Uwekezaji nyumba za kupanga


Watu wamekariri nyumba ,
50 mil huwezi kuiweka kwenye project ambayo itakufanya usubiri returns kwa miaka 20 plus ,
 
Hizo pesa za investment hii , utakuwa umetoa wapi labda ?
Umekopa?
Za urithi?
Za deal
Pensions?

Option rahisi naona kujenga nyumba za staili hii ni kama una pesa za urithi au za deal, lakini ikitumia mikopo ya benki hutoboi ,
 
Hiyo biashara ya nyumba zakupagisha ni biashara ya walio staafu na wajane, sio kwa kijana nwenye uwezo wa kuhaso inakua je niwekeze 100m kwa nyumba na kiwanja kila mwezi ni pate 500k. Wakati hata hiyo pesa nikiweka fixed deposite account benki ntapata 12% ya Liba au faida kila mwaka.
 
Exactly....hii ni retirement plan.
 
Kama ni kijana tafuta biashara ingine pambana kupitia hio biashara utajenga hizo nyumba kama retirement plan yako.
 
pole mtoa mada, lazima upate maneno ya kejeli toka kwa watu ambao hawana hata kiwanja...

sasa fanya hivi!

jenga apartments, achana na nyumba kubwa za familia, jenga chumba,sebule,choo na jiko with balcony iwe na executive finishing then weka hadi samani humo ndani za kisasa,,,,,fanya kukodishia kwa mtindo wa kisasa wa appartments,...utaniambia baadae, NB sebule chini an chumba chuu ie kigorofa
 
Hii biashara ni muhimu kuangalia soko la walengwa.
1. Nyumba karibu na chuo Kikuu, weka chumba chenye kitanda, meza y kusomea, jiko na choo laki moja kwa mwezi.

2. Watumishi wa umma, vyumba viwili-vitatu vya kulala. Sebule, jiko, choo na bafu.

3. integemeaq na eneo la kiwanja. Lakini kupangisha mashirika kwaajili ya maboss wao wanapenda nyumba nzima yenye master bedroom.
 
Nyumba ni asseti nzuri mno, na ukibahatika kupata place nzuri ukala kodi 500000 mpaka 1000000 per month umeula!
 
Aise..mm hapana kuna biashara zimepitwa na wakati..hii imo!
Sio kupitwa na wakati tu , ni biashara ambayo wanao ifanya hawako wazi kabisa na pesa wanazotumia ku fund hizo projects .

Ukiangalia gharama halisi za kufanya hizo projects, unaona kabisa sio viable kwa kila mtu
 
Uzuri waujenzi hii milioni 50 unaikusanya taratibu, ukipata milioni 3 unanunua matofali. Huwezi kwenda Chunya na milioni tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…