Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Ukitaka kupambana pambana na kubwa la maadui
Kiranga huyu Mwamba ndo mpingaji mkuu wa hoja za Mungu,sasa katika kusoma kwa kutulia nimegundua yafatayo kuhusu yeye
1.Ni mtu anayemjua Mungu vizuri na ameamua kupotosha na coat baadhi ya maneno yake
"Kiukweli, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote, atajulikana, atajulikana na viumbe wote, atajulikana na viumbe wote bila utata, hatahitaji kitabu, tafsiri, nuktadha, muongozo, mjadala ili aeleweke bila utata wowote ule."
Kaanza na neno kiukweli ,linatosha kuonesha huyu Mwamba Mungu anamjua vyema
2. Ni mtu ambaye dishi limeyumba na ana mafadhaiko sana kwenye hii dunia

"Hata mimi naweza kukuambia kuna kitu bado hujakielewa, kimba nililokunya leo asubuhi ndiyo Mungu, kimba hili lipo juu ya kika kitu hadi unachofikiria sasa hivi, na huwezi kuelewa hilo kwa sababu lipo nje ya uwezo wa mtu kuelewa."
3.Ni Muabudu shetani
"Hakuna mtu aliyetatua mikanganyiko ya kimantiki inayojitokeza katika hoja na dhana za kuwepo Mungu, kama vile "the problem of evil", kwa nini Mungu hajioneshi kwa uwazi usio na utata wowote kwa wote, freewill's"

4.Ni mtu mwenye elimu uchwara asiye elimika ,hapo tunaona ana coat vi theories vya kumwelezea Mungu KWA kutumia sayansi

5.ana tatizo la kisaikolojia
" "ili awe Mungu lazima asieleweke" hapo tayari umeacha mlango hata mimi kukuambia kuwa Mimi ndiye Mungu mwenyewe, ila sieleweki tu kuwa mimi ndiye Mungu mwenyewe."
Sasa hiyo tu inatosha kukueleza kuhusu huyu mtu yote yanaweza kuwa majibu au Moja Kati ya hayo,
Ila huyu ndugu yetu anaitaji msaada wa haraka ,unaweza kuta siku Moja akabwia madawa akafa maana nahisi dishi halipo sawa
 
Mkuu,

Asante sana kwa kunijulisha hili.

Liko wazi sana lakini wengi wanajibaraguza kutoliona.

HIstoria ya hapa JF imeonesha kuwa kadiri muda unavyokwenda, mwanga wa ujuzi unamulika ujinga wa imani na kutupa ukweli unaothibitishika vizuri zaidi kimantiki.

Mimi ni mshika mwenge tu, miongoni mwa wachache wasiochoka wa miaka ya zamani.

Kuna kizazi cha kuhoji kinakuja, watu wa imani wakishindwa kujibu maswali ya Kiranga, watakuwa na kazi kubwa sana kujibu maswali ya kizazi kipya.

Ninachoweza kusaidia zaidi jamii ni kunyumbulisha na kutafsiri haya mambo kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili.

Nimegundua mambo mengi hayaeleweki kwa sababu ya lugha tu.
 
Hii post nzima ni logical fallacy ya ad hominem attack.

Ad hominem attack ni kuacha kujadiki hoja, na kumshambukia mtka hoja.

Ulichoandika hapo juu, 1,2,3,4,5 kote unamshambulia Kiranga, badala ya kuchambua hoja alizotoa Kiranga.

Yani, badala ya ku address hoja zilizoandikwa na Kiranga, umeamua kumshambulia Kiranga personally.

Hili linaonesha huna hoja, unataka kuzima hoja kwa kumshambulia mtoa hoja.

Ad hominem attack, logical fallacy.
 
Kukulipizia,

Kwanza jifunze tofauti ya "coat" na "quote" kabla ya kujibizana nami.

Ukianza kuandika "coat" kwa kumaanisha "quote", unanipa signals kwamba you are semi literate, at best.
 
Sema mkuu huwa unalazimishaga mambo mtu alishakupeleka ignore list na hakujibu mara nyingi tu.

Ila wewe kulazimisha, acha hizo bana mtu kashakataa kuongea na wewe basi.
 
Enyi waamini mnijibu haya machache.

1. Ikiwa Mungu huyo mnayemsoma na kumuamini kwenye vitabu vyenu vitakatifu anasema alimuumba Adam na Hawa, watu hawa wawili walikuwa na rangi ipi ya ngozi na kilikuja kubadilika kipi leo hii tukawa na varieties za human races?

2. Mnatuaminisha Mungu ni mkamilifu na aliumba kwa Ukamilifu viumbe wake. Hawa Viwete, Mabubu, Viziwi, Vipofu wao waliumbwa na nani na hiyo dhana ya ukamilifu inakamilikaje ikiwa kuna upungufu wa dhahiri unaonekana?

3. Ikiwa Aliumba kwa kutamka na ikawa, tafsiri yake ni kuwa kila kitu kilikamilika kwa muda mmoja kikakaa mstarini kwa muda huo mmoja na ikadumu hivyo. Ni kipi kinachofanya upande mmoja wa dunia uwe ni asubuhi wakati kwingine ni usiku!?

Nijibuni hayo kwa kuanzia halafu nitakuja na mengine.
 

Huyu mtu anakuja mulemule hivi ni haki unataka kumjadili Mungu ambaye ni very complex spiritual staff,wakati hujui hata maana ya energy,
Okay kukusaidia
Energy (nishati ) ni Kani ya Mungu ya ufanyaji kazi katika ulimwengu wa mwili,ambayo sayansi finyu imeshindwa kueleza mwanzo ,chanzo na asili yake,hivyo ikampa ushindi Mungu Kwa kutengeneza principle ,inaitwa principle of conservation of energy ,ndio principle kuu ya ulimwengu na ndio hapo tofauti ya uungu na sayansi ilipo
Katika ulimwengu wa roho ipo na inaitwa "roho mtakatifu" walokole wanaifahamu sana japo mm SI mlokole ni mcha Mungu
2 Neno kwanini ni dhana ya mkanganyiko wa akili na siyo tu mtazamo,mfano
"Kwanini kila siku Mimi tu mke wangu ,ananijibu vibaya."
Lakini Kuna mtu pia mke wake anamjibu vibaya ukimuuliza anasema "sasa kama kaamua kujibu mm nijafanye,'
Hapo Kuna dhana mbili ya kwanza Kuna anayeona kujibuwa vibaya ni tatizo Ili kutafsir tatizo katumia Neno kwanini lakini Kuna anayeona kujibiwa vibaya ni maamuzi na haki ya mtu.
Anyway turudi kwanini Yako umeitengeneza wewe ila Haina mantiki maana kwanini Yako imebeba umimi, haiko general ipo kiselfish sana, kwanini afanye hivi lakini hujiulizi vilevile kwanini asifanye hivi
3.Thibitisha evil problems ni zipi maana hakuna evil ni real sense ,Ivo ni dhana ya kiimani kama Mungu alivyo wa kiimani,
Kama unaamini evil basi automatic unaamini Mungu

B.kuhusu utendaji kazi (how God is operate) ni jambo binafsi la Mungu ,kuwa ameumba evil au ameumba chochote kile ameamua ni kama wewe uchukue udongo mfinyanzi utengeneza gari au nyumba ya udongo,hivyo mode ya operation haihusiani ni uwepo,hapo juu nimekupa mfano wa William luto ,simjui hukuuelewa
Hapangiwi na wewe why umpangie ,mfano sisi tuje kwko tukupangie namba ya kuongoza nchi wakati wewe ni rais na katiba imekupa mamlaka no one to ask why?
4.Sayansi unayoiamini imethibitisha uwepo wa roho
Kupitia
A. Meditation
B.astral body projections na zipo nyuzi nyingi humu kuelezea .
Additional questions??🥳🥱
 
Your browser is not able to display this video.
 
MM si AMINI KAMA MUNGU YUPO
 
Twende hivihivi tutaelewana tu
 
Hawana tofauti na punda kuongea kwenye biblia, malaika wa mungu kuua kambi nzima, kushushia watu wake chakula.

Hawa wameenda mbali zaidi nyota ni kwa ajili ya kuwarushia maadui hizi hekaya huwa zinafurahisha sana
 
Ujue kiranga naweza kukupa task ambayo ubongo wako ukashindwa hata kuimagine,Vuta picha kama universe is empty ingawa ukisema universe nayo ni something can you imagine emptyness? text za bigbang theory Hii theory ni ukifikiri wa hali ya juu sana ipitie pitie utapata source Universal mind,then GOD
 
Hapana unapogundua unabishana na mtu mwenye tatizo,siyo mbaya ukamjuza utamsaidia kimatibabu
1.hoja namba Moja ni kweli kwasababu nime quotes maneno Yako,na wewe ni muumini mzuri tu unayejitoa ufahamu,inahitaji jicho la tatu kukuelewa vizuri
2.hoja namba mbili kuyafananisha kinyesi na mungu,ni kutokuwa sawa kichwani inamaana huijui maana ya Mungu hata kwenye kamusi huru,
Labda nikupe maana ya kinyesi
"Ni mabaki ya chakula Baada ya kuondolewa virutubisho muhimu na mwili na yanatokea kwenye tundu la haja kubwa" maajabu ni kuwa umeyaita Mungu hivyo inaonesha wazi dishi lako limeyumba wahi hospital haraka😂😂
3.Ni maneno Yako yakatae hapa ni zidi kuprove dish limeyumba kuhusu swala la kutukuza evil problems kwamba ni more powerful
5.Hoja ya kujiita wewe mungu,inamaana hujui maana ya Neno Mungu na matumizi yake ,hivyo inanipa picha kuwa may be unatatizo la afya ya akili wahi hospital,najua Kuna wataalamu wa magonjwa ya akili waanze na huyu ndugu yetu tusije mpoteza jukwaani ni mkongwe na Mimi nimemkuta humu,lakini pia inaonekana umri umeenda na badhi ya nuts zimelegea SI tatizo umri ukienda ni kawaida sana.
 
Unaweza kuthibitisha nishati ni kani ya Mungu?

Mungu ni nini?
 
Ashindwe kujua maana ya energy aweze kuelezea BigBang theory kuwa seriously basi kidogo mkuu
 
Umepata wapi kujua kama Mungu ni complex? Vilivyoumbwa ni complex kwetu lakini kwa Mungu vyote ni simple.
 
Unaweza kuthibitisha nishati ni kani ya Mungu?

Mungu ni nini?
Waoo Sasa tunaanza kuelewana
Nataka nikujibu katika nadharia mbili ya kisayansi na kiimani
Mungu kupitia Wikipedia imeeleza kuwa ni"Mungu ni jina lenye asili ya Kibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu."

Ila kiimani Mungu ni roho.
Roho ni imagination staff ya utendaji kazi ,sawa na energy ni tangable staff ya utendaji kazi isiyoshikika na haijulikani asili yake ,Sasa
Kama roho na energy Zina sifa sawa , kisayansi tunasema ni directly proportional .
Vile vile Mungu ni directly proportional na spirit (roho) basi automatic energy chimbuko lake ni Kwa Mungu.
Additional questions please 🥱🥱🥳
 
Ashindwe kujua maana ya energy aweze kuelezea BigBang theory kuwa seriously basi kidogo mkuu
Mkuu,

Kukuuliza energy ni nini maana yake ni kwamba sijui maana ya energy?

Unaelewa hata Socratic method ni nini?

Naanza kunusa ignorance on your part.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…