Uvumilivu wa IPTL Walipa Katika Mzozo wa Dola Milioni 168 na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong



Nilipost hii taarifa Moderator wakafuta.

Samia anamiliki km za eneo 614 za migodi
 
Hakuna mjukuu wa mudy aliechukua fedha kwenye sandalusi?
Kuna familia ya msanii mmoja hivi wa msoga ilikuwa inapishana na viroba vya sandarusi vilivyojaa hela za ufisadi. Sijui ni bilioni ngapi zile, maana hata hazijulikani idadi yake.
Sasa Askofu Kilaini na yule Askofu mwenzake walipewa tumilioni 40 tu kila mmoja! Vipi kuhusu Chenge na Tibaijuka waliopewa bilioni 1+ hela ya mboga!
 
Hawawezi kuongelea haki ktk hili eneo maana linawagusa, ile mifuko ya sandalusi aliyokuwa akiisema bwana lisu na wao walijaza mafweza
TEC walipokea sadaka. Katika dunia nzima, hakuna sehemu yeyote ile ambapo sadaka inakuwa declared chanzo chake. Hiyo siyo kodi.

Same way na ambavyo wauza madawa ya kulevya hujenga misikiti na kuweka wakfu nyumba zao wakifa. Imamu haji kuuliza chanzo cha mapato ya ujenzi huo.

Fisadi, malaya, mwizi, aliyeuza vitumbua, aliyeshona viatu, aliyeokota hela, aliyedanga, aliyerithi, aliyelipwa mshahara wote hawa wanaweza toa sadaka, zaka, fungu la kumi na majina yote ya michango ya taasisi za kidini.

Au kama vipi ifungulie kesi TEC ya kupokea fedha, uone utaambulia nini kwenye hiyo hukumu.
Mimi huwa nalipa zaka kidigitali, hakuna sehemu ya kuuliza nimetoa wapi hela.
 
TEC nao walikula hela humo
source: KKKT
Sina maslahi na TEC..,ila kusema benki ya TEC walichukua mgao katika kashfa ya ESCROW/ IPTL , ni jaribio la kutaka kuwaficha kwa makusudi wahusika wakuu wa upigaji wenyewe.
Zitto Kabwe ndiye alikuwa wa kwanza kusema bungeni wakati huo kwamba benki ya Mkombozi,inayomilikiwa na kanisa Katoliki ichunguzwe kwa vile fedha za malipo kwa bwana Rugemalira kwa kuuza hisa zake kwa kampuni ya PAP ya bwana Seth Singh,yalifanywa katika akaunti yake ya Mkombozi bank.

Zitto Kabwe kwa sababu anazozijua yeye alisema siku hizo kwamba Mkombozi bank ichunguzwe kwa kashfa hiyo.
Lakini hoja iliyokuwepo ilikuwa ni kama Mkombozi bank walivunja taratibu,sheria na kanuni za kibenki zilizowekwa na aliyewapa leseni ya biashara ..,BOT.
Sasa sijui Mkombozi bank walivunjaje taratibu endapo fedha ziliingizwa katika akaunti ya mteja wao, na mtumaji wa hiyo fedha alikuwa BOT yenyewe kwa niaba ya kampuni ya PAP.
Na Mkombozi bank ilimfanya Rugemalira awagawie aliowapenda kwa kufuata sheria za kibenki...yaani kuhamisha fedha toka katika akaunti yake kwenda kwa walengwa wake.....na ndiyo maana inajulikana nani alipewa fedha na Rugemalira baada ya kuuza hisa zake.

Kuchukua fedha kaika mifuko ya SANDARUSI hakukufanywa katika benki ya Mkombozi bank.
Kwanza ijulikane kuchukua fedha katika viroba bila kutaka kujukikana utambulisho wako ni kinyume na sheria za kibenki.
Banki ya Stanbic ndiyo ilihusika kufanya hayo...na kwa mujibu wa sheria walitakiwa kuchukuliwa hatua. Lakini Stanbic hawakuwajibishwa kwa vile mmoja wa wachukua fedha za escrow katika sandarusi alikuwa bwana Marwa,mkwe wa Jakaya Kikwete.

Kwa hiyo kashfa ya kibenki kwa mantiki ya kuhamisha fedha kinyume na taratibu ilifanywa na Stanbic na siyo Mkombozi.
 
Wahuni wamemaliza mchezo kwa kutumia sababu za kiufundi za kisheria
 
Usimseme kwa mabaya bhana.

Huyo alifadhili kampeni za uchaguzi za chama chetu.
 
I hope hapa Serikali haihusiki?? Bali ni Standard Charterd ndiyo kimemlamba
 
Mvumilivu hula mbivu, IPTL hatimaye yajisafisha. Na kuondoka na pesa ndefu safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…