A HUMBLE LEADER
Senior Member
- Sep 21, 2022
- 138
- 343
MkuuMnamo mwaka 2013 baba yangu alikutana na mchungaji mmoja huko Moshi na baba yangu akamueleza kiu yake ya kuwa karibu na Mungu kwani ujana wake hakuwa mtu wa kwenda kanisani. Mchungaji(jina limenitoka lakini ningemtaja) akamueleza habari za uwata na kwamba angemkutanisha na kiongozi wa dhehebu hilo, basi wakaanza kwenda wote faraghani na hata ilipofika wakati wa kurudi Dar(nyumbani) baba hakufika kabisa nyumbani na baada ya muda tukasikia amepatiwa mke kanisani na hivyo anafunga nae ndoa ( hakuwa anashaurika tena na tuliona walakini kwenye mental health yake, hakuwa tena kama zamani).
Ndugu zake pamoja na mama walijitahidi kuweka mapingamizi kwenye makanisa ya Dar hivyo hawakuweza kufunga ndoa hapa dar ikawalazimu ndoa ifungwe Morogoro tena wazazi fake walisimama kwa upande wa baba yangu umma ukidanganywa baba yangu wazazi wake wamefariki ilhali wako hai. Aliporudi mambo yalikuwa mabaya zaidi kwenye biashara zake mambo yakabadilika alifukuza wafanyakazi wake wote mpaka ndugu zake wa damu na kuajiri watu kutoka Uwata, alikataa malipo kwa njia ya dollar kwa kusema kwamba ni ushetani, wateja walimkimbia na kumwita kichaa! 😭 pesa alizofanikiwa kupata tunasikia amewekeza kwenye vitegauchumi vya UWATA… alipokuwa akija nyumbani kutusalimia ilimbidi aende kanisani akaungame kwa maana amefanya dhambi( huko walimbatiza mama yangu jina dellilah na kwamba yeye ni mchawi!😢) hata ilipobidi ndugu kwenda kumuona ofisini kwake ni lazima hao watu wa uwata nao wawepo hapo ofisini kusikiliza 🤦🏿.
Hali yake kiuchumi imekuwa mbaya mno waliomjua zamani na sasa wanahuzunika. Alikuwa baba, kaka, mume na mtu bora sana nitawalaumu UWATA siku zote za maisha yangu kwa kuwakosesha malezi ya baba wadogo zangu kwa maana si mapenzi tuu hata huduma hapaswi kutoa kwa watoto waliozaliwa na delila!
Unapoanza kumtafuta Mungu WAKATI yupo nawe sikuzote hayo ndio matokeo yake!!
Jamii za kilokole zina matatizo fulani FULANI hivi!!
Yaani Imani zinapozidi akili matokeo yake ndio hayo!!
Ulokole na kumiliki fedha nyingi ni mbalibali labda uwe mlokolet wa mchongo lakini mlokolet halisi kabisa huwa ni maskini wanaoishi KWA muujiza na hela ya kula tu!ukiona mlokole ni tajiri kabisa yaani tajiri haswa ujue huo utajiri ni wa mchongo tu kuna jambo anafanya nyuma ya pazia!!!!
KWA KAWAIDA ukiwa tajiri halafu siyo mlokole ukajiunga na ulokole lazima tu ufilisike na kia wa KAWAIDA!!!
Wa kwenda deep watanielewa!!!