Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Karata tatu ni uchawi?
Kwani hapa tunazungumzia karata tatu au huo ulikiwa mfano tu..... Hivyo basi kwenye karata inaweza kuwa tricks na uchawi unawez kuwa ni tricks pia lakini whether ni tricks au sio haiondoi kwamba uchawi upo kwa sababu hata ukiuita ni tricks je unaweza thibitisha...
 
Acha na mimi ,niandike kitu kidogo kumtetea Mungu huyu ninaye Muabudu.
Kwanza kabisa tuache kuweka haya mambo pamoja Mungu na dini,
-wakosoaji wengi sana wa Mungu wamejikita sana katika kukosoa katika misingi ya dini,na hivyo kukosa uhalali wa kukosoa kuhusu Mungu.
Maana Mungu si dini,Mungu akuwahi kuleta dini bali dini imeletwa na wafuasi na mitume na mtoto wake kiimani ,
pia ni njia tu ya kumtafuta au kutaka kumwelewa huyo Mungu, ambayo imefanikiwa kwa kiasi kidogo au haijafanikiw kabisa, yoyote atakaye bisha asiingize udini. Kwanza tuanzie hapo alete facts kupinga.
-Wengi wanaleta theories za kisayansi ambazo sayansi yenyewe si kamilifu ,angalia kwenye sayansi twapaswa kugundua tatizo kabla ya kwenda kuweka mawazo yetu,. Na kuyafanyia majaribio, waoo tuna pata dhana mbili
1 . Sayansi si kamilifu KWA sababu haijitoshelezi (imekuta tatizo)yenyewe si yakwanza bali inafuata tatizo. Kwasababu Mungu si tatizo so sayansi inashindwa kumuelezea vizuri,
-haina uwakika,
-na inabadilika badilika (chochote kinachobadilika si cha asili) kwahiyo sayansi si asili.so sayansi haiwezi ongelea kitu static kwasababu ni dynamic angalia mfano mabadiliko ya hali ya hewa sababu haswa Moja isiyobadilika ni nini ?zipo theories nyingi ambazo ni mitazamo,sayansi pekee haitoshi mjadili Mungu KWA sababu haijitoshelezi inaitaji update while Mungu yupo static na anajitosheleza
2. Msingi wa dini -nawenyewe una mapungufu kibwena ,Moja Mungu hajawahi Mwenyewe kusema ipi ni ipi,vitabu vya dini vimeongea" shikilia pale ulipo KWA siku hizi za mwisho na utende matendo mema." Kwahiyo hakuna dini sahihi ila ipo imani sahihi
3. Mungu ni roho-acha roho zijadili huwezi mwili ukajadili roho ila roho inaweza kujadili roho nyenzie na huu ndo Msingi wa kumjadili ,Mungu.
Nataka ubishe kama huna roho watakati sayansi imeongelea mfumo wa kutoa roho nje"astral body projection'
4.Mungu kiimani -kwasababu hatuna access ya roho alternative is" the faith'"
Vitabu vya dini nazungumzia biblia imesema wazi , imani ni mambo yanayotarajiwa ,na ni bayana ya yale yasioonekana - waebrania.
Huu ni mfumo tunaofundishw kwenye dini Ili at least kumuelewa Mungu,kumbuka Mungu ni roho na sisi ni miili,na hatuwezi control roho zetu alternative ni imani
Sasa kwanini mmnaleta mambo yasioonekana kwa yanayooneka ,kama unaamini kirusi ambacho hakionekani kipo KWA nini usiamini Mungu?
Utasema kirusi kipo scientific proved,na tunajua science ni dynamic na haijitoshelezi basi twende field tukafanye research zaid ku prove uwepo wa Mungu.
5.Science yetu ni ndogo ndogo duchu kupitiliza imagine science yetu haijatupa hata majibu ya nini kipo katika kina cha chini kabisa cha maji cha marina trent,kwamba je kwanini kanii za energy za waveza maji ni kubwa kama bomb la nyukria lakini kuna samaki?
Na lapili hatujaweza hata kwenda hapo Mars ,je tutajua nini kuhusu aliyeziumba hizo sayari zote na mjumo wake wakati hayupo hapo?
Ni kama wewe unataka kuonana ana Kwa ana kuunda urarafiki na rais wa marekani kumuelezea shida zako wakati hata nauli ya kutoka sehemu Moja ya mkoa uliopo hadi mwingine hauna.
Na wakati utaratibu upo wa kupitia ubarozini wewe unataka uwende direct ofisini white house Utaweza?
6.Tusiishie hapo mwanasayansi yoyote ni mtu mwenye imani ,science yoyote ina anza na assumption ndo inafata provement ,
Sasa kama sayansi yetu bado inaturuhusu kuwepo kwa assumption y tuforce kwenda kwenye provement wakati hata kuzuia elninyo tungeshindwa je tutaweza vingine vikubwa zaidi
**Nitaendelea ,nakaribisha maswali na majibu
 
Miaka mingi imepita tangu nilipotoa kidau kwa mchawi yeyote atakayeweza kuniroga vidole vyangu visiweze ku type, nisiweze kuja JF kuandika.

Mpaka leo hakuna mchawi akiyeweza kufanya kazi hiyo.

Cc Nyani Ngabu
Aisee unajifanya mjanja eh? Ngoja sasa niwacheki wataalamu kutoka Gambosi 🤣.

IMG_2279.jpeg

Unauona huu mti? Sasa hapo ndo penyewe makao makuu ya hao wataalamu.

Ila tusilaumiane tu….😀

IMG_2273.jpeg
 
Ili awe Mungu lazima asieleweke,mtoto wa miaka 5kushuka chini anaamini baba yake ndo mwanaume bora na mwenye nguvu kupita wote ,na hii ndiyo Msingi halisi Ili heshima yake ibaki lazima pawe na gape ki fikra Kati ya Muumba na waumbwa, ina maana Kati ya Muumba na waumbwa hawawez kuwa na mawazo sawa,Ili kutenganisha.

Bisha kila kitu lakini uwepo wa Mungu unathibitika katika monitoring.
Unaamka asubuhi,nan kakuamsha ,kibofu kinajaa kinaleta signal kwny ubongo nataka ku urinate ,moyo unapinga mara 60, nani kaweza coding chakula kinachakatwa KWA masaa 3,
Sayari zinazunguka jua,na usiku na mchana unatokea KWA dunia kujizungusha ufikirii hizo programming code ,assume y it's take 24 hours huoni ni programming? Au unazani ni bahati mbaya.
Mbegu za mwaume kutengenezwa kila siku na mwanamke kabla hajazaliwa na kukoma before 40,don't you see it's code? What if mbegu zitengenezwe hadi kufa.
Y kuna kufa n hatuwezi kurenew maisha so don't you see it's prog na
Assume ukila kitu kichafu mwili utatoa signal KWA kutapika na kuharish it's not programming,any signal is coded with coder ?
Usisahau ishu ya energy ,Mungu katupa urithi mmoja wa energy ,na akili ,mkosoe Mungu KWA principle za energies na siyo theories za wanasayansi viduchu duchu nimemuona jamaa mmoja anatumia mitazamo ya watu anaiita fact uyo jamaa anajiita Kiranga mkosoe Mungu KWA principle na siyo theories ,theories and laws ni man made na hazina uhalithia
 
Kuna jambo limenisukuma sana kuandika huu Uzi.

Mambo ambayo yanaendelea kuhusu uwepo wa Mungu.

Kuna baadhi ya watu wa amini hakuna mungu nk.

Ni ingie kwenye point.

Uwepo wa mungu una dhihirika kwa alama zake na viumbe vyake.

Hebu tutafakari kama hakuna mungu nani alieumba bahari, jua, mbingu, binadamu, wanyama hivi vitu vimetokea vipi kama hakuna alieviimba.

Leo hii hata ukimchukuwa mtoto mdogo wa miaka mitatu ukamuuliza nani kaumba mbingu atakujibu mungu.

Vipi mtu mzima mwenye akili timamu unashindwa kutambua hilo.

Yapo mambo mengi sana yana thibitisha uwepo wa mungu naweza kesha kuelezea kiufupi, Tufahamu mungu yupo na yeye ndo ametuumba sisi ili tumuabudu yeye tu.
Hakika, asingekuwepo dunia nzima isingekuwa inataabika na migogoro ya Israel na Wapalestina; fikiria tu hiyo nguvu ya sote kuvutwa huko inatokana na nini? ...

Zab 53:1 : Mpumbavu amesema moyoni mwake, HAKUNA MUNGU😭😭
 
JF wananiangusha sana, ila labda wanaona hauko serious
Si kwamba wanaona siko serious. Hakuna uchawi wa kuniroga. Hakuna uchawi.

Habari nyingi zinazosemwa kuwa ni uchawi zina explanation nzuri tu isiyohusisha uchawi, au ni habari ambazo hazijapata explanation lakini hilo halimaanishi ni lazima ziwe uchawi.
 
Kwani hapa tunazungumzia karata tatu au huo ulikiwa mfano tu..... Hivyo basi kwenye karata inaweza kuwa tricks na uchawi unawez kuwa ni tricks pia lakini whether ni tricks au sio haiondoi kwamba uchawi upo kwa sababu hata ukiuita ni tricks je unaweza thibitisha...
Unajuaje huu ni uchawi na huu si uchawi ni kitu nisichokijua tu?
 
Aisee unajifanya mjanja eh? Ngoja sasa niwacheki wataalamu kutoka Gambosi 🤣.

View attachment 2837881

Unauona huu mti? Sasa hapo ndo penyewe makao makuu ya hao wataalamu.

Ila tusilaumiane tu….😀

View attachment 2837891
Mti mpaka umeweza kupigika picha na picha ikawekwa JF hakuna uchawi hapo.

Makao makuu penyewe nilitegemea pawe hapaonekani kwenye picha hivi, kila ukipiga picha picha inaungua kwa namna ambayo sayansi haiwezi kuelezea 🤣🤣🤣
 
Ili awe Mungu lazima asieleweke,mtoto wa miaka 5kushuka chini anaamini baba yake ndo mwanaume bora na mwenye nguvu kupita wote ,na hii ndiyo Msingi halisi Ili heshima yake ibaki lazima pawe na gape ki fikra Kati ya Muumba na waumbwa, ina maana Kati ya Muumba na waumbwa hawawez kuwa na mawazo sawa,Ili kutenganisha.

Bisha kila kitu lakini uwepo wa Mungu unathibitika katika monitoring.
Unaamka asubuhi,nan kakuamsha ,kibofu kinajaa kinaleta signal kwny ubongo nataka ku urinate ,moyo unapinga mara 60, nani kaweza coding chakula kinachakatwa KWA masaa 3,
Sayari zinazunguka jua,na usiku na mchana unatokea KWA dunia kujizungusha ufikirii hizo programming code ,assume y it's take 24 hours huoni ni programming? Au unazani ni bahati mbaya.
Mbegu za mwaume kutengenezwa kila siku na mwanamke kabla hajazaliwa na kukoma before 40,don't you see it's code? What if mbegu zitengenezwe hadi kufa.
Y kuna kufa n hatuwezi kurenew maisha so don't you see it's prog na
Assume ukila kitu kichafu mwili utatoa signal KWA kutapika na kuharish it's not programming,any signal is coded with coder ?
Usisahau ishu ya energy ,Mungu katupa urithi mmoja wa energy ,na akili ,mkosoe Mungu KWA principle za energies na siyo theories za wanasayansi viduchu duchu nimemuona jamaa mmoja anatumia mitazamo ya watu anaiita fact uyo jamaa anajiita Kiranga mkosoe Mungu KWA principle na siyo theories ,theories and laws ni man made na hazina uhalithia
Mungu kutoeleweka kwa uwazi, bila utata, kwa wote, ni moja ya classic arguments against the existence of God.

Ukishaanza na "ili awe Mungu lazima asieleweke" hapo tayari umeacha mlango hata mimi kukuambia kuwa Mimi ndiye Mungu mwenyewe, ila sieleweki tu kuwa mimi ndiye Mungu mwenyewe.

Kwa sababu ili niwe Mungu, ni lazima nisieleweke uungu wangu.

Kiukweli, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote, atajulikana, atajulikana na viumbe wote, atajulikana na viumbe wote bila utata, hatahitaji kitabu, tafsiri, nuktadha, muongozo, mjadala ili aeleweke bila utata wowote ule.

Ukishaona Mungu anajadiliwa, anaelezewa, ameandikwa, anatafsiriwa, anawekewa muktadha, anahubiriwa, etc, ujue hakuna Mungu hapo, hizo ni siasa za watu tu hizo.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kutojitambulisha ajulikane bila utata ni ukatili mkubwa unaosababisha vita vya kidini, migogoro ya kimataifa, crusades za maelfu na maelfu ya miaka.

Mungu mwenye tabia hizo (ujuzi wote, uwezo wote, upendo wote) hsi mkatili hivyo.

Ama Mungu mwenye tabia hizo yupo, na watu wanamuelewa bila utata, ama watu wanamuelewa Mungu huyo kwa utata na Mungu huyo hayupo.

Watu wanamuelewa Mungu kwa utata, ndiyo maana mijadala hii haiishi hapa JF.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.
 
Mpaka sasa.

1. Hakuna mtu aliyethibitisha Mungu yupo.

2. Hakuna mtu aliyetatua mikanganyiko ya kimantiki inayojitokeza katika hoja na dhana za kuwepo Mungu, kama vile "the problem of evil", kwa nini Mungu hajioneshi kwa uwazi usio na utata wowote kwa wote, freewill's incompatibility with God's perfect knowledge, etc.

3. Hakuna mtu aliyeweza kutatua mikanganyiko ya kimantiki ya kwenye vitabu vya imani vinavyojinadi kuwa ni vitakatifu na vya Mungu, kama Quran na Biblia, kwa mifano ya kuanzia tu.

Haya yote yanatokana na ukweli kwamba, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hayupo kiuhalisia. Mungu huyu ni muhusika wa hadithi za kutungwa na watu tu, nje ya hadithi hizo, Mungu huyu hayupo.

Kama unabisha, tatua masuala yaliyoorodheshwa hapo juu katika 1, 2 na 3.
 
Swali zuri. Nakujibu kwa swali, unakubali Kuna mwanzo yaani wa kwanza katika binadamu ? Huyu wa kwanza alitokeaje mpaka ukawepo wewe ? Je alitokana pasi na chochote au alijiumba yeye mwenyewe ?
Sifahamu kwa hakika,

Lakini kwanini unadhani ni lazima awepo wa kwanza tu?

Kwasababu Inawezekana asiwepo mtu mmoja pekee wa kwanza ambae ndiye alisababisha wengine kuwepo, (Elewa neno inawezekana),

Ushawaza uwezekano wa kuwepo wengi!?

Kwanini unauliza swali ambalo umelijenga katika mtindo wa kwamba kuna mtu mmoja tu asababishe uzao wote tulionao hapa duniani!?

Na hata nkikubali wazo lako, vipi kama mtu huyo alijiumba yeye mwenyewe kutokana na either reaction za kikemia miaka mingi iliyopita ila bado hatujajua tu!?
 
Mti mpaka umeweza kupigika picha na picha ikawekwa JF hakuna uchawi hapo.
Lakini, hata kama kuna uchawi, kwa nini picha ishindikane kupigika?

Kama hakuna mtu/ mchawi ambaye alikuwa amelenga kufanya vitu vyake ili kamera isifanye kazi, huo uchawi ungefanyaje kazi?

Ili uchawi ufanye kazi, si kwamba ni lazima mtu au-activate?
Makao makuu penyewe nilitegemea pawe hapaonekani kwenye picha hivi, kila ukipiga picha picha inaungua kwa namna ambayo sayansi haiwezi kuelezea 🤣🤣🤣
Wenyeji niliwauliza swali kama ulivyoeleza hapo. Wakasema kwamba kama mtu umeenda kwa amani na si kwa shari, hayo mauzauza ya kichawi huwezi kuyaona.

Wengine wakasema eti ni mpaka upewe ‘green light’ na fundi [mganga/ mchawi] ndo uweze kuyaona hayo mambo.

Binafsi nikaona ni mwendelezo ule ule tu wa visingizio.

Waumini wa hayo mambo hawawezi kuyathibitisha.

Hawawezi kuyathibitisha kwa sababu ni mambo ya uongo tu.

Ukiwabana wakuthibitishie, wanaleta visingizio.
 
Ni ngumu kama unataka kulazimisha Mungu ambaye hayupo awepo.

Vinginevyo unaweza kuthibitisha kimantiki kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hayupo, kama vile unavyoweza kuthibitisha 10 si square root ya 2 katika base 10 math.
😂😂😂

Kiranga wewe unajulikana jf nzima kuwa wewe ni Atheist.

Hivyo lazima ukane uwepo wa Mungu vikali mno.

Ila kitu ambacho nimeonaga mimi ni kwamba "wanao sema Mungu yupo wanapata ugumu mno kuthibitisha hilo ( hoja ni chache na hazina mashiko sana maana ni za kufikirika tu), na wanao sema Mungu hayupo wana hoja zina sound angalau kuliko wanaosema yupo"
 
Vitu vingine havihitaji kufikilia.

Jiulize,miaka kumi iliyopita mtaani kwako kulikuwa na madhehebu mangapi. Leo? Je, kila kukicha kuna Mungu mpya?
Haya,ndo yale yale. Mchungaji akihitaji kodi ya nyumba,ada za shule watoto,godolo kubwa, waumini mchangie. Muumini unaumwa pesa yote ulimalizia kwa matapeli,ohhh njoo uombewe. Gari la mchungaji halina mafuta,toeni elfu 50 apitie shell. Kudadeki zetu. Acha tupigwe tumetaka wenyewe.

Wenzetu hizo sadaka wanaweka akiba,mtoto anakuwa mamilioni yamesogea kwenye akaunti,huku tunawapa wajanja za kujengea kanisa na kununua vyombo vya mziki. Ukihoji viko wapi, mleteni akaombewe huyo ana pepo mchafu
Wa kweli wapo na wapigaji wapo pia
 
Hivi kweli,ni haki mpaka wa leo akili zetu zitawaliwe na utapeli wa watu kama sisi,wanaotaka tuiname wapite?
Kila siku wanadai muombeni,unaumwa lakini unaenda hospitali,wengine wanakata pumzi. Matatizo kibao,mara kwa waganga,kesho kanisani. Tena mara mia utapeliwe na mganga unayeona anajifanya anaongea na wakubwa.
Kila unaemuuliza Mungu ni nini? Anakujibu muumba. Kaumba lini? Jibu hamna. Niaminije? Eti we si umezaliwa ukakuta wanaamini?

Kwa hiyo,Mungu ni kufata mkumbo tu basi. Hawa hawa wanaojifanya wanamjua Mungu,wanakuja kwetu huku,ukinunuliwa bodaboda tu za 1500, unatoa ngombe eti fungu la 10 mijama inaenda kuuza na kupiga hela.
🤣🤣🤣

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
 
Mungu kutoeleweka kwa uwazi, bila utata, kwa wote, ni moja ya classic arguments against the existence of God.

Ukishaanza na "ili awe Mungu lazima asieleweke" hapo tayari umeacha mlango hata mimi kukuambia kuwa Mimi ndiye Mungu mwenyewe, ila sieleweki tu kuwa mimi ndiye Mungu mwenyewe.

Kwa sababu ili niwe Mungu, ni lazima nisieleweke uungu wangu.

Kiukweli, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote, atajulikana, atajulikana na viumbe wote, atajulikana na viumbe wote bila utata, hatahitaji kitabu, tafsiri, nuktadha, muongozo, mjadala ili aeleweke bila utata wowote ule.

Ukishaona Mungu anajadiliwa, anaelezewa, ameandikwa, anatafsiriwa, anawekewa muktadha, anahubiriwa, etc, ujue hakuna Mungu hapo, hizo ni siasa za watu tu hizo.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kutojitambulisha ajulikane bila utata ni ukatili mkubwa unaosababisha vita vya kidini, migogoro ya kimataifa, crusades za maelfu na maelfu ya miaka.

Mungu mwenye tabia hizo (ujuzi wote, uwezo wote, upendo wote) hsi mkatili hivyo.

Ama Mungu mwenye tabia hizo yupo, na watu wanamuelewa bila utata, ama watu wanamuelewa Mungu huyo kwa utata na Mungu huyo hayupo.

Watu wanamuelewa Mungu kwa utata, ndiyo maana mijadala hii haiishi hapa JF.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.
Waooo sasa umekuja pale patamu, kumbe shida yako ni kuwa hujamuelewa vizuri ,hajaonekana ,unapata contradictions za upendo na hasira zake vizuri.
Sasa hizo sifa ndo sifa za kuwa Mungu,lazima kuwepo na gape na Muumba na waumbwa ,kuto muelewa au kutoelewa kani yake ya ufanyaji kazi si dhana yakusema hayupo.
Let say kuna watu hawatambui serikari ya william luto rais wa kenya lakini ,serikari ipo kutotambua kwao haibadilishi chochote,kutojaliwa kwao,na kukatiliwa kwao ,au kutopemdwa kwao hakubadilishi chochote.
Hoja zako ni fupi mno, hoja yako ni mfu.
Twende kwenye laws ya "action and reaction ",au laws ya" charge s"hizi laws ukiziangalia vizuri zina operate utendaji kazi wa energy ambayo Mungu katupa kama zawadi wanadamu na na akatupa akili Ili tujue tunaitumiaje energy,na huu ndo uungu upo hapa.( Mungu akupi hela,wala mali zaidi ya akili na kugovern energy)
Hebu twende ( kuchanganua energy) na laws za charge na actions na reaction law.
Ukiona sehemu pana chuki jua ilitangulia upendo
-kwahiyo kama unahisi upendwi na Mungu jua kuna anaopenda na kuwajali. So facts ya kupendwa ni wrong point ya kujadili uungu na Mungu .
- Hukihisi humuelewi laws ya actions na reactions,itakwambia wapo waomuelewa, sasa kama wapo it's means Ili umuelewe lazima upige goti ujifunze kumuelewa ,kutomuelewa wewe tu hakukupi justification ya kusema siyo Mungu ,kama wapo hata wachache wanamuelewa basi yupo bcoz hujaamua kumtafuta utamuelewaje,kwamfano usipo pambana kusaka maokoto hutokaa uyapate.
.Halafu lazima positive na negative ziwe na utofauti .
Nimeeleza hapo juu ,Mungu hatokani na miili ya nyama bali anatokana na miili ya roho ,roho hujadili roho huwezi kuwa nyama ukajadili roho, Ili ujadili roho lazima kuwa katika Msingi wa kiroho ,
Utasemaje nitakuwaje kiroho, zipo njia nyingi ambazo scientifically proved
Mfano 1.Meditation na 2.astral bodies projection,etc
Toa gape change state nenda kamjadili Mungu ukiwa katika roho Ili mlingane state ,wewe kiumbe dhaifu,uliyeitwa Mpumbavu kwenye vitabu vya dini.

Na hoja yako ya mwisho, Waoo vizuri ,hakuna sifa kama usiri ,usiri ndio sifa ya Mungu, Mwenyewe lazima aweke mipaka na anaweka Ili ukitaka kujua siri zake lazima upige goti, hao wengine wanaomueleza wamepata maarifa baada ya kusujudu,usiache kusujudu KWA sababu ,yeye Hakubembelezi ana watu wakutosha hapa na nyulimwengu nyingine anazomiliki pia watu wa kwake huko haliko sasa why ahangaike na wewe,una faida gani kwake.

-Ashakuwa Mungu why umpangie namna ya ku operate yeye kaaamua kuoperate KWA namna hiyo ,mfano Magu aliamua kuwa mbabe sasa kuwa kwake mbabe akubadilishi dhana kwamba si rais ,ndo namna Mungu kaamua kuweka gape Ili heshima iwepo ,ukitaka kummanage mtu weka gape ,tumia principle ya Mungu utamanage watu wote duniani

- Wewe kujiita Mungu au kuna comment uliita mavi yako mungu, naona nuts zinaanza kulegea kichwani ni haki y'ako kujiita hivyo kikatiba maana humzuru yoyote,
But uchizi wako usioneshe public kuwa Mungu lazima uwe na sifa ya kuweza kuunda na kubomoa nishati ,kwenda tofauti na principle zote za misingi ya dunia ,kama umesoma science nikikwambia principle utaelewa mfano kuweza kucontrol mwendo na muda on sport kama alivyo Sema hesergnbergy, kuweza kucontrol nishati kwa kuunda na kubomoa ambapo principle ya energy inakataa .
Na principle nyingine sasa kama hiyo sifa huna huwezi kuwa na yupo aliyeunda principle na anayeweza kutengua ,kama zipo ziliwekwa na nani na yeye ,yeye ni nan ndo Mungu.
Uje na hoja bwana Kiranga habari zaku coat mitazamo ya sayansi isiyoweza kujikamilisha sitaki isiyo static sitaki nataka facts
 
Mpaka sasa.

1. Hakuna mtu aliyethibitisha Mungu yupo.

2. Hakuna mtu aliyetatua mikanganyiko ya kimantiki inayojitokeza katika hoja na dhana za kuwepo Mungu, kama vile "the problem of evil", kwa nini Mungu hajioneshi kwa uwazi usio na utata wowote kwa wote, freewill's incompatibility with God's perfect knowledge, etc.

3. Hakuna mtu aliyeweza kutatua mikanganyiko ya kimantiki ya kwenye vitabu vya imani vinavyojinadi kuwa ni vitakatifu na vya Mungu, kama Quran na Biblia, kwa mifano ya kuanzia tu.

Haya yote yanatokana na ukweli kwamba, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hayupo kiuhalisia. Mungu huyu ni muhusika wa hadithi za kutungwa na watu tu, nje ya hadithi hizo, Mungu huyu hayupo.

Kama unabisha, tatua masuala yaliyoorodheshwa hapo juu katika 1, 2 na 3.
Yupo kwa sababu
1.Energy ipo energy ndo Msingi wa kujua kujua Mungu yupo, kama unabisha uwepo wake basi bisha na energy maana hakuna aliyeunda.
2.Kwanini ipo katika dhana ya mtazamo binasfi ,namm nikuulize wewe kwanini unakataa Mungu hayupo,kwanini siyo fact kwanini ni dhana wa mpishano wa mafikirio binasfi na kujitengenezea swali lakini si kila mtu amejitengenezea swali kama wewe.

3.Evil ni kiumbe kilicho na uhuru kama wewe na chenyewe kinajua kutumia nishati vizuri aliyoumba Mungu mwenyezi,kwasababu wewe hujui kikaamua kutumia udhaifu wako kukutengenezea tatizo, na wewe tatizo unaliita evil problems,sasa hizo evil kama unaziamini , basi automaticatically unaamini Mungu ,bcoz evil ni tangable,sasa wewe inaonekana unajichanganya kimantic maana unaamini evil problems ambapo nikikwambia u prove unaweza ??
3.Kutatuaje wakati wewe ndo umejitungia maswali ,kama ulivyo yatunga hapa ya kutokuwepo KWA Mungu, hivyo vitabu vipo katika Msingi wa imani,
Narudia tena Mungu ni roho kimuundo Ili umuelewe lazima uwe katika muundo wa roho, sasa wewe upo katika muundo wa kimwili ,automatically haiwezekani kumwelewa ,change state .nakama imeshindikana
Basi tunachange gear imani ni alternative ya kujua misingi ya kiroho kama huwezi kuwa kwenye state ya kiroho
 
Huwezi kuelewa mambo ya kiroho ikiwa haupo open minded GOD is really ila ukiwa low minded you can't understand this power
Usiwe open minded kwa kuacha mashimo au matundu ambayo yataruhusu uongo kutumbukia kwako.

Kuwa open minded hakufanyi usifuate sheria za mantiki na sayansi katika kithibitisha vitu.

Kuwa open minded hakukulazimishi ukubali tu habari za Mungu kiurahisi bila kufuata kanuni.

Unaelewa hilo?
 
Yupo kwa sababu
1.Energy ipo energy ndo Msingi wa kujua kujua Mungu yupo, kama unabisha uwepo wake basi bisha na energy maana hakuna aliyeunda.
2.Kwanini ipo katika dhana ya mtazamo binasfi ,namm nikuulize wewe kwanini unakataa Mungu hayupo,kwanini siyo fact kwanini ni dhana wa mpishano wa mafikirio binasfi na kujitengenezea swali lakini si kila mtu amejitengenezea swali kama wewe.

3.Evil ni kiumbe kilicho na uhuru kama wewe na chenyewe kinajua kutumia nishati vizuri aliyoumba Mungu mwenyezi,kwasababu wewe hujui kikaamua kutumia udhaifu wako kukutengenezea tatizo, na wewe tatizo unaliita evil problems,sasa hizo evil kama unaziamini , basi automaticatically unaamini Mungu ,bcoz evil ni tangable,sasa wewe inaonekana unajichanganya kimantic maana unaamini evil problems ambapo nikikwambia u prove unaweza ??
3.Kutatuaje wakati wewe ndo umejitungia maswali ,kama ulivyo yatunga hapa ya kutokuwepo KWA Mungu, hivyo vitabu vipo katika Msingi wa imani,
Narudia tena Mungu ni roho kimuundo Ili umuelewe lazima uwe katika muundo wa roho, sasa wewe upo katika muundo wa kimwili ,automatically haiwezekani kumwelewa ,change state .nakama imeshindikana
Basi tunachange gear imani ni alternative ya kujua misingi ya kiroho kama huwezi kuwa kwenye state ya kiroho
1. Energy ni nini?

2. Kwa nini unasema kwa nini ni dhana ya mtazamo binafsi? Umeshawahi kutoka nje ya mtazamo binafsi ili kujua nini kipo ndani ya mtazano binafsi na nini kipo nje ya mtazamo binafsi?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wite hayupo kwa sababu anakanushwa na the problem of evil.

3. Hujathibitisha Mungu yupo, hutakiwi kusema evil ni kiumne cha Mungu. Thibitisha Mungu yupo kwanza kablabya kusema evil ni kiumne cha Mungu. Na ikiwa evil ni kiumbe cha Mungu, imekuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe evil katika ulimwengu ambao angeweza kutoumba evil?

4. Unaweza kuthibitisha roho ipo? Usizungumzie roho kabla ya kuweza kuthibitisha roho ipo.
 
Back
Top Bottom