UWT watoa tamko kuhusu Pauline Gekul, yasema haitamvumilia kiongozi yeyote mwanamke anayekiuka Haki za Binadamu

UWT watoa tamko kuhusu Pauline Gekul, yasema haitamvumilia kiongozi yeyote mwanamke anayekiuka Haki za Binadamu

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetangaza kusikitishwa taarifa za tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati Mjini, Mhe Pauline Gekul kuhusu kumfanyia ukatili kijana Hashimu Ally huko Babati Mjini, Mkoani Manyara.

Taarifa ya UWT kwa umma imesema Umoja huo hautavumilia kiongozi yeyote mwanamke atakaethibitika kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kubainisha kuwa UWT inazunguka nchini nzima kupinga na kukemea ukatili wa kijinsia na kuporomoka kwa maadili.

Hivyo UWT inasisitiza umuhimu wa viongozi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viapo vyao, maadili ya uongozi na utawala bora. UWT inapinga vikali kitendo hiki na endapo tuhuma hizi za Mhe Pauline Gekul zitathibitika hatua stahiki zichukuliwe na adhabu kali itolewe dhidi yake.

UWT inampongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM kwa maamuzi ya kutengua uteuzi wa Mhe Pauline Gekul kama Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha, UWT tunaviomba vyombo vya dola kukamilisha uchunguzi kwa haraka ili kuleta imani kwa wananchi na tunatoa pole kwa familia iliyoathirika.

Soma:
- Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

WhatsApp Image 2023-11-27 at 20.26.54.jpg
 
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetangaza kusikitishwa taarifa za tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati Mjini, Mhe Pauline Gekul kuhusu kumfanyia ukatili kijana Hashimu Ally huko Babati Mjini, Mkoani Manyara.
Tamko la kisiasa hili
 
Tunataka haki zetu wanaume tunaonewa sana na wanawake Tanzania tunaomba ulimwengu na jamii itutetee wanaume
 
Picha linaweza kuanzia kushoto likaishia kulia au likaanzia kulia likaishia kushoto.[emoji3447][emoji3447]
JamiiForums954137435.jpg
 
Back
Top Bottom