Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Mshana Jr ni kweli nimefanya hivyo makusudi,lakini hiyo story ni kama imechukua sura nzima,kwa muda huu nikisema kesho nitakosea.Baadaye nitaweka vifungu vilivyo vifupi,ila nitakuwa kimya watu wachangie je aliyeamshwa na yule mwanamke ni Samweli wa ukweli mtumishi wa Mungu au janja ya shetani?Hapo tunamwitaji Roho mtakatifu atufundishe kwani yeye pia ni mwalimu.
Aaamen barikiwa zaidi [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Dunia imekuwa kama kijiji kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha mwanadamu wa kugundua hata ambavyo vilifikirika kwamba haviwezekani

Elimu na ufahamu kuhusu mwili wa mwanadamu kuanzia kuumbwa tumboni kuzaliwa hadi kufa umetafitiwa na kunyumbulishwa kwa mapana yake na wengi wamepata elimu ya juu kabisa PhD kwenye hili eneo, lakini wakashishindwa kitu kimoja tuu!!! Uwezo wa kumuita marehemu na kuongea naye

Zamani kabla ya dini za kigeni hazijaja Africa tulikuwa kwa kiasi fulani tuna uwezo wa kuwaita marehemu kwa njia ya matambiko na kuwaomba hili au lile, lakini ikumbukwe kwamba hawakuja live bali dalili na ishara kadha zilionyesha uwepo wao na kukubali au kukataa ombi husika

Tumekuwa tunaondokewa na wapendwa wetu na watu tunaowahitaji mno katika maisha yetu, tumekuwa na vipindi vigumu kabisa ambapo tunawahamu na kuwahitaji japo wajitokeze kwa dakika chache tu lakini haikuwezekana kabisa

Mfu ni mfu na hatuna uwezo wowote iwe wa kimwili au wa kiroho kuweza kumuita na kuongea naye lolote, hii ni kwakuwa roho inapotengana na mwili hakuna tena huyo MTU bali kunatokea vitu vitatu visivyoweza kuungana tena na kutengeneza kitu kimoja. vitu hivyo ni roho mwili na nafsi, vitatu hivi ndio vinatengeneza MTU nje ya hapo kuna 'mwili wake', 'roho yake' au 'nafsi yake'

Watu wamejaribu kutoa shuhuda nyingi za kutokewa na marehemu, hili linawezekana kwasababu baada ya kifo kuna roho huwa zinawayawaya duniani, zipo tu na hizi ndizo ambazo hugeuka mizimu mizuri au mibaya

Wakati mmoja tu marehemu anaweza kusikia sauti ya mwanadamu na kuitii ni pale tu anapoandaliwa kwa safari yake ya mwisho kaburini, hasa kwenye ishu ya kumsafirisha au kumvalisha nguo

Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza

Tuna wajuaji wengi Siku hizi wanaojifanya wametokewa na marehemu fulani na kumpa maagizo Fulani hizi kwa asilimia 90 ni story tu kwakuwa hatujakuwa na uwezo wa kuwaita au wao kututokea tu na uchafu wote huu tulionao
Hiyo elimu inajulikana kitaalamu kama Negromancy au Necromancy.Kibongo bongo inajulikana kama Ritifaa .Binafsi ninamjua Mganga mmoja tu hapa Tz mwenye elimu hii.Hata Shariff Ibrahim, anaetajwa kama bingwa wa visomo Afrika hana elimu hii ya kuongea moja kwa moja na wafu.Al marhum Juma Njemba wa Ujiji Kigoma ambae yeye alikuwa amespecialize kwenye kuua watu kichawi alifariki akiwa hajahitimu darsa la namna ya kuwasiliana na wafu..Hata Yule mzee wa kidendeule aliyekuwa akiishi porini karibu na mbuga za Selous hakuwa na elimu hii hadi mauti yalipo mkuta..Kwa utafiti wangu ili mganga aweze kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wafu moja kwa moja lazima kwanza awe mkonikoni.Kuwa mkoni koni pekee hakukupi uwezo wa kuzungumza na wafu moja kwa moja ila ni daraja kueleke uwezo wa kuzungumza na wafu.Sasa basi katika ulimwengu wa wakonikoni hakuna kitu kinacho itwa " kifo" katika mantiki inayo julikana na wengine.Kwao kifo ni uwepo wa uhai wa roho ya mauti .Kwao kuzungumza na wafu maana yake ni kuzungumza na roho iipayo mauti uhai
 
Unauhakika yule aliyeamshwa na mwanamke mwenye pepo la utambuzi alikuwa ni Samweli mtumishi wa Mungu?Hapa sitakuwa wazi ili tujifunze kitu na wengine wachangie kutokana na level za ufahamu wao.Hiyo habari ipo 1Samwel28:3-25, ukiwa unasoma ,soma kwa kutafakari zaidi ya mara moja 1Samweli28:6-7
Uhakika upi zaidi ya Maandiko ambayo yanatuambia aliamshwa Samweli? Hayo mengine ni maoni mawazo na uchambambuzi tu ambayo yanaruhusiwa lakini maandiko yanasema aliamshwa Samweli na akasema yatayotokea kwa Sauli.
 
Ama kweli wahenga walinena "Elimu haina mwisho"
Hiyo elimu inajulikana kitaalamu kama Negromancy au Necromancy.Kibongo bongo inajulikana kama Ritifaa .Binafsi ninamjua Mganga mmoja tu hapa Tz mwenye elimu hii.Hata Shariff Ibrahim, anaetajwa kama bingwa wa visomo Afrika hana elimu hii ya kuongea moja kwa moja na watu.Al marhum Juma Njemba wa Ujiji Kigoma ambae yeye alikuwa amespecialize kwenye kuua watu kichawi alifariki akiwa hajahitimu darsa la namna ya kuwasiliana na wafu..Hata Yule mzee wa kidendeule aliyekuwa akiishi porini karibu na mbuga za Selous hakuwa na elimu hii hadi mauti yalipo mkuta..Kwa utafiti wangu ili mganga aweze kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wafu moja kwa moja lazima kwanza awe mkonikoni.Kuwa mkoni koni pekee hakukupi uwezo wa kuzungumza na wafu moja kwa moja ila ni daraja kueleke uwezo wa kuzungumza na wafu.Sasa basi katika ulimwengu wa wakonikoni hakuna kitu kinacho itwa " kifo" katika mantiki inayo julikana na wengine.Kwao kifo ni uwepo wa uhai wa roho ya mauti .Kwao kuzungumza na wafu maana yake ni kuzungumza na roho iipayo mauti uhai
Yaani huu uzi naurudia mwanzo mwisho.
Kuna mengi ya kujifunza
[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
 
Uhakika upi zaidi ya Maandiko ambayo yanatuambia aliamshwa Samweli? Hayo mengine ni maoni mawazo na uchambambuzi tu ambayo yanaruhusiwa lakini maandiko yanasema aliamshwa Samweli na akasema yatayotokea kwa Sauli.
Mkuu uko sahihi unaweza sema ni mawazo ila yanasupport ya maandiko,nitakuja baadaye ngoja na wengine watoe mchango wao,ila jiulize Sauli aliwau wenye pepo la utambuzi unajua ni kwanini?Hata alipoenda kwa yule mama,yule mama alisema hicho kitu ya kwamba mbona unahatarisha maisha yangu?Jiulize wale ambao mwanzo aliwau kwa sababu ambazo nilitegemea utazijua,leo baada ya kuona Mungu hamjibu kwa njia ya manabii na njia zingine zilizoandikwa,Sauli huyo huyo anaenda kuwaomba msaada.Nilipo post nilibold neno pepo la utambuzi ili nikupe wepezi lakini umefail kutumia muda kuchunguza,mkuu usiwe na haraka taratibu utanielewa nitarudi.
Alichokifanya Sauli ndicho wanakifanya watu wengi baada ya kuona Mungu anachelewa kuwajibu kwa mtazamo wao,huenda kwa waganga wa kienyeji ambao in a nutshell ni shetani yuleyule ila akitumia watu.Si unaona hapa kuna mtu amesema kuna mganga anamjua anauwezo wa kuamusha wafu,nitakuja huko kote just be cool,nikusihi tu si lazima unjibu muda huu,take your time.
 
Iko hivi sikuwa anakataa live bali wakati wa kumvisha kama ni koti shati au hata suruali kuna kiungo kimoja hukakamaa kwa mfano kama ni mkono haunyanyuki au haukunjiki, kama ni mguu unajipinda au unakuwa mzito kunyanyua
Hivi vitu vinafanyika kwa namna ya ajabu na ya kipekee kabisa

Vilevile kuna kukosea vifungo au zipu kujichanganya! Yani mnaanza kufunga kifungo cha kwanza vizuri kabisa mkifika mwisho aidha vimepishana au mmeruka matundu, tulishawahi kukosea vifungo Mara SABA
Ni mpaka nilipotumia elimu niliyojifunza kuongea na marehemu kwa upole na kwa kumbembeleza ndio mambo yakawa sawa, na pia ndani ya chumba husika kama yupo mtu alikuwa na ugomvi na marehemu hakuna kitakachokwenda sawa hapo mpaka yule mtu atoke
na kuna wengine kama marehemu mkewe alichangia kifo chake dhakari husimama mpaka mkewe ajichomeke tena ndio ilale naye azikwe salama.
 
Japo mwili hutawanyika na kuwa kitu kisicho kamili lakini maneno yoyote ya marehemu hubebwa na roho na nafsi yake
Hizi habari za wosia si kitu cha kupuuza hata maramoja waliopuuza walipata habari yake mifano halisi ipo mingi kama marehemu alisema sitaki hivi na mkafanya tofauti baada ya yeye kufa maafa hutokea mara zote
Hivi nini tofaut kati ya nafsi Na roho
 
Njoo newala, nitakupeleka ng'ambo ya mto ruvuma katika kijiji cha namatili yupo bibi mmoja anauwezo mkubwa wa kuongea na wafu! na kupitia yeye anaweza kukwambia marehemu ambae mlimzika miaka hata kama ni 20 au 40 anasema nini na anahitaji nini, huyu bibi kwa kufanya huduma hiyo haitaji pesa yoyote zaidi ya kukwambia katoe sadaka ktk nyumba za ibada, au kwa yatima na wajane.
 
Sijakuelewa kabisa
One more QN
So baada ya kufa kuna maisha mengine even katika mwili au kiumbe kingine
Ili uweze kuwa wewe I mean kwa utambulisho wa majina yako unahitaji vitu viwili ambavyo ni mwili na roho... Muunganiko wa hivi vitu viwili ndio hutengeneza nafsi, nje ya muunganiko huu hakuna nafsi
Baada ya kifo (mchakato unaotokana na mwili kujitenga na roho) mwili huharibika na kuoza... Roho hubaki hai
 
Njoo newala, nitakupeleka ng'ambo ya mto ruvuma katika kijiji cha namatili yupo bibi mmoja anauwezo mkubwa wa kuongea na wafu! na kupitia yeye anaweza kukwambia marehemu ambae mlimzika miaka hata kama ni 20 au 40 anasema nini na anahitaji nini, huyu bibi kwa kufanya huduma hiyo haitaji pesa yoyote zaidi ya kukwambia katoe sadaka ktk nyumba za ibada, au kwa yatima na wajane.
Kwa hakika nitakuja nikiwa tayari nitakuambia most likely this July
 
Mimi nakubaliana na wewe katika hili.Ni kweli kabisa unayosema maana nimewahi kusikia hivi kutoka kwa bibi yangu akinihadithia mikasa aliyoiona kwa macho yake.
Pia marehemu babu yangu amewahi kufanya hivi pale alipoingia adui yake katika chumba alichokua anaoshewa.
Kwahili ni dhahiri marehemu hua wanasikia.
Marehemu waliokufa kwa ugonjwa gani hao ambao huwa wanasikia?

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Dunia hii wapumbavu "hatuishi"
 
Back
Top Bottom