Uwezekano mkubwa sana Shambulio la Marekani dhidi ya IRAN ni alfajiri ya ya Jumapili kesho kutwa

Mbona Venezuela rais katekwa kabisa na nchi haijapinduliwa? Huwezi ng'oa utawala kwa kuua kiongozi si anateuliwa Ayatollah mwingine tu na maisha yanaendelea!!

Njia pekee ni kuleta wanajeshi wa ardhini kitu ambacho USA hawezi maana atapata losses kubwa kwa vita ya miaka na miaka kama Afghanistan
 
Vita vya Arabs na Muslims huwa vina mbwembwe ila ukilala ukiamka wamedundwa wanaanza kulia huku wakihamasisha maandamano duniani. wakipigana wao kwa wao kimya. wakichokoza wakapigwa nongwa
Iran wamelia lini? Si Israel ndio iliomba ceasefire baada ya kuishiwa interceptors za David sling!!
 
Uchumi wa Iran mbona upo vizuri, otherwise wasingeweza sustain tokea vikwazo viwekwe. Trust me bila vikwazo Iran ingekua uchumi mkubwa zaidi MENA.
 
Jamaa unaongea kama vile wewe ni miongoni mwa top officials wa jeshi la jamhuri ya kiislam ya Iran😂😂
 
Jamaa unaongea kama vile wewe ni miongoni mwa top officials wa jeshi la jamhuri ya kiislam ya Iran😂😂
Anamuona Iran kama Russia/China. Iran anga lake lilitekwa lote na adui akawa anapiga atakavyo.
 
Hicho unachikitamani kitokee marekani anakiogopa kuliko unavyofikiria hawezi kithubutu kirusha hata jiwe
 
Jumapili mbona imefika.. tusubiri hadi lini tena..

Wasichokijua Iran hivi sasa yupo kwenye mode nyingine kabisa, hataki mchezo...

Sijawahi kushuhudia Iran ikijibu kwa jeuri kiasi hiki... US alidhani mikwara ya kusogeza hayo mameli yatawafanya Iran kuogopa... hivi sasa US ndiye anajivuta na kutafakari mara mbili mbili...
 
Ayatollah Ali Khomen kisha sema US kweli ni Super Power lakini kuna wako ma Super power walichapwa kibao na ule u Super power wao ukaisha.

Hapo Iran anajambo anataka kulifanya kisha chimba makaburi 5000 ya wanajeshi wa US kule Iran sababu hizo carriers zitakuwa ni history. Intelligence ya Israel wamedai Iran ana uwezo wa kuzizamisha Carriers na zitasambaratishwa na Hypersonic za Iran.

Israel ambaye ana mlazimisha US kushambulia Iran kisha sema hatuwezi kuzuia Missiles za Iran na hata kama hatutaingia vita Iran atatushambulia tu.

Hao Israel vichaa kweli wao wanamlaxzmisha US aingie vitani na Iran wanataka Iran asiwashambulie 😄
 
Uchumi wa Iran mbona upo vizuri, otherwise wasingeweza sustain tokea vikwazo viwekwe. Trust me bila vikwazo Iran ingekua uchumi mkubwa zaidi MENA.
Kama ni mzuri yale maandamano yamekuwa ya nini na ndio makubwa tokea huu utawala wa kiimla uingie madarakani 1979.
 
Akiletwa rais mwingine naye analiwa kichwa, mwendo unakuwa ni huohuo.
 
Iran walifahamu kitambo sana kuwa ipo siku marekani wataanzisha vita dhidi yao ili kuipa Israeli pawa mashariki ya kati. Irani walijiandaa na vita hii siku nyingi sana kwani walijua itatokea tu na wamejiandaa sana na wapo kamili gado. Mpila umebaki kwa marekani kulianzisha kama wao ni kweli super power
 
Kama ni mzuri yale maandamano yamekuwa ya nini na ndio makubwa tokea huu utawala wa kiimla uingie madarakani 1979.
Huwezi pendwa na kila mtu, hata USA kuna maandamano makubwa sana dhidi ya ICE ila sijaona popote mkisema USA ni failed state!!

Imagine epstein files zingetaja Iran kusafirisha vitoto kutoka USA!! Si wangeshapingwa nuclear kabisa. Sema sababu US ndio waliokosea basi kesi inafia hewani
 
Ukweli unabaki palepale kwamba wananchi wa Iran wamechoka na utawala wa kiimla wa Ayatollah na wanataka serikali mpya isiyo ya kidini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…