UVCCM wamekengeuka, kumkomalia Spika kujiuzulu ni dalili kuwa hampendi bunge kufanya kazi zake za kuisimamia Serikali. Mnatumika bila kufikiri

Wanapigana vikumbo walau kwenye mkeka wa wakuu wa Wilaya/mkoa wakumbukwe.
 
Hawa madogo hawana akili ,wao ni bendera fata upepo.
 
Madhambi yake ndiyo yametufanya tusimtetee ni shetani pekee anaweza kumtetea Ndugai
Mbona chadema ilizunguka nchi nzima kwa miaka 8 kusema Lowasa no fisadi ila mbowe alipomfanya gwajima kuwa mshenga wa kumleta LOwasa chamani ukaunga mkono bila maswali?
Tena si huyo tu kuna Nyarandu, sumaye na wengine wengi tu?
 
Mbona chadema ilizunguka nchi nzima kwa miaka 8 kusema Lowasa no fisadi ila mbowe alipomfanya gwajima kuwa mshenga wa kumleta LOwasa chamani ukaunga mkono bila maswali?
Tena si huyo tu kuna Nyarandu, sumaye na wengine wengi tu?
Lowasa yupo wapi sahivi?
 
Mkuu Ndugai alijijengea uadui kila kona bila yeye kujua. Sasa ndiyo anaelewa kumbe bora ya wapinzani huongea hadharani muda wowote ila ccm ni kama kikulacho ki nguoni mwako.
Aliendesha bunge kama mali yake binafsi na ubabe wa kijinga sn alaaniwe yeye na kizazi chake chote
 
Uvccm mko sahihi nyokeni na dungayembe..

Amekuwa akitoa kauli za kuzingua na kuudhi Sana,mara aseme toka Mwendazake kafa eti umuhimu wa Dodoma haupo wakati anafahamu Mama katoa zaidi ya bil.600 za kuendelea na ujenzi wa Makao makuu awamu ya pili.

Kuendelea kuwa na mtu kama huyu haifai,kila Rais anaweka watu watakomsaidia kuanzia Spika hadi wateule wengine wote ndani ya serikali hadi kwenye chama.
 
Mi nadhani anayekaa kimya kwenye hili sakata ndo smarter than all.
 
Unataka wawe kinyume na mwenyekiti wa wa CCM Taifa, inakuingia akilini.
 
Na kwanini Samia awachukie wanaoutaka urais 2025?
Hata hayati Magufuli aliwachukia watu waliotaka urais .Membe alibaki ndani ya chama au aliondoka? . Hakuna Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm amewahi kuvumilia wanachama wenzake wanaotaka urais akiwa madarakani, hata Lowassa anajua.
 
Tatizo ni huyo mdhibiti mkuu wa bunge ndio kawachosha. Anaonyesha ubabe uliopitiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…