#COVID19 UVCCM: CCM imchukulie hatua Askofu Gwajima kwa kuhamasisha Watanzania kukataa chanjo ya Uviko-19
Aliongelea jimboni au kanisani?

Tusichanganye dini na siasa!
Hii ndio Impact ya kuchanganya ☝
Kuna kiongozi mwingine ye kutwa kuchwa yuko ✌,wengine hawana cha kusema wao kwao ni 👋.
Siku zijazo kila mtu afanye kazi yake kulingana na Taaluma aliyosomea.
 
Msihangaike na Gwajima,hangaikeni na mameno ya Mwendazake aliyetuasa chanjo Zina madhara.Gwajima anaendeleza tu alipoishia Mwendazake.
Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema

Source: Mwananchi
 
Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema
Eti asubiri party cocus?
We kijana kumbe wewe unatanguliza maslahi ya chama badala nchi?
Huna uchungu na Watanzania wewe Labda unauchungu na kule ulikotoka.
Mwache Gwajima atusemee Watanzania.
 
NUKUU ZA KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) NDUGU. KENANI LABAN KIHONGOSI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO 27/07/2021

"Tunapenda kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama chetu Kwa namna ambavyo ameendelea Kufanya Kazi bila kuchoka na kuendelea kulinda Amani ya Nchi yetu, na sisi Vijana tupo pamoja naye kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya 6 inaenda kutimia"

"Lakini jambo lingine sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na Rais Wetu na Serikali yetu, Watanzania msirubunike, nendeni Kwa hiari yenu mkapate Chanjo. Rais ndiye raia namba moja na hawezi kuliongoza Taifa Kwenye mambo yasiyofaa"

"Sambamba na Hilo sisi Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na viongozi Wetu wa Serikali kwani Maendeleo tunayoyapigania ni Kwa manufaa ya Watanzania wote kwa hiyo wale wote wanaopinga Maendeleo yanayofanywa waache mara Moja"

"Sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kauli zile tunazilaani na tunazipinga vikali Maana kama utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge ana hoja Kuna party cocus ambazo zipo peleka hoja zako kwenye vikao, na anaposema anayesisitiza kuhusu Chanjo atakufa ajue yeye sio Mungu"

"Tunaomba Chama kiwachukulie hatua Kali na waache mara Moja kuropoka"

"Niwaombe Watanzania twendeni tukapate Chanjo Kwa hiari yetu Huku tukiendelea Kufanya mazoezi ili Taifa letu lipate kuwa na watu wenye Nguvu Kwa Maendeleo ya Taifa letu"

"Tunapomuongelea Rais tunamuongelea Raia namba moja kwenye nchi hii ambaye Mungu ametupa, kama huwezi kumheshimu kama Mzazi basi mheshimu Kwa mamlaka yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Kuna jambo pia naomba niliseme, Juzi Kuna viongozi wameongea kuhusu Chanjo, Mbunge wa Kawe Gwajima ameongea maneno yasiyofaa kuhusu Chanjo ya Corona na Chanjo imeshaletwa, Sasa anapotokea Kiongozi wa mhimili mwingine anaenda kuwahubiria Waumini na kuwatisha watu kuwa wanaosapoti watakufa sasa Tumweleze kuwa anayetoa Uhai ni Mungu na anayechukua Uhai ni Mungu"

"Tunapenda kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama chetu Kwa namna ambavyo ameendelea Kufanya Kazi bila kuchoka na kuendelea kulinda Amani ya Nchi yetu, na sisi Vijana tupo pamoja naye kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya 6 inaenda kutimia"

IMG-20210727-WA0030.jpg

IMG-20210727-WA0031.jpg

IMG-20210727-WA0032.jpg

IMG-20210727-WA0033.jpg

IMG-20210727-WA0034.jpg

IMG-20210727-WA0035.jpg

IMG-20210727-WA0036.jpg

IMG-20210727-WA0037.jpg
 
KKanyoka walichokafuga CCM kamegeuka na kuwa joka- Dragon.
Sasa hivi gwajima ana kofia mbili, kupambana naye itawacost
 
Mkitaka kumkomoa Gwajima mfuteni uaskofu,ubunge uwaziri na urais kwake si lolote wala si chochote.
Lakini mbona Magufuli alikataa chanjo na mkawa mnashangilia mkikenua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapenda kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama chetu Kwa namna ambavyo ameendelea Kufanya Kazi bila kuchokana kuendelea kulinda Amani ya Nchi yetu, na sisi Vijana tupo pamoja naye kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya 6 inaenda kutumia"

"Kuna jambo pia naomba niliseme Juzi Kuna viongozi wameongea kuhusu Chanjo, Mbunge wa Kawe Gwajima ameongea maneno yasiyofaa kuhusu Chanjo ya Corona na Chanjo imeshaletwa, Sasa anapotokea Kiongozi wa mhimili mwingine anaenda kuwahubiria Waumini na kuwatisha watu kuwa wanaosapoti watakufa sasa Tumweleze kuwa anaetoa Uhai ni Mungu na anaechukua Uhai ni Mungu

"Lakini jambo lingine sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na Rais Wetu na Serikali yetu Watanzania msirubunike nendeni Kwa hiari yenu mkapate Chanjo Rais ndiye raia namba moja na hawezi kuliongoza Taifa Kwenye mambo yasiyofaa"

"Sisi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kauli zile tunazilaani na tunazipinga vikali Maana kana utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge ana hoja Kuna party caucus peleka hoja zako Huko na pia
Tunaomba Chama kiwachukulie hatua Kali na waache mara Moja kuropoka"

"Sambamba na Hilo sisi Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunasimama na viongozi Wetu wa Serikali kwani Maendeleo tunayoyapigania ni Kwa manufaa ya Watanzania wote kwa hio wale wote wanaopinga Maendeleo yanayofanywa waache mara Moja"

" Niwaombe Watanzania tukapate Chanjo Kwa hiari yetu Huku tukiendelea Kufanya mazoezi ili Taifa letu lipate kuwa na watu wenye Nguvu Kwa Maendeleo ya Taifa letu"
 
Wewe Kihongosi si ndiye ulikuwa unapendekeza Zitto Kabwe auwawe, haya sasa Gwajima kawatieni kidole kabisa mpigeni risasi, mbona kwa Tundu Lissu mliweza? Wacheni kutupigia kelele, muueni Gwajima muone moto wake, ana watu huyo
 
Back
Top Bottom