UWT watoa tamko kuhusu Pauline Gekul, yasema haitamvumilia kiongozi yeyote mwanamke anayekiuka Haki za Binadamu

UWT watoa tamko kuhusu Pauline Gekul, yasema haitamvumilia kiongozi yeyote mwanamke anayekiuka Haki za Binadamu

Kwa hiyo anataka kusema Mh. Rais amemsimamisha kimakosa huyo naibu Waziri bila kufanya uchunguzi? Mbona kama sijaelewa?
 
Hawa panya buku wanaflo na beat tu hawana lolote, mwenyekt wao angekaa kimya nao wangekaa kimyo hvo hvo.

WANAFIKI WAKUBWA
 
UWT HAITAMVUMILIA KIONGOZI YEYOTE MWANAMKE ANAYEKIUKA HAKI ZA BINADAMU

27 Novemba, 2023

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mary Pius Chatanda amesema UWT imepokea kwa masikitiko tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul kuhusu kumfanyia ukatili kijana Hashim Ally.

"Sisi UWT tunazunguka nchi nzima kupinga ukatili wa kijinsia na kuporomoka kwa maadili hivyo tunapinga vikali kitendo hiki na endapo tuhuma hizi za Mhe. Pauline Gekul zitathibitika hatua stahiki zichukuliwe na adhabu kali itolewe dhidi yake" - Amesema Mhe. Chatanda.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutengua Uteuzi wa Mhe. Pauline Gekul kama Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

#UWTImara
#UWTJeshiLaMamaSamia
#TunapingaUkatiliWaKijinsia

View attachment 2827264View attachment 2827265
Mbona hamjamvua uanachama wa UWT?
 
Bangusilo kapatikana.
Wanampika supu mwanzo mwisho....
 
Kwa hiyo anataka kusema Mh. Rais amemsimamisha kimakosa huyo naibu Waziri bila kufanya uchunguzi? Mbona kama sijaelewa?

Waache warukeruke tu, hadi Rais amtengue, anazo taarifa kuwa tuhuma ni za kweli.

Paulina Gakul baadae tena akajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe kwa kuachia video akimhoji huyo kijana huku akionekana yupo uchi. Hii inaendelea kuthibitisha ukweli wa tuhuma kwamba alimdhalilisha huyo kijana. Zaidi pia huyo katili Gekul amejiongezea makosa kwa kuvujisha hiyo video.

CCM kama haitomvua Gakul uanachama itabidi ituambie inaunga mkono vijana wa kiume kuingiziwa chupa kwenye njia ya haja kubwa.

Gekul kwa ukatili na udhalilishaji alioufanya hakupaswa kuwa mbunge hadi muda huu.
 
Bila kumvua Pauline uanachama wa UWT mnaropoka bure tu, embu fanyeni haraka!
 
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetangaza kusikitishwa taarifa za tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati Mjini, Mhe Pauline Gekul kuhusu kumfanyia ukatili kijana Hashimu Ally huko Babati Mjini, Mkoani Manyara.

Taarifa ya UWT kwa umma imesema Umoja huo hautavumilia kiongozi yeyote mwanamke atakaethibitika kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kubainisha kuwa UWT inazunguka nchini nzima kupinga na kukemea ukatili wa kijinsia na kuporomoka kwa maadili.

Hivyo UWT inasisitiza umuhimu wa viongozi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viapo vyao, maadili ya uongozi na utawala bora. UWT inapinga vikali kitendo hiki na endapo tuhuma hizi za Mhe Pauline Gekul zitathibitika hatua stahiki zichukuliwe na adhabu kali itolewe dhidi yake.

UWT inampongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM kwa maamuzi ya kutengua uteuzi wa Mhe Pauline Gekul kama Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha, UWT tunaviomba vyombo vya dola kukamilisha uchunguzi kwa haraka ili kuleta imani kwa wananchi na tunatoa pole kwa familia iliyoathirika.

Soma:
- Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

View attachment 2827309
Porojo kama porojo nyingine tu!!
 
Back
Top Bottom