Uwanja wa Mkapa | Kombe la ASFC, Simba SC 2 - 1 Kagera Sugar

Uwanja wa Mkapa | Kombe la ASFC, Simba SC 2 - 1 Kagera Sugar

Hilo goli la kusawazisha ni clear offside, tuna safar ndefu sana
Basi tufanye hilo la pili ndilo la kusawazisha. Hapo bado una la kusema. Bado tupo na ninyi bega kwa bega hesabuni Utopolo bado tuna game mbili na nyie. Labda muombe mfungwe njiani lakini TFF ni waungwana watapanga SIMBA na Yanga robo fainali ili msikimbie
 
nadhani makadirio ya kocha ilikua kupata mabao ya mapema halafu kipindi cha pili kiingie kikosi kwa ajili ya ku defense ushindi
watawapa wachezaji fatigue sasaa. na inaonekana kocha ameshajua aina ya mashabiki wa kitanzania ndio maana anaogopoa kupoteza mechi.hii gemu sio ya kuanza na kikosi cha kwanza, hata ukipoteza haina madhara yoyote ,ukilinganisha na kupoteza gemu zilizo mbeleni. malengo yetu ni nusu fainali ya champions league na kuchukua ligi. haya mengine ziada tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Patashika ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) linapigwa leo Mei 1, 2021 saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, ambapo Mabingwa Watetezi, Simba SC wanakwaruzana na Kagera Sugar katika mchezo wa hatua ya 16 ya michuano hiyo.


========

Naaaam mpira umeanza uwanja wa Mkapa.

15' Mchezo ni mkali Wanaume hawa wanapambana lakini Simba SC wanamiliki mpira huku wakikosa nafasi nyingi zaidi kuliko Kagera Sugar

25' Kagera Sugar hawajaleta hatari zaidi kwa Simba, kama ambavyo Simba SC wanajaribu kutafuta bao

Simba SC 0-0 Kagera Sugar

40' Free Kick kuelekea Kagera Sugar, anapiga Wawaaaaa, golikipa anatema shuti lile.

42' Kagera Sugar wanakosa utulivu wa kuweka wavuni mpira, Mayanga alifanya kazi nzuri ya kumpiga chenga Wawa.

Golikipa wa Kagera Chalamanda anaonyeshwa Kadi ya Njano kutokana na kupoteza muda.

45' Goooooooooooooooooooooal

Erick Mwijage anaipatia Kagera Sugar bao la kwanza akiunganisha krosi ya kichwa

Simba SC 0-1 Kagera Sugar

Vitals Mayanga anaonyeshwa Kadi ya Njano baada kuzuia mpira usipigwe.

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Kagera Sugar wapo mbele kwa bao moja.

HT, ASFC; Simba SC 0-1 Kagera Sugar

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, na Ametoka Taddeo na ameingia Morrison upande wa Simba SC.

Free Kick kuelekea Kagera Sugar, anapiga Chamaaa loooooo golikipa anatema na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

54' Ametoka Bwalya na ameingia Bocco upande wa Simba SC

55' Morrisoon Gooooooooooooaaal Gooooooaaal

Bernard Morrison anaipatia Simba bao la kusawazisha kazi nzuri ya Miquissone.

Simba SC 1-1 Kagera Sugar

Miquissone anaachia shutiiiiii kali, lakini mpira unatoka nje na kuwa Goal Kick.

67' Kagere Goooooooooooooaaal Gooooooaaal

Maddie Kagere anaipatia Simba SC bao la pili, akipokea pasi safi kutoka kwa Morrison

Simba SC 2-1 Kagera Sugar

Ametoka Mwijage na ameingia Seseme upande wa Kagera Sugar. Na ametoka Maddie Kagere na ameingia Nyoni upande wa Simba SC
Uzi umeupozesha sana. Updates zinatakiwa mara kwa mara siyo kusubiri goli tu. Wengine tuko barabarani tunategemea kutoka kwako, tafadhali.
 
Yaani Simba tunashinda kihalali bila makando kando yoyote yaani mtu anafungwa kisha anaridhika kabisa kuwa kweli nimepigwa na timu bora.

Sio umnashida huku makando kando kibao watu wanalalamika mara refa kipofu mara sijui ml 40 yaani figisu tupu.

Hii ndio maana halisi ya timu kubwa yaani Mnyamaa.
 
Back
Top Bottom