Ni aidha watu hawana elimu ama ufahamu wa kina kuhusu dini ama ni propaganda zimejaa kichwani ama wanapenda kusikia na kuona wanavyopenda. Binafsi nashangaa sana hasa humu jukwaani watu wakigombana kuhusu dini Fulani, kitu ambacho hakikusaidii chochote na si kwamba utaumiza mtu nk. Kwa Kila mtu akiishi vile dini yake inavyosema ilimradi hadhuru mtu kwani Kuna tabu gani?, wale wa mizimi wafuate mizimu Yao no problems na wengine pia, suala la Imani likimuingia mtu basi muache apambane nalo na si kumlazimisha aamini unavyoamini wewe, lazima tujifunze kuishi maisha yetu na kuacha kufuatiliana Ili basi Kila mtu apambane na Hali yake. Mbona hakuna tabu kuhusu hili, it's very simple.