Ulichopaswa kufanya ni kuongea tu na kumwambia kila kitu, asingeweza kukujibu kwakuwa tayari alishaachana na nafsi lakini amini usiamini ungeyapata majibu kwa namna ya ajabu kabisa
Naomba kujua kwa nn uliacha hiyo kazi jeeh kuongea na maini ni somo la darasani au ni upeo tu uliopewa na mwenyezi muumba...
Duuuu dagii kweli upo kwenye nyagi....!!!!
Nduguyangu mshana nyagi ilikwisha jana hiyo,naswali mpenzi mamayangu alifariki takribani miaka mi 2 sasa na alikuwa ananipenda sana ila tangu afariki hajawahi kunitokea japo kwenye ndoto je nifanyeje anitokee?au kuna baya nimelifanya?
wakikosi shetani hajawahi kusema hivyo kwakuwa shetani naye hana uwezo huo wa kuongea na wanadamuHadithi tu hizi ,hakuna lolote.Mtu akifa hawez tena kuwasiliana na walio hai.Kinachoendelea baada ya kifo ni ujanja wa shetani tu kuwadanganya wanadamu kuwa marehemu wao wapo sehemu fulani wanaishi.
Kwani kuna baadhi ya watu huwainaaminika kuwa wanaongea na mizimu kwenye baadhi ya koo na familia fulani hapa nchini,utaona mtu anasema nimezungunza na marehemu babu yenu jana.
Mkuu mshana jr umetisha kwenye uzi huu, ila endelea kutiririka ujue tunakusoma kwa makini sana tuweze kufahamu haya ambayo wengi hatuyajui. Inaelekea katika mambo haya uelewa wako ni mkubwa sana kama ilivyo katika mambo mbali mbali ambayo huchangia hapa jamvini.
Mshana habari mkuu...sante kwa somo nzuri..japo nadhani ni pana na gumu ila umejaribu kuliweka kwwnye wepesi...
Mkuu mshana niambie kuhusu roho..baada ya kifo huenda wapo..kuna sehemu nilisoma wanasema zinakuwa ni wondering soul...je mwisho wake ni nini...zinakufa
Kwenye kusoma soma kunasehem mtu alisema kuna watu hawaji ila zile soul zinatafuta mwili mwingine na kuishi...kuna ukweli gan???..
Kuna pengine wanasema soul zote duniani they are connected..kwamba this life unaweza kuwa mwanadamu next life unakuwa mti..next unakuwa labda mbwa...n so on n so on..kuna ukweli gani hapo!!!!.
Samahani mkuu mshana jr kama ntakuwa nje ya mada..napenda kujifunza na kufaham yaliyomo kwa ulimwengu.
Roho na nafsi huwa havifi bali hubaki vikizunguka huko na huko na ndio maana kwasababu haijakamilika kuwa binadamu kamili basi huitwa mzimu/mizimu
Mizimu si majini wala vinyamkera bali ni roho za watu waliokuwa na maisha yao kama sisi
Zamani tukienda kutambika tulikuwa tunaimba hivi
Taaambaa tiase nkoba, tiombe Mungu mzimu wa Saita kagone
Yaani... tughani tutupe tunguli,tumuombe Mungu MZIMU wa Saita kalale
Haya ni mambo ya kimila.mizimu ilikuwepo na iliabudiwa
Sabrina ni kweli roho huko ziliko ni ready made yani kinachofanyika ni kutafutiwa maumbo tu ya kuingia na utambulisho/nafsi kwamba huyu ni mnyama, mdudu, mwanadamu, nk na hakuna roho inayoangamia hata siku moja bali kinachoangamia ni umbo, utambusho/ID hubaki kama kumbukumbu kwamba 'a'likuwepo mshana jr 'a'kawa hivi au vile 'a'kafariki maiti/mwili 'wake' 'u'kapotea/'u'kazikwa/'u'kaungua na Mungu 'a'ilaze roho yake mahali pema peponi huo ndio utambulisho unaobaki
Kwahiyo mimi ni muunganiko wa vitu vitatu mwili nafsi na roho, nje ya hapo kuna mwili wangu, roho yangu na nafsi yangu