuruka zikiwa na matatizo yanayojulikana? Na kwa nini mameneja wa Nasa waliamua kwamba ilikuwa salama kuruka licha ya maonyo kutoka kwa wahandisi wao? Ili kuandaa mazingira ya Columbia, Nasa kwanza ilibidi isahau masomo yote ya Challenger.

Kuna zaidi ya kusahau taasisi kuliko kusahau jambo moja kubwa, iwe ni "ukiidanganya EPA, wanaweza kuigundua" au "mfereji una shimo la kuziba". Mashirika yanaweza pia kusahau jinsi ya kufanya mambo.

Nikiwa kijana nilivutiwa na ndege ya Lockheed TriStar kwa sababu ya umbo lake lisilo la kawaida, ikiwa na injini moja mkiani. Huioni sana siku hizi — TriStar haikuwa na mafanikio ya kibiashara.

Sikuwa mtu pekee niliyevutiwa na ndege hiyo, lakini mwanasaikolojia wa shirika Linda Argote alikuwa na sababu tofauti ya kuichunguza. Ndege nyingi hupata bei nafuu zaidi kutengeneza kwa faida ya uzoefu — ni mfano halisi wa kujifunza kwa kufanya. Lakini TriStar ilibaki kuwa ghali kutengeneza. Argote alitaka kujua ni kwa nini. Wazo lake lilibadilisha wazo la kujifunza kwa kufanya: vipi kuhusu kusahau kwa kutofanya?

Katika makala ya mwaka wa 1990, Argote na Dennis Epple walihitimisha kwamba kampuni ya Lockheed lilikuwa limetengeneza ndege chache sana kiasi kwamba walikuwa wakisahau haraka kuliko walivyokuwa wakijifunza. Hasa, mwaka wa 1977 na 1978 uzalishaji ulishuka hadi TriStars 14 pekee kwa jumla, na kufikia mwanzoni mwa miaka ya 1980 gharama halisi zilikuwa juu kuliko mwaka wa 1975.

Mwanauchumi Lanier Benkard baadaye alikadiria kwamba utaalamu wa Lockheed wa kuokoa gharama ulipungua kwa kasi ya kutisha ikiwa haukuboreshwa na shughuli, na nusu ya maisha ya zaidi ya mwaka mmoja. Hatuwezi kujumlisha mengi kutoka kwa hilo. Ndege ni ndege, na kila kesi ni tofauti. Hata hivyo, mtu yeyote ambaye amewahi kuwasilisha marejesho ya kodi anaweza kuthibitisha kwamba mwaka ni muda wa kutosha kusahau jinsi ya kufanya mchakato wowote mgumu.

Kusahau kunaweza kutokea kwa sababu nyingi. Watu huondoka. Kumbukumbu halisi zinaweza kuathiriwa na ukungu na moto na kupotea. Kumbukumbu za kidijitali huwa hazisomeki kadri teknolojia inavyobadilika - kwa kweli marejeleo ya mwisho katika ingizo la Wikipedia kuhusu kumbukumbu ya shirika ni kiungo kisicho na maana kwa tovuti iliyopotea ya NHS. Na wakati mwingine mashirika husahau kimakusudi. Sababu kuu ya kashfa ya Windrush nchini Uingereza ilikuwa kwamba sehemu moja ya Ofisi ya Mambo ya Ndani idara ya Uhamiaji iliamua kutoa madai magumu kwamba wakazi wa Uingereza wathibitishe kuwa wana haki ya kuishi na kufanya kazi nchini, bila kujua - au kujali sana - kwamba sehemu nyingine ya Ofisi ya Mambo ya Ndani ilikuwa imeharibu rekodi zilizowezesha uthibitisho huo.

Zaidi ya kurasa 100,000 za serikali ya Marekani zilitoweka baada ya Rais Trump kuchukua madaraka. Bado haijabainika ni nini kimetoweka kwa muda na ni nini kimepotea milele.

Ni rahisi kwa mashirika kusahau, hata wanapojaribu kukumbuka. Tusifanye hili kuwa baya zaidi kuliko linavyopaswa kuwa, la sivyo litakuwa zaidi ya Mfereji wa Chesterfield tunaoupoteza.

Imeandikwa kwa ajili ya na kuchapishwa kwa mara ya kwanza katika Financial Times mnamo tarehe 18 Aprili 2025

Ni rahisi kwa mashirika kusahau, hata wanapojaribu kukumbuka. Tusifanye hili kuwa baya zaidi kuliko linavyopaswa kuwa, la sivyo litakuwa zaidi ya Mfereji wa Chesterfield tunaoupoteza.

Imeandikwa kwa ajili ya na kuchapishwa kwa mara ya kwanza katika Financial Times mnamo tarehe 18 Aprili 20 na watu wa 'control' wakiondolewa ghafla wakati mali za kampuni au nchi (dhahabu) zinapoanza kuuzwa kiholela, ujue kuna mtu amekataa kuweka saini kwenye madili yasiyo na tija
Badiliko la gafla la mzoefu na mtaalamu naibu gavana anayehusika na udhibiti ndugu Julian Banzi Raphael na kumweka mtu wa haiba moja kuanzia lahaja hadi ufikili wakati mali ya nchi (dhahabu) inapoanza kuuzwa kiholela, ujue tu kuna mtu amekataa kuweka saini kwenye madili yasiyo na tija kwa Taifa haikua coincidence kumpachika Dkt. Rahma Salim Mahfoudh kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani mda utasema
 
Dhahabu yenyewe kaanza Samia kununua mwaka 2023, bado mnamponda wakati kabla yake mlikuwa na Tani SUFURI. Hivi sasa ziko Tani 15, kuna ubaya gani kuuza kiasi wakati soko liko juu ili kuepuka kukopa kwenye commercial banks kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa miundombinu??
Dhahabu yenyewe kaanza Samia kununua mwaka 2023, bado mnamponda wakati kabla yake mlikuwa na Tani SUFURI. Hivi sasa ziko Tani 15, kuna ubaya gani kuuza kiasi wakati soko liko juu ili kuepuka kukopa kwenye commercial banks kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa miundombinu??
Ninyi ni moja ya watu mnaohusika kumpoteza mh, ni dhahiri hujui tofauti ya hazina ya taifa na pochi au account binafsi ya Samia , Rais hajatoa hela mfukoni kwake kununua hizo tani 15 ametoa kodi zetu na rasilimali zetu kupitia BoT. Hivyo, hiyo dhahabu ni dhamana ya Taifa (National Sovereign Reserve). Huwezi kuanza kuuza akiba ya uzee ukiwa bado una nguvu ya kufanya kazi ndo point yangu.Pia Kama kila kitu kiko shwari na ni halali kuuza, kwanini mlinzi mkuu wa Udhibiti wa Ndani (Internal Control) pale BoT, Julian Banzi Raphael, aondolewe ghafla? Katika taaluma ya usimamizi vijana wa Assad watakua wananielewa, ukiona mhasibu au mdhibiti anabadilishwa katikati ya zoezi la kuuza mali za kampuni, ujue kuna harufu ya wizi jikoni. Labda Banzi alikataa kufuata hiyo mantiki ya watu wa aina yako "si alinunua mwenyewe, auze tu?
 
Naongezea....

Kumbuka kabla ya Samia BOT ilikuwa hainunui gold. Tumeanza kununua mwaka 2023 kwa mikakati yake na sasa tuna tani 15. Kuna ubaya gani kuiuza kiasi kipindi hiki ambacho gold imepanda kwa zaidi ya 60% soko ili ku finance ujenzi wa miundombinu?? Mikakati ni ya kwake ndiye aliyeanzisha kununua. Na siyo vibaya kuuza kiasi kuliko kwenda kukopa kwenye mabenki kwa ajili ya kujenga hiyo miundombinu
KUmbe tumeanza kununua 2023?
 
Niliwahi kuwashauri wanaharakati sababu serikali haitambuliki, wafungue kesi kuzuia serikali batili kutumia hazina ya serikali ya Tanzania kama raid wa Venezuela Maduro alivyozuiliwa kutumia hazina yao ya dhahabu ila wao wameendelea kutumia mikakati ileile iliyozuiliwa.
 
Hivi hii nchi imeanza kukusanya dhahabu kama hazina tangu lini nadhani hata miaka 5 nyuma inaweza isifike … leo hii watu wanajifanya wanachambua hasara na faida lengo la kukusanya lilikua nini ? Ukilifahamu huwezi kushangaa na hii move ya kuuza
 
Back
Top Bottom