Aqua
JF-Expert Member
- Jul 23, 2012
- 1,657
- 1,231
Hivyo vyote ni vitu visivyoonekana na huwezi kuvitenganisha nafsi ilipo ndipo na roho ilipo ila nafsi inahusika na kufanya maamuzi(faculty of thinking, reasoning, and applying knowledge) na roho(spiritual nature of humankind) ni kama mwili katika ulimwengu wa roho.Hivi nini tofaut kati ya nafsi Na roho
Nafsi na roho zikiwa ndani ya mtu(kwa maana ya huu mwili wa nyama) mtu huyo anakuwa hai,au niseme roho ni pumzi ya uhai ambayo Mungu aliweka ndani ya mwandamu.Mtu akifa nafsi na roho zinakuwa zimetoka katika huu mwili.Niishie hapo,kwa sisi tunaoamini kuna Mungu tunnamini siku ya unyakuo kwa wale watakao kutwa hai,miili yao itabadilishwa lakini nafsi na roho zinakuwa zilezile.Siku moja nikiwa kweny sunday school,kidogo nimulize mchungaji kwamba biblia inasema baada ya kifo ni hukumu,je kama mwili wa mtu aliyekufa tuko nao anayehukumiwa ni nani?Sometimes mtu inamanisha nafsi na roho ukisoma biblia hasa mwanzo kuna maeneo watu huchanganywa kwa ufahamu wao na kuona kama kuna makosa.So mtu anaweza kuwa body,mind and soul na kuna muda katika ulimwengu wa roho mtu ni nafsi na roho,wachawi wakimloga mtu au anapokuwa amefungwa gerezani,yeye katika physical world anaendelea na maisha yake lakini nafsi inapofungwa hata mtu anaweza kuwa anafanya maamuzi ya ajabu yakauathiri mwili wake.
Kama hujaokoka mpokee Yesu leo,huko kuna sunday school utafundishwa utaelewa,yamkini kuna sehemu nimekosea katika kuelezea kwangu ruksa kuulizwa.