Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Bila kujali uko sahihi au siyo sahihi, ila nimependa umejenga hoja zimenyooka
Hivi kweli,ni haki mpaka wa leo akili zetu zitawaliwe na utapeli wa watu kama sisi,wanaotaka tuiname wapite?
Kila siku wanadai muombeni,unaumwa lakini unaenda hospitali,wengine wanakata pumzi. Matatizo kibao,mara kwa waganga,kesho kanisani. Tena mara mia utapeliwe na mganga unayeona anajifanya anaongea na wakubwa.
Kila unaemuuliza Mungu ni nini? Anakujibu muumba. Kaumba lini? Jibu hamna. Niaminije? Eti we si umezaliwa ukakuta wanaamini?

Kwa hiyo,Mungu ni kufata mkumbo tu basi. Hawa hawa wanaojifanya wanamjua Mungu,wanakuja kwetu huku,ukinunuliwa bodaboda tu za 1500, unatoa ngombe eti fungu la 10 mijama inaenda kuuza na kupiga hela.
 
1.Mungu ni nini?

2.Kwa nini humkubali Mungu wa dini hizi (zipi)?

3. Kama kuna unayemkubali, unayemkubali wewe ni yupi?

4. Unayemkubali wewe ana tabia gani?

5. Kitu gani kinakufanya umkubali?
binafsi naamini MUNGU wangu mimi kaka mimi na hizo dini sjui Islamic au Christian sijui nini nishatoka huko sababu MUNGU wa hizo dini anaubaguzi kabisa.

Lakini MUNGU wangu mimi hana ubaguzi.

staki kukujibu maswali ya kuumiza kichwa saana...sababu bado najifuza hasa pia kupitia nondo zako.

Vipi kwanza ushalipa KODI ya nyumba mkuu?
 
Hii maada ni ngumu sana, na tatizo linaanzia kwa sababu ni nadharia.
 
Peponi lugha itakayo tumika ni kiarabu bisha na hii
 
Hii maada ni ngumu sana, na tatizo linaanzia kwa sababu ni nadharia.
Vitu vingine havihitaji kufikilia.

Jiulize,miaka kumi iliyopita mtaani kwako kulikuwa na madhehebu mangapi. Leo? Je, kila kukicha kuna Mungu mpya?
Haya,ndo yale yale. Mchungaji akihitaji kodi ya nyumba,ada za shule watoto,godolo kubwa, waumini mchangie. Muumini unaumwa pesa yote ulimalizia kwa matapeli,ohhh njoo uombewe. Gari la mchungaji halina mafuta,toeni elfu 50 apitie shell. Kudadeki zetu. Acha tupigwe tumetaka wenyewe.

Wenzetu hizo sadaka wanaweka akiba,mtoto anakuwa mamilioni yamesogea kwenye akaunti,huku tunawapa wajanja za kujengea kanisa na kununua vyombo vya mziki. Ukihoji viko wapi, mleteni akaombewe huyo ana pepo mchafu
 
Sasa hizi si stori tu za Wana Sayansi, wewe leta ushahidi ya kuwa Maji yanapatikana vipi kwenye nazi, na lazima swali la nani anayaweka liwepo, sababu ya uwezo wa anaye yaweka.

Wewe leta ushahidi utuambie maji yanapatikana vipi kwenye nazi. Usituletee stori za Wanasayansi.
 
Mabikira 72 Mito ya pombe, hizi ni nadharia nzuri sana
Hivi, hujawahi sikia wanaojiita wachungaji wakisema kwamba kila kilichopo duniani huku na huko ni hivyo hivyo? Sasa unajiuliza huko kwa Sir God(bwana Mungu),baamedi wapo,madangulo fulu kujiachia,lodge zenye wale wadudu wanaowatesa wafaransa! Kama huko hakuna tofauti na duniani huku,wanaotaka kwenda watafata nini?
Mara Mungu yupo popote. Waliyopo jera wane huko huko. Kama hama makosa kashikiliwa kwa nini sasa?

Walihopo mochwari,huko huko. Kama kafa,ana msaada gani sasa!

Khe, badala ya mabikra hao 72, bora nipate msukule mi ntamalizana nae kimtindo. Si yale yale
 
Kuamini unaruhusiwa kuamini unavyotaka, hata ukiamini uongo ni haki yako ya kikatiba na kiutu.

Lakini kwenye kutafuta ukweli hayo maswali yanahusika.

Kodi ya nyumba mimi silipi, nalipwa.

"I got cribs in the suburbs, the hood and the city" - AZ
 
Hii maada ni ngumu sana, na tatizo linaanzia kwa sababu ni nadharia.
Ni ngumu kama unataka kulazimisha Mungu ambaye hayupo awepo.

Vinginevyo unaweza kuthibitisha kimantiki kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hayupo, kama vile unavyoweza kuthibitisha 10 si square root ya 2 katika base 10 math.
 
Blender mbona unacheka sasa?
 
Suhendra Mungu akiwanunulia feni watu wa Dar bila kuzama mifukoni mwao rudi hapa. Hawezi,nae kama sisi tu.
 
Peponi lugha itakayo tumika ni kiarabu bisha na hii
Sipo hapa kubishana, bali nipo hapa kubainisha haki na ukweli.

Hakuna ushahidi wa kweli kuonyesha hilo. Hadithi inayotumika kuelezea hili. Wanazuoni wetu wa Kiislamu wameidhohofisha. Mfano Imamu al-Albaaniy na wengine walio mtangulia.
 
Suhendra Mungu akiwanunulia feni watu wa Dar bila kuzama mifukoni mwao rudi hapa. Hawezi,nae kama sisi tu.
Hivi mungu anunue feni wakati kuna watu wana kufa njaa. Halafu hapa duniani sio mahala pa starehe lifahamu hilo kwanza
 
Kwanza INA bidi ufahamu kwamba mungu ametakasika na kila sifa ya mapungufu. Haja wahi kukosea kwa lolote lile

Hapa duniani tupo katika mtihani wa majaribio yule ambae atafaulu atapelekwa peponi ambae atafeli atapelekwa Motoni
Allah ametupa akili na maarifa tofauti na wanyama ukifanya dhambi nafsi yako lazima ikusute kwa masaasi uliyo Fanya hiyo ni dalili yakuwa binadamu tuna utashina uelewa

Shetani wala sio msaidizi wa mungu tambua kwanza hilo

Utofauti wa imani unachangiwa na utofauti wa uwelewa kati ya mtu mmoja na mwingine

Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hekima ya Allah ili kuepusha mkanganyiko wa dini ya kiislam
Hebu fikiria wee mwenywe ange kuwa anajuwa kusoma na kuandika si mngesema Qur'an ametunga Muhammad hiyo ni hekma ya Allah na ndo mana Qur'an watu wameshindwa kuibadirisha kwa sababu ni maneno ya mungu direct.
 
Kama mungu angekuwepo basi Hata huu Uzi usingekuwepo kabisa
Nonsense
Hayo ni mawazo yako lakini haina maana kila mtu aishie hapo kufikiria kama ulivyo ishia wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…