Uwapi "wembe wa Mdude uliotumika kumnyoa Mwendazake" ambao Samia Alitishiwa nao majuzi?

Huo wembe inasemekana umekuwa butu baada ya wanaoumiliki kuanza kunyolea ndevu zao na pubic hair.😁
 
Ndio maana katiba mpya ni ya muhimu sana aliyotufanyia shujaa wa afrika yametosha na katushtua ya kuwa kwa katiba hii tutawaachia wanetu majanga
 
Kuna chama au taasisi isiyo na wahuni?
Mkuu nimekuuliza na wewe unaniuliza. Si ungenijibu kwanza halafu ndio ukaniuliza na wewe swali lako??

Narudi kukuuliza, kwahiyo Mdude Nyagali ni muhuni tu??
 
Evarist Chahali umeniudhi sana twitter lakini ulichoandika ndio ukweli... Hapa kuna watu itawauma lakini hawana namna ya kufanya. Kama kweli inawauma sana watanzania basi wachukue action lakini hakuna mwenye uwezo.

Ingekuwa SA hata muda wa kutoa kitisho online usingekuepo zaidi ya kuona watu barabarani tu. Upinzani Tanzania una hali ngumu sana.
 
Umeandika ukweli mtupu!

Mawazo yako ni kama ya kwangu ila ya kwako yameenda kina zaidi.

Ila ukweli huu Chadema hawataki kuusikia! Ndiyo maana tofauti ya Makada wa CHADEMA na MATAGA binafsi siioni. Ni bomba mbili tu zilizofungwa sehemu mbili tofauti ila zote zinapeleka maji kwenye tank moja.
 
Mkuu nimekuuliza na wewe unaniuliza. Si ungenijibu kwanza halafu ndio ukaniuliza na wewe swali lako??

Narudi kukuuliza, kwahiyo Mdude Nyagali ni muhuni tu??

Kama una uelewa mzuri hilo ni jibu lililo katika mtindo wa swali. Huyo Mdude ni muhuni kama alivyo Sabaya na Makonda.
 
Acha upotoshaji, umesahau moshi wa Lindi? time will tell
 
WANACHADEMA WATAKUWA WAMEMUAMBIA ANAENDA RESS SANA ANAWAHARIBIA CHAMA NAONA KATULIA ATULIZE DISH MAANA LIMEYUMBA SANA
 
Samia ni dikteta kwa sababu hafuati sheria, kutumia kigezo cha kuwafutia kina Mbowe kesi ndio u-justify Samia sio dikteta ni ufinyu wa kufikiri, hii nchi inaendeshwa kwa sheria sio hisani.
Hebu subiri...kina Mbowe hawakufutiwa kesi bali walishinda rufaa dhidi ya kesi ile...mama hakumtoa Mdude gerezani bali alishinda kesi!
 
Yaani hii ni typical mindset ya mijitu mioga kwenye hii nchi, hata kama hili tayari lilishakimbia.
Angalau baadhi ya watu wa CHADEMA wanaojesha ujasiri wa wazi wa kupambania maslahi ya watanzania na sio kwenye mitandao bali barabarani na huko kwenye makongamano yao. Watu wenye akili tunapaswa kuwaunga mkono kwa hali na mali. Wamekuwa wakionyesha leadership kwenye kipindi kigumu sana.

Sijui kwanini watu wana hii mindset. Mikondoo halafu perepeche nyingi yaani, maneno mingi kama hili lileta uzi. Halafu inalalamika, mara tozo, sijui ajira, maisha magumu! Halafu wachache ambao wamejitoa kupambana tunawavunja moyo na maneno uchwara kama haya.

Halafu hili si ndio lilimpigia kampeni yule dhalimu aliyetutesa! Eti lilisema ni consultancy na Kinana atalilipa!

Mindset ambazo ni defeatist zinaturudisha nyuma.
 
Takataka kabisa kama wewe ni kachero kwanini umekimbia nchi?

Pumbavu
Hili ni zaidi ya pumbavu. Yaani linakera sana.
Mjadala wa katiba na mapambano halisi ya baadhi ya watu unayashusha kwa mada petty kama hii.
Sipendi personal attacks lakini hilo jamaa ni pimbi sana halafu inaonekana ni lioga pia. Very defeatist.
 
Duniani hakuna mtu ambae haigi hata MAENDELEO tuliyonayo tumeiga kwa Wazungu hivo kuiga kitu sio kosa.

Kuna mahali nimsema kuwa kuiga ni kosa ?

Ukiiga ubunifu wako nao unatakiwa sio unaiga kitu ambacho kwenye mazingira yako kinakuwa hakina tija sana .

Katiba sio ajenda kubwa kwa wananchi wao wanapoteza muda na kuushusha ushawishi wao .

Utake iko hivyo usitake itakuwa hivyo.
 
Ni wakati sasa Mwenyekiti wa Chademaa ang'atuke apishe wengine aina ya siasa zake hazileti tija kwa sasa.
 
wanapima kina cha maji kwa nn kipind cha magu hawakujaribu
 
Kipindi cha Magu mimi mwenyewe niliwaunga mkono sana! Ila kwa hili wameteleza. Ajabu iliyokubwa nilidhani kejeli, dharau na matusi ya jumla na rejareja huwa wanayatoa Mataga tu kumbe makamanda/makada wao nao vilevile.

Ijapokuwa ajenda yao ni nzuri ila katika hili Chadema hawatoungwa mkono na raia na huwezi ukasikia mtaani au kijiwe wanazungumza masuala ya Mbowe, sijui Chadema wala katiba. Watu hawana habari wanashughulika na maisha yao. Zaidi makada ambao ni kundi lilelile lililopo Jf na Twitter.

Kuna mambo ambayo wangeyagusa wangeanza nayo kama ajenda zao wangeungwa na wengi kwa sababu nguvu ya wanasiasa ni umma. Mtanzania hana habari kabisa na katiba! Yeye anachokitaka maisha yake yawe nafuu na ugumu ambao ulisababishwa na awamu iliyopita. Ingelikuwa ni vyema wangejikita na haya na kuangalia mapungufu na athari hasi ya sehemu za bajeti zilizopitishwa wangeungwa mkono na raia.

Kuna mambo yangewakwamisha tu mbeleni. Hapa ndiyo ingelifaa kuwaambia raia tunahitaji katiba mpya ili mambo yawe sawa! Kwa wanachokifanya sasa hivi kwa mambo ambayo Mama Samia aliyowafanyia kwa waliyofanyiwa awamu iliyopita, ukilinganisha na kauli wanazozitoa viongozi wake na wanayoyafanya imma yawe sahihi au yasiwe sahihiwataonekana wanaleta fujo tu! Na ndivyo wengi wa raia watakavyowatafsiri.
 
Ukiwa barabarani hata kama ni haki yako ukiona kuna dhara linataka kutokea jihami.

Sawa upo kwenye haki lakini utadhurika. Siasa ni sayansi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…