Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Sawa lakini ujue nyumba ina resale value
 
Naomba ramani yko mkuu. Hili nkipata pesa nijenge kama ww mkuu
 
Endelea kusave akiba kutokana na mapato ya kodi. usiache kufanya ukarabati mdogo mdogo na kuzifanya zizidi kuonekana mpya na kuongeza bei ya kodi kila mwaka
Ukarabati ni kitu muhimu kwenye majengo.

Na kama unakuwa karibu na majengo yako inakuwa rahisi lutembelea mara kwa mara na yale mapungufu unayolutana nayo unayafanyia kazi kuyarekebisha.
 
Nimeanza safari na mimi ya kutafuta hayo mamilioni nifanye uwekezaji 😜 vitu gani nizingatie
Zingatia sana kuweka akiba kabla hujatumia hela. Wengi huwa wanaweka akiba baada ya kutumia mshahara wake kwa mfano. Mimi niliweka utaratibu ambao mshahara unapoingia, zaidi ya nusu inakatwa na kupelekwa kwenye fixed account ambayo sina access nayo hata iweje. Save kadri ya uwezo wako, baada ya muda utapata kiasi ambacho unaweza fanya kitu.
 
Endelea kusave akiba kutokana na mapato ya kodi. usiache kufanya ukarabati mdogo mdogo na kuzifanya zizidi kuonekana mpya na kuongeza bei ya kodi kila mwaka
Asante mkuu. Ukarabati muhimu sana, ili nyumba zisichoke. Nazi manage kwa karibu sana, hivyo nitakua nafanya ukarabati kila mwaka, na kupandisha pia kodi kila mwaka (ndio maana nimeanza na hiyo 150K).
 
Hii business ya Airbnb inashika kasi sana kwa sasa bongo....! Sema inahitaji eneo strategic ambalo linafikika kirahisi
Eneo lifikike kwa gari hata kama ni mbali, liwe karibu na rami au utoke kabisa rami ufike, lisiwe uswahilini na vichochoroni, liwe nje ya mji kidogo sio katikati kwenye joto kali na makelele.

Otherwise basi eneo liwe sehemu expensive kama Masaki, Oysterbay na Mikocheni na hapo upangishe apartments za maghorofa na sio ujenge.
 
Mkuu naomba kuulza mfumo wa mashimo ya choo umetumia huu wa kisasa wanaosema unapoteza maji au ule tuliouzoea wa shimo kubwa na dogo?
 
Eeeh zaidi ya nusu unasave sasa hapo sii inabidi uwe na mshara wa kama million 10 hivi.
Ah wee sio mwezetu
 
landlord wangu ana units kadhaa zina zaidi ya maiaka 5.
Na sasa anaongeza nyingine na anampango wa kuongeza nyingine pia.

Inaonekana hii investment inalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…