Uwezekano mkubwa sana Shambulio la Marekani dhidi ya IRAN ni alfajiri ya ya Jumapili kesho kutwa

Hii wala haihitaji ushahidi, Tel Aviv itawaka!

USA anaenda kuishambulia Iran kwa vigezo vya kuilinda Israel.

Tel Aviv lazima itiwe kiberiti, hii inaitwa kama mbwai na iwe mbwai.
 
Kwa nini sasa hivi uchumi wa Iran haujawa kwenye hiyo 7 bora duniani ?
 
Hao 'exiles' wasio na mizizi ndani ya nchi sio hakikisho la kudumu.

Hao waliopo serikalini wakiondolewa wote wataingia msituni kuanzisha uasi kama jeshi la Iraq lilivyofanya baada ya kuvunjwa.

Iraq ilikabidhiwa kwa kina Chalabi ambao hawakua na mizizi na kilichotokea sote tunakijua.
 
Ikiwa hii vita US ataanzisha yeye, sioni Iran akijipapatua sana otherwise USA awe anampiga kwa kumuonea huruma Iran.

Wakuu, US ni habari nyingine ile kabisa.
 
Ikiwa hii vita US ataanzisha yeye, sioni Iran akijipapatua sana otherwise USA awe anampiga kwa kumuonea huruma Iran.

Wakuu, US ni habari nyingine ile kabisa.
Wale hawapigani kwa kisa kuchokozwa ila kuto ongea na Wamerakani ipo damuni kwao. Na wanaweza wasijibu hata mapigo ila mtastukia israeli inatafuta sehem ya hifadhi.
 
Kuna kikundi kipo yemen kina eneo kubwa lakini kili sababisha mazito sana kwa ndugu zetu.

Wangeanza na kile kwanza kujipima nguvu kabla hawajafata eneo kubwa zaidi.
 
Vita vya Arabs na Muslims huwa vina mbwembwe ila ukilala ukiamka wamedundwa wanaanza kulia huku wakihamasisha maandamano duniani. wakipigana wao kwa wao kimya. wakichokoza wakapigwa nongwa
Muda si mrefu tutasikia pray for Iran
 
USA ataenda kuabika
Tatizo wayahudi walisha.muingiza kwenye sanduku la Epstein sa hana ujanja lazima apigane vita kwa niaba ya Israeli, lakini motokeo yatakuwa machungu kwa USA na Israel.

Iran wako mbali sana kwenye Science na Technology USA ataadhirika labda akatumie Nuclear tu ndio atawashinda Iran.
 
Ikiwa hii vita US ataanzisha yeye, sioni Iran akijipapatua sana otherwise USA awe anampiga kwa kumuonea huruma Iran.

Wakuu, US ni habari nyingine ile kabisa.
Kumbuka hypersonic haina air defense ya kuidhibiti..

US anakuwa na kiherehere na hii vita kwa sababu anajificha nyuma ya washirika wake... Iran ikishambulia Diego Garcia utakuwa ni mgogoro tena na UK, maana kuishambulia Diego Garcia ni kuishambulia UK, maana Diego Garcia ipo chini ya UK...


Kambi za US zilizopo middle East , Bahrain, Kuwait, Qatar, UAE, Oman , Jordan, Iraq, Syria, Saud Arabia ambapo Iran imesema italenga inaweza pelekea mgogoro na nchi hizo....

US anaongea kila muda kuishambulia Iran akifahamu fika yupo nyuma ya washirika..

Iran wanasema wanaweza kusogeza meli karibu na US wakalenga mji wowote wa US, hasa Washington..
 
Iran wanasema wanaweza kusogeza meli karibu na US wakalenga mji wowote wa US, hasa Washington..
Iran haina uwezo wa kufanya hii kitu katika dunia ya uhalisia labda kama tunakubali kujipa matumaini hewa, ingekuwa Iran dhidi ya Tanzania hapo sawa lakini sio Iran dhidi ya U.S

U.S ina uwezo wa kumfuata Iran kwake iwe kwa anga,maji au ardhini lakini kinyume chake Iran haiwezi labda kama unataka kufananisha U.S Army na IDF naweza kukuelewa angalau lakini kwa U.S yale ni maji marefu sana Japan alijaribu huo mchezo kwa suprise attack natambua unajua kilichompata.

Iran ina jeshi zuri dhidi ya jamii yake ya mashariki ya kati lakini kwa U.S wenye ubavu wa kumfuata kwake ni Russia na China na wenyewe itategemeana na situation atakayo kuwa nayo U.S katika vita
 
Endapo US ikifanya mashambulizi kutoka kwenye meli zake za kivita, unadhani Iran inashindwa kulenga hizo meli?
 
Iran ni mbwa anebweka huku hana meno!..
. Hela yake imeanguka kabisa!

Wanachi wengi wako against utawala.....

USA na Israel watajipigia tu maana alishalemazwa toka ile vita ya siku 12..
.
Kwa jinsi USA alivyokusanya vifaa hapo meddle East ni ngumu sana kuvirudisha bure.
 
Vitalengwa, tupo hapa...
Pesa imeanguka sababu ya vikwazo... hata hivyo wanajitahidi sana, Israel haiwezi pewa vikwazo kama hivyo waka survive miaka mitatu.

Si kweli kwamba wananchi wengi wapo against utawala... Linapokuja suala la vita.. utawaona wanatoka na mabango yao ya 'death to America' maelfu kwa mamilioni, tupo hapa...

Itakuwa umefuatilia haya maandamano ya sasa... fuatilia maandamano ya 2009(green movement), futilia maandamano ya 2017-18 kuhusu uchumi, maandamano ya 2019/20 kuhusu bei ya mafuta kupanda..

2022/23 maandamano ya yule mwanamke aliyeuawa na Polisi.. hapo sijazungumzia maandamano kabla ya mwaka 2000.. miaka ya 90s huko pia kulikuwa na maandamano...

Lakini baadae unawaona hao hao wanasema 'death to America'....

Hivyo usijidanganye mkuu, vita ikianza wananchi wapo na serikali yao.

12 days war haikuilemalaza Iran, Iran ilikuwa kwenye sintofahamu kwa masaa kadhaa kabla hawajajipanga na kuji restore fully kisha kujibu mashambulizi hadi Israel ikaomba ceasefire, Israel ndiye aliumia pakubwa ndio maana hivi sasa humsikii akiwa mbele kujitangaza kuishambulia Iran.. hypersonic haina kinga.

Tujipe muda...
 

View: https://youtube.com/shorts/zCGXb4zV3zo?si=LuDQ6DKQELplYQMf
Anasema Steve Witkoff US special envoy to the Middle East tulizani Iran atakubali masharti yetu, lakini hawajakubali hata moja, Iran inaonekana kama inataka vita na wao ndiyo wanatupa masharti sasa.

US naona wanaogopa kuingia vita wewe baki na story zako eti USA watashambulia Iran Jumapili 😄
 
Ikiwa hii vita US ataanzisha yeye, sioni Iran akijipapatua sana otherwise USA awe anampiga kwa kumuonea huruma Iran.

Wakuu, US ni habari nyingine ile kabisa.
Kipigo cha fullscale tokea USA kitamfuta Khamenei chap ila kama wakimtumia Netanyau basi Israel itachakaa😂
 
Speculations!! Iran sio Iraq
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…