Hapa sio vya kuchimbia tena....hapa ni jiko...yaan ww unaletewa dhahabu unaipima ubora wake unanunua! Kwahiyo hapa ni jiko na mzani wake...na mtungi ule mkubwa wa gesi,.haipungui 10m-15m! Na vibakuli vya kuchomea dhqhabu..kuna vibakuli.vyake maalumu maana kitu kinachomwa kwenye moto mkali!mara ya mwisho vibakuli bei ilikua 300k...hapo lazima uwe navyo si chini ya 6! Mzan wa kusoma purity ya dhahabu...mara ya mwisho ulikua btn 7-10m!hapa wanadai ya dubai ndo bora than china!
Sasa hii biashara lazima ujue hesabu! Hesabu zikikuchenga tunaambizanaga ....kuna zile kodi(mirahaba) ya serikali 7% usipoipigia hii mm.daily nakuletea mzigo maana ntapata faida nzuri mno daily....! So unawekq mtu walau wa form 6!
Yaan unaweza nunua mzigo wa 1m lakini makato yanafika hata 213,000! Sasa ww ukinipa yote 1m imekula kwako...Usipoikata hii ww utaning'inizwa mbeleni.itakula kwako!
Kakola kuna jiko walimuweka kilaza tulikula hela mno mno!
Hii shoga angu haina kuchafuka[emoji39]!hii hata ukibandika kucha haiswii[emoji3]!.uko ofisini na "dell" yako na kiyoyozi kikali kwa draw kuna kama 70m zinasubiri kuondoka[emoji3059]!tena na ulinzi wa mitutu kbs nje!
Siri ya hii biashara uwe na kauli nzuri...utapata wateja wanapanga folen kwako....! Na uwe loyal...mfano...mteja anakuletea dhahabu katoka nayo sehemu A, kila mchimbaj anajua area hii dhahabu zinasoma kuanzia asilimia 80_93%..ss wewe uje umshushe umwambie inasoma 75 hakika utamfukuza...ofcourse wanaibia hapo ila hakikisha hupishan naye saaana! Dhahabu ikisoma safi mfano 92% unauzia bei ya juu zaidi ya iloyosoma ya chini! Sasa wenye majiko wanachezea yale maji ya kupimia dhahabu...! Mtu anaamua kurudi na mzigo wake...!
Ah nna njaa mie !hope kidogo dogo utapata mwanga!