Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Kuna kitu kidogo tu bado huja kielewa vyote ulivyo sema ni sawa, mungu ninae mzungumzia hapa yupo juu ya kila kitu hadi unacho kifikiria hasaivi
Hiyo ni kauli ya kiimani ambayo haina uthibitisho, haina mantiki wala haina ushahidi.

Hata mimi naweza kukuambia kuna kitu bado hujakielewa, kimba nililokunya leo asubuhi ndiyo Mungu, kimba hili lipo juu ya kika kitu hadi unachofikiria sasa hivi, na huwezi kuelewa hilo kwa sababu lipo nje ya uwezo wa mtu kuelewa.

Habari uliyoandika haina tofauti na hiki nilichoandika hapa.
 
Nnachoamini Mimi,

Hakuna kiumbe asiyeamini Hakuna Mungu, Bali kila kiumbe kina Mungu wake kinaemuamini, wengine mnaita "miungu"

Tatizo linakuja pale mnapotaka kutuaminisha kwamba Mungu wenu wa kwenye biblia na qurani kua ndio Mungu sahii.

Hao wengine mmewabatiza majina mabaya mabaya TU Kama majini,mizimu,miungu, misukule,frimasoni,mapepo n.k
Mungu ni nini?

Sifa gani zinafanya hiki kuwa Mungu na hiki kutokuwa Mungu?
 
Kuna jambo limenisukuma sana kuandika huu Uzi.
Mambo ambayo yanaendelea kuhusu uwepo wa mungu.
Kuna baadhi ya watu wa amini hakuna mungu nk.

Ni ingie kwenye point
Uwepo wa mungu una dhihirika kwa alama zake na viumbe vyake.

Hebu tutafakari kama hakuna mungu nani alieumba bahari, jua, mbingu, binadamu, wanyama hivi vitu vimetokea vipi kama hakuna alieviimba.

Leo hii hata ukimchukuwa mtoto mdogo wa miaka mitatu ukamuuliza nani kaumba mbingu atakujibu mungu.

Vipi mtu mzima mwenye akili timamu unashindwa kutambua hilo.

Yapo mambo mengi sana yana thibitisha uwepo wa mungu naweza kesha kuelezea kiufupi, Tufahamu mungu yupo na yeye ndo ametuumba sisi ili tumuabudu yeye tu.
Mungu yupo na ndiye anayetupa pumzi na uwezo wa kuziishi kesho zetu..
 
Ni ajabu Sana kuendelea kuamini vitabu vilipitwa na maarifa.

Sayansi kila siku wanaendelea kufanya tafiti Zaidi, na Ku update taarifa mbalimbali.

Vitabu vya Dini vinamapungufu mengi mpaka unajiuliza huyu mungu, mbona hana Masri sahihi
 
Kama mungu angekuwepo basi Hata huu Uzi usingekuwepo kabisa
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, si mchoyo wa kuwafunulia watu wajue uwepo wake.

Angekuwepo, angejiweka wazi kwa namna ambayo kila mtu angejua kwa uhakika uwepo wake, kwa namna ambayo, mjadala wowote wa kuwepo Mungu usingewezekana.

Ukiona kuna swali lolote, kuna utata wowote, kuna kitabu, tafsiri, muktadha au sintofahamu yoyote katika kuelewa uwepo wa Mungu huyo, ujue hayupo.

Hapo utapata siasa za watu, saikolojia za watu, hadithi za kutungwa na watu tu.

Watu wananuwezo mkubwa sana wa kutunga hadithi ya uongo na kuifanya ukweli.

Wamelichukua karatasi, wakachora mapichapicha, wanakwambia hii ni noti ya dola 100 za Marekani, ukiwa nazo karatasi hizi 12 thamani yake ninsawa na kazi zote anazofanya Mtanzania wa wastani kwa mwaka mzima.

Tumekubali kwamba karatasi hizo zina thamani kubwa sana.

Hatushindwi kutunga hadithi na kuipa thamani yabukweli ambao haupo.

Tofauti ni kwamba, kwenye kuipa paper money thamani, tunakubali hapa tumeipa thamani tu hii karatasi.

Kwenye Mungu, Mungu naye ni hivyo hivyo tu, watu wamemtunga, wakampa thamani, wakati hayupo.

Ila hawakubali tu hilo.
 
Tupe uzibitisho Kwamba hivi vitu vimeumbwa na mungu,
Mbona haendelei na huumbaji?
Labda utuambie nani amesha tengeneza mbingu yake na kama hakuna basi ujewe kitu ambacho anakifanya mungu binadamu hakiwezi,
Kuhusu kuendelea na umbaji
Mungu hana mapungufu kila kitu kimekamilika hakuna alicho sahau na ndo maana wana sayansi wanatumia neno "Tumevumbua" ina maana kilikuwepo mungu ametakasika na kila sifa ya mapungufu
Kuna watu watakuja kukupinga ety😂
Nawa suburi
 
Kama vilivyo complex hivi vyote vyenye high order hivi ulivyovitaja, bahari,jua, watu, wanyama, ni lazima viwe vimeumbwa na higher intelligence, basi complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa na higher intelligence.

Sasa, hapo hapo linakuja swali, kwa kanuni hiyo hiyo ya kwamba kilicho complex hakiwezi kuwepo tu, ni lazima kiwe kimeumbwa, hata Mungu wako naye atahitaji juwa aneumbwa, na aliyemuumba naye atahitaji kuwa na muumba, hivyo hivyo, bila mwisho.

Kwa hiyo, ukisema kuwa bahari, jua, watu ni lazima vimeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea tu, kimsingi hapo unasema Mungu hayupo, labda hujaelewa tu kwamba unajenga hoja kwamba Mungu hayupo.

Ni hivi.

Ama, hivi vitu complex ni lazima viwe vimeumbwa, ama si lazima.

Kama si lazima viwe vimeumbwa, hapo Mungu hahitajiki, kwa sababu kama ulivyosema, unatumia dhana ya kwamba Mungu kaumba kudhihirisha Mungu yupo. Kama vitu hivi si lazima viwe vimeumbwa, basi Mungu hahitajiki.

Kama ni lazima viwe vimeumbwa, basi huyo unayemuita Mungu naye ni lazima awe kaumbwa, na kama ni lazima awe kaumbwa, huyo si Mungu.

Sijui hata kama una uwezo wa kuelewa hizi hoja.
Kuna siku mambo ya kiroho yalisibitika kisayansi?
 
Kama vilivyo complex hivi vyote vyenye high order hivi ulivyovitaja, bahari,jua, watu, wanyama, ni lazima viwe vimeumbwa na higher intelligence, basi complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa na higher intelligence.

Hivi vyote ni "Self evident truth" kuwepo kwake tu kunathibitisha uwepo wa aliyefanya vikawepo. Huyo aliye fanya hivi vikawepo ni Mjuzi mwenye nguvu.
Sasa, hapo hapo linakuja swali, kwa kanuni hiyo hiyo ya kwamba kilicho complex hakiwezi kuwepo tu, ni lazima kiwe kimeumbwa, hata Mungu wako naye atahitaji juwa aneumbwa, na aliyemuumba naye atahitaji kuwa na muumba, hivyo hivyo, bila mwisho.

Kwanza type sababu tano ambazo zinaonyesha ulazima wa Muumba awe na chanzo.

Nukta ya pili infinity hai exist, Sasa sijui ni utoto au ni upungufu wa akili, kulazimisha lisilo kuwepo likawepo. Hakuna kitu "Bila mwisho".

Yaani hakuna Infinity, Mola ndio wa mwanzo na ndio wa mwisho.

Nani amekwambia Kuna "Bila mwisho" ? Hata hiyo Sayansi yenu dhaifu hili pia inalikataa
Kwa hiyo, ukisema kuwa bahari, jua, watu ni lazima vimeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea tu, kimsingi hapo unasema Mungu hayupo, labda hujaelewa tu kwamba unajenga hoja kwamba Mungu hayupo.
Hili tatizo la kiakili, Sasa hapa umejengwa hoja gani, juu ya kutokuwepo kwa Mungu au nukta ipi inaonyesha ya kuwa Mungu hayupo, wakati vyote vimeumbwa na aliyeumba hajaumbwa ? Mbona mnajenga hoja kitoto na kubitimisha kirahisi pasi na kujadili hoja ?
Ni hivi.

Ama, hivi vitu complex ni lazima viwe vimeumbwa, ama si lazima.

Kama si lazima viwe vimeumbwa, hapo Mungu hahitajiki, kwa sababu kama ulivyosema, unatumia dhana ya kwamba Mungu kaumba kudhihirisha Mungu yupo. Kama vitu hivi si lazima viwe vimeumbwa, basi Mungu hahitajiki.
Vimeumbwa na hakuna kinyume chake, mpaka uje uthibitishe ya kuwa aidha havijaumbwa( yaani vimejiumba) au vimetokea pasi na chochote na viwili hivi ni muhali.
Kama ni lazima viwe vimeumbwa, basi huyo unayemuita Mungu naye ni lazima awe kaumbwa, na kama ni lazima awe kaumbwa, huyo si Mungu.

Sijui hata kama una uwezo wa kuelewa hizi hoja.
Hapa kwenye lazima awe ameumbwa unatakiwa utupe sababu walau tano zinazo onyesha ya kuwa Muumba lazima awe ameumbwa.

Kisha ututhibitishie ya kuwa je ni kweli "Infinity" ipo ? Yaani utuambie huko "Bila mwisho" ni wapi na umejuaje uwepo wake na maana yake ni nini ?
 
Hiyo ni kauli ya kiimani ambayo haina uthibitisho, haina mantiki wala haina ushahidi.
Kila siku huwa nawaambia nyinyi kwanza mlitakiwa mjifunze maana ya haya maneno. Nani alikwambia Imani haithibitishiki ?

Msingi wa mantiki ni nini ? Mantiki ni nyenzo tu kama ilivyo kisu, au panga au Bunduki, ina sifa zake anuai, bali ina madhaifu mengi kuliko ukamilifu. Vipi iwe kama kigezo cha kuujua ukweli ?

Onyesha wapi Haina ushahidi na utuambie kwako wewe ushahidi ni nini ?
 
Hata mimi naweza kukuambia kuna kitu bado hujakielewa, kimba nililokunya leo asubuhi ndiyo Mungu, kimba hili lipo juu ya kika kitu hadi unachofikiria sasa hivi, na huwezi kuelewa hilo kwa sababu lipo nje ya uwezo wa mtu kuelewa.

Halafu kwa akili hizi kweli usiseme Mungu hayupo ? Hili muhali kwenu.

Jifunze kwanza maana ya neno Mungu ili ukitoa mifano upatie katika hiyo mifano.

Mungu ni Muumba, kwahiyo wewe Kimba ulilokunya ndio limekuumba wewe ? Sasa huu si uhayawani.

Wewe umejuaje kama Kimba lako juu ya kila kitu na umelinya wewe mwenyewe ? Aisee Kuna uchizi wa sampuli nyingi ila wa kwako umechupa mipaka. Yaani kwa ujinga wako unashindwa kuona ya kuwa Kimba ulilo linya limetoka kwako maana yake wewe ndio umeamua ulinye halafu liwe juu ya kila kitu ?

Nimecheka sana. Ila kila siku nawaambia katika kutoa mifano mlifeli tangu zamani, yaani hamuwezi kabisa.
 
Back
Top Bottom