Mkuu, ila jamaa anachokiongea kina uhalisia fulani, mwaka 2019 nilienda Kakola yale machimbo ya namba 6 karibu na Bulyankhulu Gold Mine...nikakodi mwalo nikawa nanunua mawe kwa "manyani" na maduarani, napiga chabo na tathmin napeleka makarashani (namba 9) nakamua dhahabu, mara nachomwa(hasara) mara napata.(hapa lengo langu nikuze lundo niende plant)..kuna mama mmoja nilikuwa nampelekea dhahabu Geita , yule maza akatokea kuniamini kutokana kwamba nilikuwa namuuzia dhahabu yenye purity nzuri(93%-98%) tofauti na dhahabu ya (Nyankanga, Katoma hill na maeneo mengineyo ya Geita), yule maza akanipa million 4 nimkusanyie dhahabu, mimi hapo nilikuwa na mill zangu kadhaa so nikawa na nguvu za kutosha, kufika kakola kumbe mzungu kawapiga ban wachimbaji wadogo, watu wakafurushwa...ikabidi niende Segese-Ntambarale, kufika kule nikafanya kama Kakola, nanunua mawe nachenjua dhahabu, biashara ikawa ngumu kutokana kwamba kule chabo zake zilikuwa za kusua, nikabadilisha style(kumbuka yule mama alikuwa ananidai gram zake), nikawa nanunua "mbulaja", sasa dhahabu ikawa ya kusubir sana na cost of living ziko palepale, siku baada ya siku mtaji ukawa unapungua, nilikuwa na kalundo nikakauza bado ngoma ikawa ngumu, siku ya siku nimenunua mawe ili "niokoe" NILICHUMILA(hasara inayoweza kula robo tatu ya mtaji au mtaji wote)
Nikajifunza kitu toka siku ile
Yule anaenunua processed gold risk yake ni ndogo ukilinganisha na yule anayenunua mawe maduarani,
Biashara ya dhahabu kufirisika na kutajirika overnight ni kitu cha kawaida, na sio biashara ya kuiendea kichwa kichwa,
Alafu kuna mwamba alishawahi kuniambia "Kazi na Dawa" hii kauli siyo ya kuibeza kwenye biashara yoyote . ..
Kwa sasa nipo Geita "napiganisha"