Uwezekano mkubwa sana Shambulio la Marekani dhidi ya IRAN ni alfajiri ya ya Jumapili kesho kutwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,274
Reaction score
9,326
Wadau, taarifa hii ni kwa mujibu wa uchambuzi wa vyanzo mbalimbali vya uhakika duniani na taarifa za ndani, hivyo uwezekano mkubwa ni alfajiri ya kuamkia jumapili tarehe 22.2.2026 kwa saa za Marekani. Shambulio hilo malengo ni kuuangusha utawala wa Kiislamu wa AYATOLLAH KHAMENEI. Kibali kimetolewa cha ratiba ya kijeshi dhidi ya IRAN na Rais atatoa tamko ndani ya masaa 24 kuanzia muda huu. Tayari ameridhia ratiba ya kijeshi na anasubiriwa atoe tamko rasmi yaani AMRI kwa jeshi kuanza shambulio
 
Hawawezi kuanza mashambulizi jua likiwa limetoka,hata kwa Saddam walianza usiku
 
Sasa ulimwengu unazidi kuchangamka wacha sisi tukae na kusikiliza maumivu ya hao wakubwa wakitandikana huko maana mafuta yakiguswa kwaajili ya hivi vita sisi pakukimbilia sijui ni wapi. Hii itakuwa vita mbaya sana sio ya kuombea kabisa maana huyo Irani sio wa mchezo mchezo nae aende kupigwa tu na asilete majibu tena kwa washirika wote wa USA kwa nguvu ambayo haikutegemewa.
 
USA ataenda kuabika
Vibaya mno dunia haitoamini kwa watakacho kishuhudia
safari muajemi kachafukwa marekan kama anajiamini yeye ndio JAMBAZI la dunia kwa ujiita super power
USA ataenda kuabika

ajarib tu kushambulia iran huo ndo utakuwa mwazo wa kufutwa kwa taifa la kigaid na la kishetani srael kwenye uso wa dunia na ndio mwanzo raia wa Palestine kupata nchi yao na uhuru kutoka kwa mashetan ya Israel.
Pia gaid na mtekaji MAREKANI asahau kuhusu hizo military base zake hapo middle east na hivyo vi meri vyake vitapotelea baharini😃
USA ataenda kuabika
 
Israel imekaa kimya kuepuka yaliyomkuta ile vita ya siku 12...

Lakini kama kweli US atashambulia, basi nyuma yake yupo Israel ikifuatiwa na nchi za Ulaya Magharibi...

Iran ikifahamu Israel inahusika kwa ushahidi, wataanza kutuma vimondo kuelekea Israel..

Middle East itawaka...
 
SI nimeona trump anawapa siku 10-15? Nafkir jumapili itakuwa bado siku hazijaisha
 
Utapata pressure bure, shauri yako. 😲😲
 
Mikwara tu hiyo. Hakuna vita hapo
 
Hii taarifa sio kweli. Trump ameipa Iran takriban siku 10 hadi 15 kufanya uamuzi wa busara utakaoweza kuiokoa Iran na watawala wake.

Vinginevyo safari hii ndio utakuwa mwisho wa utawala wa kiimla wa Ayatollah na genge lake.

Safari hii Iran ikianza kupigwa wahanga wa mapema kabisa watakuwa ni Ayatollah mwenyewe na wapambe wake akina raisi Masoud Pezeshkian na wengineo.

Wakishauliwa hao wanajeshi wa Iran watakuwa hawana tena wa kuwapigania hivyo ni lazima kutatokea mapinduzi na ndio utakuwa mwisho wa utawala wa kiimla wa Ayatollah na genge lake. Tusubiri tuone.
 
Sasa wakishauangusha utawala wa Khamenei kuna plan 'B' ya kuendesha nchi au ndio kama yale ya Iraq na Libya kusambaratika baada ya Saddam na Gadaffi kuanguka?..
 
Hii taarifa sio kweli. Trump ameipa Iran takriban siku 10 hadi 15 kufanya uamuzi wa busara utakaoweza kuiokoa Iran na watawala wake.
Trump haaminiki, Iran imekaa tayari muda wowote, mbinu ya Trump ni mashambulizi ya kushtukiza, ile vita ya siku 12, US iliwalaghai Iran kwamba wapo kwenye mazungumzo badala yake wakashambuliwa ghafla. Hivyo ndio maana unaona Iran wamekuwa wakali na hawataki tena kukubaliana na lolote toka kwa Trump.

Kwa ufupi Iran imejipanga kivita.. Binafsi sikuwahi shuhudia Iran ikijibu kwa ukaidi kiasi hiki.. Iran hawamuamini tena Trump..
 
Sasa wakishauangusha utawala wa Khamenei kuna plan 'B' ya kuendesha nchi au ndio kama yale ya Iraq na Libya kusambaratika baada ya Saddam na Gadaffi kuanguka?..
Iran ina wasomi wengi sana kwenye nchi za magharibi na wako tayari kushikilia usukani kuiongoza nchi yao.

Wakija kwanza kabisa watafuta serikali feki ya kidini na serikali itakuwa ni secular na mtaona ndani ya miaka 10 uchumi wa Iran utakuwa kwenye 7 bora duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…