Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Iwapo kutakua hamna maintenance kama mpangaji kaondoka inarudi. But hapo kuna operation cost zitakuja baada ya miaka miwili.

Pia bado anajenga ukuta. Akimaliza ataweka geti. Akimaliza wapangaji watataka paving.

So real return unakuja kuipata kuanzia miaka 8-10...
Ujanja ni kupangisha Vibachelor kama MANESI,MADAKTARI,WATU WANAOFANYA KAZI ZA KUSAFIRI SAFIRI .HAWA HAWAKAI SANA NYUMBANI.SO UHARIBIFU UNAPUNGUA.CHUKUA HIYO!!!
 
Mkuu huo ni uwekezaji mkubwa sana dunia nzima.
Na ni biashara ambayo ina vihatarishi vidogo sana (very low risk).
Halafu ni biashara inayolipa unapata kitu kinaitwa passive income
Achana na watu wanaotegemea miujiza ya Mwamposa.Hawana kitu wanajua🥱🥱🥱
 
Hawezi kuelewa huyo hao ndio wale wanaosema kujenga nyumba ya kuishi ni kupoteza pesa Sasa jiulize yeye anaishi porini hao ndio wanajikuata wamezeekea kwenye upangaji na mfukoni hamna hata mia watoto wanaanza kumuita mchawi anawatishia laana
Achana na hawa wafuasi wa motivational speakers,they are empty headed.Financial literacy iongezwe kwenye mtaala na ijitegemee kama somo.Hii nchi ujinga ni mwingi😄
 
Hii business ya Airbnb inashika kasi sana kwa sasa bongo....! Sema inahitaji eneo strategic ambalo linafikika kirahisi
Ndo mjifunze kununua maeneo yaliyopimwa.mpate njia na mitaa inayoeleweka iliyonyooka.


Unakuta mtu anahela na kashusha mjengo wa maana ila kajenga kwenye squatters huko😬😬😬😬
 
Ok sijaangalia vzr, nilikuwa nakushauri maana nina investment kama hiyo hapo kongowe na niliwahi kufanya kosa hilo hapo mwanzo
Japo nimejikita san kwenye self contained rooms only at half the price of your rent, ana half the costs of your investment
mkuu Spread this kama hutojali naona kuna vitu umeongea ila umetunyima minyamanyama😄😄😄
 
Wanakusini hawana hela.Njia ya kibaha inamnyororo wa thamani pia na bagamoyo nayo ni muundelezo wa tegeta na bunju.Huko ukipeleka hela huwezi jutia.
Yeah, na hiyo bagamoyo kuanzia gari za Arusha na Tanga zianze kupita kule basi ndio imezidi kuwa ghari, mapinga zamani ilikua viwanja bei chee ila sasa hivi sidhani kama hata viwanja venyewe vipo pale😅😅😅
 
Kwa structure ya nyumba aliyojenga, UTT bado ungekuwa uwekezaji mzuri kwake. Kwa maoni yangu. Service ya nyumba baada ya kuondoka kwa wapangaji huwa ni kubwa sana, wapangaji wengi wa units ni wapangaji shikizi ambao wanajiandaa kujenga nyumba zao. Wabongo si wastaarabu inapokuwa kwenye kuondoka, labda pawepo na mkataba mkali unaemlazimisha afanye service ya nyumba wakati wa kuhama.
Weka hoja mezani
 
Hii biashara ni nzuri hasa ukiwa kazini na mambo yako yanakwenda vzr.

Wakati naanza maisha nilikopa then nikajenga nyumba ya 3 rooms,

Baadae nikaongeza nyumba 2 za
wapangaji ya chumba na sebule

Kwa sasa nimepangisha zote, nyumba kubwa 270,000 na nyumba ndogo 2 kwa 150,000 each. Kila baada ya miezi mi3 nikawa nachukua hela

Matokeo
Niliweza Jenga nyumba self ya 2 bedroom for 2 yrs kutumia hela ya Kodi (of course iliegemea ukuta so initial cost nilikuwa nimeiweka na maybe plus small addition from mfukoni kwangu)

Kwa sasa nachukua Kodi ya 800,000 kwa mwezi na nazipokea kila baada ya miezi mi4.

Kwa sababu Niko kazini, all is going well na target yangu nikumaliza haka kamjengo Ka 2bedroom nilikokaanza mwaka huu kwa hela ya pango Tu. Yaani faida ya kuoangisha najengea.
Watoto wanasoma St.Likud au EMS.Maana it seems unamshahara mkubwa kidogo bandugu😄😄😄
 
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.

Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa.

Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).

Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana.

Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).

Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).

Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili.

Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit.

Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.

View attachment 3241776View attachment 3241777

Yule mwamba wa ile TRA yenyewe akiku-beep usiache pia kutuletea mrejesho
 
Yeah, yaani kibaha imefungana na mbezi for now... Huoni zamani watu walikua wanachukua viwanja kibamba na kiluvya ila kuna watu walidharau kwakuona mbali, ila check now tuko hapa tunaijadili kibaha😅😅😅
Bora viwanja vya kibaha ila ile miinuko ya kibamba,Bonyokwa,Maramba mawili na Kinyerezi siwezi kutoa hata mia mbovu kununua kiwanja maeneo hayo🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom