Uuzaji wa Akiba ya Dhahabu ni dalili mbaya ya kushindwa kwa dola

Uuzaji wa Akiba ya Dhahabu ni dalili mbaya ya kushindwa kwa dola

TRAORE AFUTILIA MBALI VYAMA VYA SIASA NA KUTAIFISHA MALI ZOTE ZA VYAMA. IPO SIKU CCM NAYO ITAKUBWA NA DECREE HII KUTOKANA NA UHUJUMU UCHUMI NA UMOJA WA TAIFA

29 January 2026
Ouagadougou, Burkina Faso

Burkina Faso Yavunja Vyama vya Siasa Huku Kapteni Ibrahim Traoré , Akiamuru mali zote za vyama kutaifishwa​

1769776441534.jpeg

Serikali ya Kapteni Traore inasema kwamba mfumo wa vyama vingi, kama ulivyobadilika, umekuwa chanzo cha mgawanyiko badala ya mshikamano wa kitaifa.
Serikali inayoongozwa na jeshi la Burkina Faso imetangaza kuvunjwa kwa vyama vyote vya siasa na miundo, uamuzi mkubwa unaosisitiza mabadiliko makubwa ya kisiasa ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traoré na mradi unaoendelea wa kile ambacho mamlaka inakielezea kama "ujenzi mpya wa serikali."

Uamuzi huo ulichukuliwa Alhamisi wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri, ambapo amri ya kufuta rasmi vyama vya siasa ilipitishwa. Maafisa wa serikali wanasema kwamba mfumo wa vyama vingi, kama ulivyobadilika, umekuwa chanzo cha mgawanyiko badala ya mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri wa Utawala wa Maeneo na Uhamaji Émile Zerbo alisema kuongezeka kwa vyama vya siasa kumedhoofisha mfumo wa kijamii na kudhoofisha umoja wakati ambapo nchi inakabiliwa na changamoto za usalama wa maisha.

View: https://m.youtube.com/watch?v=rgHQbd2z-nM
"Uamuzi huu mkubwa na muhimu unaangukia ndani ya mfumo wa kuanzishwa upya kwa serikali na unafuata utambuzi wa kina wa mfumo wa vyama," Zerbo alisema. "Utambuzi huo ulionyesha tofauti nyingi katika matumizi ya utawala wa kisheria unaotawala vyama vya siasa na miundo."

Kiongozi wa Mapinduzi Mwenye Rufaa ya Watu

Kuvunjwa kwa vyama kunakuja huku Kapteni Ibrahim Traoré akiendelea kufurahia uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa makundi makubwa ya jamii ya Burkinabè, hasa miongoni mwa vijana, makundi ya kiraia yanayoendana na mpito, na harakati za Pan-Africanist kote barani Afrika na watu wanaoishi nje ya nchi.

Tangu achukue madaraka, Traoré amejenga taswira ya mwanajeshi-kiongozi wa mapinduzi aliyeazimia kuachana kabisa na kile ambacho wengi nchini Burkina Faso wanakiona kama miongo kadhaa ya utawala wa kisiasa, kijeshi, na kiuchumi wa Ufaransa — mara nyingi huelezewa na wafuasi wake kama minyororo inayoendelea ya ukoloni mamboleo.

Kote Ouagadougou na miji mingine mikubwa, michoro ya ukutani, mabango, na kauli mbiu zinazomsherehekea Traoré zinamwonyesha kama ishara ya heshima na uhuru wa Kiafrika. Hotuba zake, mara nyingi zikitaja kujitawala na urithi wa kiongozi wa mapinduzi Thomas Sankara, zinasikika zaidi ya mipaka ya Burkina Faso, na kumpatia sifa katika sehemu za Magharibi, Kati, na Kusini mwa Afrika.

Kwa wafuasi wengi, kuvunjwa kwa vyama vya siasa hakutafsiriwa kama shambulio dhidi ya demokrasia, bali kama mgawanyiko muhimu na tabaka la kisiasa linaloshutumiwa sana kwa ufisadi, utekaji nyara wa wasomi, na uzingatiaji wa maslahi ya kigeni. Uongozi wa kijeshi unasisitiza kwamba utaratibu wa kisiasa uliopita ulishindwa kutoa usalama, fursa za kiuchumi, au uhuru wa kweli
 
View attachment 3536586

We’ve seen this movie before,Traore yuko very wrong hapa, na nimeanza kuamini huyu jamaa ni propaganda tuu
 
mada nzuri here are your answers:
1) Dhahabu ziliwekwa kama akiba, na akiba kazi yake kutumika wakati wa majanga, but uzuri ni hio hio dhahabu inachimbwa ndan sio kwamba tunaenda kununua

2) Miradi lazima iendelee, kuna competition kali sana ya biashara kwenye region yetu tukizubaa basi inakula kwetu,
3) Alternative ingine ni kukopa, ukitaka kujua madhara yake nenda kenya apo
Bado adbul anakufr fir ee ujaacha uchoko wangechimba ndo wauze kwanin wauze zilizokusanywa ilihali hawajusanya ata kilo kumi!
Majanga unayoyasema wewe ni yapi adi nchi iuze dhahahabu kwani mlivyoua watu ovyo mlifikir mmewazaa nyie hamtohjiwa apo
Sasa ni hivii auze uo mikund wako na wa mama ako si ni akiba pia
 
Katika uchumi wa dunia akiba ya dhahabu ya nchi (National Gold Reserves) inatazamwa kama ngao ya mwisho ya uhuru wa kiuchumi. Taarifa kuwa nchi yangu Tanzania inapanga kuuza sehemu ya hazina yake ya dhahabu ili kufadhili miradi ya miundombinu imenistua sana.

Ni jambo linalopaswa kutafakariwa kwa kina na kila mzalendo , imekuwaje uzalishaji wa kila siku wa dhahabu nchini unashindwa kukidhi mahitaji ya ukwasi (Current Liquidity Needs), mpaka nchi ilazimike kugusa akiba ya kimkakati (Strategic Reserves) . Hatua hii si tu uamuzi wa kifedha, bali ni ishara tosha ya kupungua kwa uwezo wa serikali katika kusimamia uzani wa mapato na matumizi (Fiscal Deficit).

Dhahabu ni rasilimali inayoweza kugeuzwa kuwa fedha wakati wowote (Liquid Asset) na thamani yake haishuki kirahisi kama haya makaratasi mengine. Tunapouza akiba hii wakati sarafu yetu (Shilingi) ikiwa inapoteza nguvu dhidi ya dola ya Marekani, Kitaalamu, uamuzi huu unashusha uaminifu wa nchi mbele ya wakopeshaji wa kimataifa (Sovereign Creditworthiness) jambo ambalo linaweza kuifanya nchi ionekane inaelekea kufilisika (Insolvency)

Serikali inasema inauza dhahabu ili kujenga miundombinu. Hapa kuna fumbo kubwa la kiuchumi(opportunity cost). Miundombinu kama reli na barabara ni uwekezaji wa muda mrefu ambao unachukua miongo kadhaa kurudisha faida (Long term gestation period). Kwa upande mwingine, dhahabu inazidi kupanda thamani duniani kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi za Magharibi. Kuuza dhahabu inayopanda thamani ili kuwekeza kwenye long term investiments ni sawa na kutumia kiinua mgongo cha mafao kununua hiace ya biashara ambayo huna uhakika wa abiria hapa namaanisha hivi miundombinu mfano barabara na reli, ingawa ni muhimu, zinaanza kuchakaa (depreciate) siku ile tu zinapomalizika kujengwa. Zinahitaji mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo (maintenance costs). Pia, reli au barabara haianzi kuleta faida kesho inachukua miaka 20 hadi 30 kurudisha hata ile gharama ya ujenzi. Maana yake ni kwamba tunauza kitu ambacho kingetulinda dhidi ya mfumuko wa bei (dhahabu), ili tujenge kitu ambacho kitatugharimu pesa zaidi kukitunza (Reli/Barabara). Kwa lugha rahisi ni hivi Ikitokea dharura ya kitaifa kesho kama njaa(nimesema njaa maana mvua zimegoma) au vita, huwezi kuing'oa reli au barabara na kuiuza ili upate dola za kununua chakula au silaha. Lakini dhahabu unaiuza ndani ya dakika tano na kupata fedha. Tunapoteza uwezo wa kuwa na fedha mkononi (Liquidity) na kubaki na majengo/barabara ambazo haziwezi kutusaidia wakati wa dharura ya haraka.

Katika mazingira ya ukata wa fedha za kigeni (Forex Crunch), mara nyingi serikali hufanya maamuzi ya dharura chini ya shinikizo unajua serikali ya sasa kuna uwezakano wajanja washasoma gap la kupiga na kwakua Rais anaonekana kutokujali mambo basi anapenyezewa mkakati naye anaubaliki kama ulivyo.Swali la msingi ni je, uuzaji huu utafanyika kwa uwazi (Open Market Tender) au ni mikataba ya chini ya meza inayohusisha madalali (Middlemen)? Historia ya nchii hii inaonyesha kuwa rasilimali za taifa zinapouzwa kwa dharura kama wale twiga waliopanda ndege, nchi hupata hasara kubwa kupitia bei za michongo (Underpricing) huku kundi dogo la watu likinufaika na kamisheni nono si mnajua tena wanaomuongoza mheshimiwa ni watu wa aina gani?

Pindi hazina ya dhahabu inapopungua, imani ya soko kwa sarafu ya ndani huporomoka. Hii itapelekea kushuka zaidi kwa thamani ya Shilingi (Currency Devaluation). Kwa nchi inayotegemea kuingiza bidhaa nyingi kutoka nje kama yetu hii, bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya petroli, mitambo na dawa itapanda maradufu. Huu ni mnyororo unaosababisha mfumuko wa bei (Hyperinflation) ambao utamuumiza zaidi mwananchi wa hali ya chini tutarajie hili mda si mrefu

Uuzaji wa hazina ya dhahabu unapaswa kuwa hatua ya mwisho kabisa baada ya vyanzo vingine vyote kufeli. Badala ya kugusa akiba ya vizazi vijavyo. Serikali inapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (Austerity Measures) kama maposho ya kufuru safari za nje zisizo na maana magari ya anasa nk. Najua hapa hawapataki pia mtindo wa maisha wa ufahari usio na tija; kama Rais kuigiza sinema ni matumizi ya hovyo maana hakuna return yoyote kwenye utalii matokeo yake tunagusa hazina, kudhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia fedha za kigeni.

Kama wachumi na wazalendo wa Taifa hili, hatuwezi kukaa kimya wakati kibubu cha Taifa kikivunjwa ili kuziba mapengo yaliyosababishwa na usimamizi mbovu wa uchumi.Tunauza dhahabu maana yake vyanzo vingine vya Forex (Utalii, Mauzo ya mazao, Mikopo ya nje) vimeshindwa kukidhi mahitaji yetu kama kulipa madeni ya nje na kuagiza bidhaa na yote ni sababu ya uongozi mbovu na ulafi wa watu.KAMWENE
UNOGAGE!
 
Yanamtokeaje puani kama kuna uwezekano wa kuiuza nchi ili yeye awe salama?. Nadhani Sisi wananchi na vizazi vyetu ndio tutatokewa puani
THE SALE OF OUR GOLD RESERVE REQUIRES A NATIONAL CONSENSUS! A FEW CCM STALWARTS CANNOT DECIDE FOR THE WHOLE NATION,
 
Umechambua vizuri sana mzee mwenzangu. Kitu kingine ni kwamba Tanzania sio nchi ya kwanza kuuza gold reserve yake, cha kujiuliza hapa

Hiyo hela itatumika kwa ufanisi kulingana na malengo yake, au zitaishia mifukoni mwa watu kama kawaida yetu?

Kitu kingine, misaada inayo-boost bajeti yetu bila shaka imesitishwa kwa sababu ya lile doa la MO29, sasa kwanini tusiwatoe kafala wahusika ili nchi ipone?
 
Niliwahi kuwashauri wanaharakati sababu serikali haitambuliki, wafungue kesi kuzuia serikali batili kutumia hazina ya serikali ya Tanzania kama raid wa Venezuela Maduro alivyozuiliwa kutumia hazina yao ya dhahabu ila wao wameendelea kutumia mikakati ileile iliyozuiliwa.
Kwanini hiyo kesi usifungue wewe?
 
THE SALE OF OUR GOLD RESERVE REQUIRES A NATIONAL CONSENSUS! A FEW CCM STALWARTS CANNOT DECIDE FOR THE WHOLE NATION,
THEY CAN NOT???. UNAMAANISHA KWAMBA HAWAWEZI KUKIUKA UTARATIBU ILI KUPITISHA JAMBO LAO?
 
Sababu ya kuuza ni moja tuu, hatuna dollar za kuagiza petrol na vyakula, petrol tunaagiza 100% , ngano tunaagiza karibu tani milioni moja kila mwaka, vikikosekana hivyo vitu nchi haitakalika, kwa sasa beberu na utalii vimekata hakuna dollar na treasury imekauka, only solution ni kuuza dhahabu tuu, kwa wiki mbili tuu shilingi imeanguka kutoka 2400 installers 2600, na madeni lazima yalipwe mengi in dollars na huwezi default la sivyo tutageuka Zimbabwe soon, na kuuza dhahabu ni temporary solution tuu akiba ni ndogo, only permanent solution ni kukaa chini na wapinzani na beberu ili dollar na utalii virudi, trillion 3 za TRA ni mashilingi tuu huwezi fanyia kitu na hakuna nchi inaweza kukuuzia chochote
Andiko moja mujarab sana machawa wa Samia wanajaribu kulichokonoa lakini wameshindwa kukidhi viwango...

Wazo la KURUDISHA kununua dhahabu as reserve sio la SAMIA. Ni Magufuli ndiye aliyelizungumza. Na aligusia akiwa na hasira sana baada ya kugundua utapeli mkubwa na visingizio kadhaa visivyokuwa na mashiko yoyote.
Mbona sasa aliishia tu kuongea Januari 2019 na hakufanya kitu hadi anakufa Machi 2021?

Kama ni hivyo basi sifa zimuendee Ali Hassan Mwinyi ambaye alinunua dhahabu kupitia BOT kuanzia 1987 hadi 1991 walipositisha.
 
we ni mjinga, dhahabu inanunuliwa kwa tsh ikiwa ndan ya nchi lakini hio dhahabu ina nguvu nje ya nchi, we ni lijinga na huelewi kwann ziliekwa apo
Ungekuwa na akili wala usingetapika kinyesi hapa, hizi Tshs ni mawe au karatasi za magazeti?
Screenshot_20250729-090555~2.png
 
mada nzuri here are your answers:
1) Dhahabu ziliwekwa kama akiba, na akiba kazi yake kutumika wakati wa majanga, but uzuri ni hio hio dhahabu inachimbwa ndan sio kwamba tunaenda kununua

2) Miradi lazima iendelee, kuna competition kali sana ya biashara kwenye region yetu tukizubaa basi inakula kwetu,
3) Alternative ingine ni kukopa, ukitaka kujua madhara yake nenda kenya apo
Maswali yangu kwako
1) Tanzania kuna janga ambalo limepelekea serikali kuuza akiba ya dhahabu

2) Una proof gani ya kuwa hiyo miradi ya maendeleo itavuta investment opportunities ndani ya Taifa letu?
 
Back
Top Bottom