Hapana,
Lugha yetu haija define mambo vizuri, nakutaka unielezee una maana gani unapotumia neno akili? Umeshindwa.
Umeshindwa hata kuuliza swali!
Suppose nikikwambia sina akili, au nina akili, hilo lina prove vipi Mungu yupo au hayupo?
Jibu lolote nitakalokupa, hali prove Mungu yupo au hayupo.
Nikikwambia nina akili, ukaniambia thibitisha una aklli. Nikakwambia siwezi. Kutoweza kwangu kuthibitisha kuwa nina akili hakuthibitishi Mungu yupo.
Ukitaka kufanya kushindwa kwangu kuthibitisha kuwa nina akili kuwa sawa na Mungu kuwepo ila watu kushindwa kumthibitisha tu, utakuwa unafanya logical fallacy ya logical non sequitur.
Na mimi naweza kukwambia, una akili? Ukasema ndiyo. Nikakwambia thibitisha una akili. Ukasema siwezi, ila ninazo. Na mimi nikakwambia ahaa, basi kwa kuwa wewe una akili na huwezi kuthibitisha kuwa una akili, basi na mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kama ambavyo wewe huwezi kuthibitisha una akili, ndivyo hivyo hivyo huwezi kuthibitisha kuwa mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ika wewe huwezi kuthibitisha hilo tu, kama ambavyo wewe una akiki, ila huwezi kuthibitisha hilo tu.
Logical non sequitur.
Wewe kushindwa kuthibitisha kuwa una akili hakuthibitishi kwamba mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Nikisema mimi ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inabidi nithibitishe hilo.
Ukisema Mungu yupo, thibitisha hilo. Usitake kufanya mimi kushindwa kuthibitisha nina akili ndiyo uthibitisho kwamba Mungu yupo, ila hatuwezi kuthibitisha yupo.
Mimi nikishindwa kuthibitisha nina akili, hilo halithibitishi Mungu yupo, litathibitisha tu kwamba mimi siwezi kuthibitisha nina akili.
Umeelewa kuwa swali lako, katika kuthibitisha Mungu yupo au hayupo, ni irrelevant?
Nikisema nina akili, nikashindwa kuthibitisha akili ninayo, hilo hali prove Mungu yupo.
Nikisema nina akili, nikaweza kuthibitisha akili ninayo, hilo halithibitishi Mungu yupo.
Nikisema sina akili, nikashindwa kuthibitisha akili sinayo, hilo hakithibitishi uwepo wa Mungu.
Nikisema sina akili, nikaweza kuthibitisha akili sinayo, hilo halithibitishi uwepo wa Mungu.
Swali ni irrelevant. Kwa sababu jibu lolote halitusogezi popote katikankujua zaidi kama Mungu yupo au hayupo.
Maswali kama haya ya kuokoteza kwenye video clips za comedy za Wa Nigeria yanaweza kuonekana magumu na ya muhimu kwa watu wajingawajinga wasiojua kutumia mantiki katika kuwaza.
Watu wanaoangalia kila sentensi kimantiki, wanaona logical non sequitur fallacu katika huu mchezo wa kitoto wa Ki Nigeria kuwakamata atheists.
Zaidi ya yote, madai ya kusema Mungu hayupo hayatokani tu na ukweli kwamba watu hawawezi kuthibitisha Mungu yupo.
Ni kweli, inawezekana kitu kikawepo halafu watu wakashindwa tu kukithibitisha kuwa kipo. Hivyo, ingekuwa madai ya kwamba Mungu hayupo yanatokana tu na watu kushindwa kuthibitisha Mungu yupo, madai hayo ya kusema Mungu hayupo yangekuwa dhaifu. Tumeishi miaka mingi bila ya kujua formulaes za kemikalo za madawa ya antibiotics kwa mfano, ila sisi kutojua formulaes za kemikali hizo hakukufanya kemikali hizo zisiwepo.
So, kusema tu Mungu hayupo kwa sababu watu hawawezi kuthibitisha yupo ni weak argument.
Ni sawa na kusema babu wa babu yako hajawahi kuishi, kwa sababu wewe leo huwezi kuthibitisha babu wa babu yako aliishi. Pengine huna record tu, lakini huyo babu wa babu yako aliishi.
Tunapinga uwepo wa Mungu kwa sababu hamuwezi kuthibitisha Mungu yupo na pia dhana ya kuwepo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote iko contadicted na ulimwengu huu tunaouona unaoruhusu mabaya, the problem of evil shows God and this universe are mutually exclusive, and because this universe exists, Gid does not.
I am not sure you can get that through your head.