Uchaguzi 2020 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. John Pombe Magufuli

Uchaguzi 2020 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. John Pombe Magufuli

Wabongo wanashangaza kweli,unakuta kaenda pale Asubuhi Hana hata Mia mchana anaanza kuunga unga nauli ya kurudi kwake
 
Hawawezi kwenda, hawajaongezwa mishahara kwa miaka mitano.
1602245040372.png
 
Wazee wa picha za drone mbona siwaoni leo asubuhi walikuwa na machachari kweli. Crimea ukowapi ndugu yangu utupie tupicha twa drones tuwafunge mdomo machadema..

Asubuhi kwenye uzi huu walikuwepo wote na aamsha amsha kama yote now siwaoni tena. Wangetest mbinu ya machadema ya kuchakata picha wananchi tupate burudani eti
 
Hivi leo lugha itakayotumika ni ipi...Kiswahili cha kijiji, Kiswahili cha taifa au Kiswahili cha dunia? Mimi ningemshauri atumie Kiswahili cha Dar es Salaam tu kama itawezekana na ajiepushe kuchomekea kile cha dunia.

mna lingine la kusema?
 
Kwahiyo watu wa mikoani kama huko Morogoro ndio mijinga sana kiasi kwamba hadi wanabebwa kuja kuangalia wasanii Dar?
Enyi wafuasi wa chama cha mbowe, Pengine siku moja mkiacha kuwaza na ?kunena upuuzi labda mnaweza mkajitahidi kuongeza viasilimia vya ushindani. Maana sasa hivi hamna ushindani bali mna upinzani. Mmechelewa sana yani
 
Enyi wafuasi wa chama cha mbowe, Pengine siku moja mkiacha kuwaza na ?kunena upuuzi labda mnaweza mkajitahidi kuongeza viasilimia vya ushindani. Maana sasa hivi hamna ushindani bali mna upinzani. Mmechelewa sana yani
Magufuli alidai aambiwe ati dhambi yake nini hata asipewe tena Miaka Mitano.

Dhambi za Magufuli ni Nyingi sana Uwongo, Tamaa, Uuaji, Ukatili kutokuwa na Uaminifu, Uonevu na Wizi.

Kutaja tu chache.
 
Baada ya kupumzika kwa siku kadhaa, mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea na kampeni leo katika mkoa wa Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.




Up dates;

HOTUBA YA DKT. MAGUFULI
....gonjwa hili la Corona na kilio cha Wanakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta katika kuliombea taifa na kumuomba Mungu kuondoa Ugonjwa huu, napo Kenya utaondoka. Kwasababu Mungu ukimuomba hakuna kitakachoshindikana, na Mungu ni mwema siku zote. Mungu hoyeeee! Tanzania hoyeee! Kenya hoyee!

UMUHIMU WA JIJI LA DAR KWA UCHUMI WA TAIFA
Ndugu zangu wana Dar es Salaam, jiji la Dar es Salaam ni muhmu sana hapa nchini. Ni kwasababu jiji hili lina idadi kubwa ya watu kuliko miji mingine yote nchini. Takwimu zinaonesha jiji hili linakadiriwa kuwa na watu milioni 6. Na itakapofika mwaka 2030 linatarajiwa kuwa na watu wapatao milioni 10.

Hii italifanya jiji hili kuwa miongoni mwa majiji manne yenye hadhi ya “Megacity” barani Afrika. Majiji mengine ni pamoja na Lagos, Luanda pamoja na Kinshasa.

Kwahiyo jiji la Dar es Salaam ni jiji muhimu sana. Mbali na kuongoza kwa idadi, Dar es salaam ni jiji kuu la biashara hapa nchini ambalo linachangia mapato mengi ya serikali, lakini pia linatoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa.

Takwimu zinaonesha kuwa kwa tarkribani miaka mitano iliyopita Dar es Salaam imekuwa ikiongoza kwa uchangiaji mapato ya serikali, hususani mapato ya kodi.

Takriban 90 % ya kodi yanatoka Dar es Salaam. Nataka nitoe takwimu.

Mwaka 2015/16, mapato ya Dar es Salaam yalikuwa Tshs. Trilioni 11.9 ambayo ni asilimia 89.9

Mwaka 2016/17 ilikuwa Trilioni 12.6, asilimia 88.6

Mwaka 2017/18 ilikuwa Tshs. Trilioni 13.6 ambapo ni asilimia 89

Mwaka 2018/19 ilikuwa Tshs. Trilioni 13. 9 ambayo ni asilimia 88.7

Mwaka 2019/20 ilikuwa Tshs. Trilioni 16.01 ambayo ni asilimia 89.7

Aidha, kwa miaka mitano Dar es salaam imeendelea kuongoza katika kuchangia pato la taifa. Mwaka 2015 ilichangia Tshs Trilion 16.2 ambapo pato la Taifa lilikuwa Tshs. 94.3

Mwaka 2016 Dar es Salaam ilichangia Tshs. Trilioni 18.4 wakati pato la taifa lilikuwa trilioni 108.4

Mwaka 2017 Dar es ilichangia Tshs. 20.5, pato la taifa lilikuwa Trilioni 118.7

Mwaka 2018 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 22.5, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 129.04

Mwaka 2019 Dar es Salaam Ilichangia Tshs. Trilioni 23.9, wakati pato la taifa lilikuwa Trilioni 139. 9

Hii inahihirisha umuhimu wa jiji hili kwa maendeleo ya nchi yetu. Hongereni sana wana Dar es Salaam.

Ndugu zangu wana Dar es Salaam, kama hilo halitoshi, jiji hili ni lango kuu lashughuli za uchukuzi na usafirishaji. Siyo tu kwa hapa nchini, lakini pia kwa nchi nyingi zinanotuzunguka.

Kama mnavyofahamu, nchi yetu inapakana na nchi 8 na nchi 6 hazina bandari, na hivyo kutegemea Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao.

UTEKELEZAJI WA AHADI ZA MWAKA 2015
Ndugu zangu Wana Dar es Salaam, ni kwa kuzingatia hayo yote nilipokuja hapa Dar es Salaam kuomba kura mwaka 2015. Niliahidi mambo mengi lakini leo nitataja mambo maubwa manne ambayo niliahidi mwaka 2015.

La kwanza, niliahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Pili, niliahidi kuimarisha miundombinu ili kurahisisha usafiri wa hapa Dar es Salaam lakini pia usafiri wa kwenda mikoani pamoja na nje ya nchi.

Tatu, niliahidi kuboresha huduma za jamii ikiwemo Afya, Elimu, Maji pamoja na Umeme.

Na nne, tuliahidi pia kuboresha mazingira ya biashara kwa ajili ya Wana Dar es Salaam na kwa ajili ya Watanzania wote.

Nafarijika kuona kwamba kwenye hii miaka mitano muliyotupa tdhamana ya kuliongoza taifa, tumeweza kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo.

i. ULINZI NA USALAMA
Wakati tunaingia madarakani, hapa Dar es Salaam, vitendo vya ujambazi hususan vya kutumia silaha vilikuwa vimeanza kushamiri. Ilikuwa mtu ukienda benki kuchukuwa hela, unakuwa na hofu kama fedha zako utazifikisha salama maana uhakika ulikuwa mdogo kwasababu ya ujambazi. Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kudhibiti vitendo hivyo. Sio tu hapa, bali maeneo ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti.

Kwa kuimarika hali ya usalama, wananchi wanaendelea na shughuli zao za Maisha bila hofu.

Nawapongeza Wana Dar es Salaam lakini pia navipongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama.

ii. MIUNDOMBINU
Mambo mengine ni kuhusu miundombinu…tumefanya mambo mengi sana.

Kwanza, tumejenga barabara za lami kwenye mitaa ya Dar es Salaam. Ukijumlisha hizo barabara zote za lami zilizojengwa na zinazojengwa, ni zaidi ya kilometa 200 ambapo tumetumia zaidi ya bilioni 660.

Ninyi Wana Dar es Salaam ni mashahidi kwamba hivi sasa mitaa mingi ya jiji hili la Dar es Salaam ina lami na nyingine zimewekewa mpaka na taa, ikiwa barabara ya njia nne kutoka Morocco hadi Mwenge inayojengwa kwa gharama ya Tshs. Bilion 74.8; barabara ya Bamaga-Shekilango, na barabara nyingine. Lakini, barabara ya njia nane ya kutoka Kimara-Kibaha inayojengwa kwa Tshs Bilioni 140, nayo inaendelea kwa kutumia fedha zetu.

Kuhusu hii barabara ya Kimara-Kibaha yupo mgombea mmoja wa Urais amesikika akisema eti tunajenga barabara pana sana. Tena anasema yeye ametembea nchi nyingi na hajawahi kuona barabara pana kama hii. Majibu yake ni kwamba si kweli kwamba hii ndiyo barabara pana kuliko zote duniani, kule “Hoston” (Houston), Marekani ipo barabara inaitwa Katty Freeway, ina njia 26.

Lakini, hata kama kwa mfano, ingekuwa barabara yetu ni pana kuliko zote duniani, mimi sioni ubaya wowote. Hakuna ubaya wa Tanzanania kuwa na kitu kikubwa kuliko chochote duniani. Siyo lazima kila kitu kizuri, kikubwa kiwe kipo Ulaya.

Mbona Mwenyezi Mungu aliamua kumuweka mtu wa Kwanza hapa Tanzania? Anashangaa kitu gani?

Mbona Mungu alitupa Mlima mrefu na mti mrefu kuliko yote barani Afrika?

Mbona Mungu aliamua kutupa Tanzanite wakati haipo mahali pengine?

Zaidi ya hapo ndugu zangu, tumekamilisha barabara ya mabasi ya mwendokasi, awamu ya kwanza. Kutoka Kivukoni hadi Kimara na kutoka Magomeni hadi Morocco, kwa gharana ya Tshs. Bilioni 403, na sasa tunaanza ujenzi wa awamu ya pili kutoka Gerezani hadi Mbagala. Nyie wenyewe ni mashahidi munaona barabara inawekewa mpaka nondo.

Lakini vilevile tumejenga daraja la juu pale Mfugale, TAZARA kwa Tshs. Bilioni 101 na daraja la Ubungo kwa Tshs. Bilioni 229.8.

Na tumekamilisha Daraja la Nyerere pale Kigamboni ambalo lilianza kujengwa kwenye awamu iliyopita. Na sasa tunaendelea na daraja la kilometa moja pamoja na barabara yake ya kilomita 7 pale Selander Bridge.

Kwa Tshs. Bilioni 270 na madaraja mengine ya juu pale Gerezani kwa Tshs Bilioni 24.8.

Kuna baadhi ya wilaya, jhasa hizi wilaya mpya za Ubungo na kigamboni tunataka kufumua barabara huko, ndiyo maana tumekuja kuwaomba kura hapa.

Kuhusu miundombinu ya usafiri, jana mumeshuhudia tumeweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa stendi ya kisasa wa stendi ya kimataifa pale Mbezi Louis, yenye uwezo wa kupokea mabasi 3446 kwa siku na ina eneo la kulaza mabasi 1000.

Zaidi ya hapo, kwenye miaka mitano iliyopita tumekamilisha ujenzi wa jengo la tatu la abiria JKNIA kwa gharama ya Tshs. Bilioni 722.5. Jengo hilojipya lina uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni 6, wakati majengo mawili ya mwanzo yalihudumia wageni milioni 2 tu. Kwahiyo kwa sasa uwanja una uwezo wa kuhudumia wageni milioni 8 kwa mwaka.

Lakini ninyi ni mashahidi tumenunua ndege 11. Na katika miaka mingine mitano kama mutatupa ridhaa, tumepanga kununua ndege nyingine 5 mpya, ikiwemo ndege kubwa ya kubeba mizigo.

Zaidi yah apo, kwenye miaka mitano iliyopita tumetumia Tshs. Bilioni 9020 kufanya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam

Hakuna jipya CCM.
 
Back
Top Bottom