Uzalendo ni nini?

Uzalendo ni nini?

Tatizo la nchi hii hususani kwenye masuala ya kitaifa kila mtu anataka aonekane yeye ndiye mshika bendera leo hii CHADEMA wakianzisha hoja na ikawa nzuri sana na yenye mashiko CCM hawawezi kuiunga mkono kwa sababu watakosa popularity kwa wananchi vivyo hivyo kwa CHADEMA hawataunga mkono hoja pia ninanchokiona hata kwenye issue ya mchanga ndicho kinachotokea hapa ndo kila mtu anataka aonekane ndiye mzalendo wa kweli
 
Unamsikia mtu anasema uzalendo utazidi ikiwa tutasimama na wahisani kuwashawishi kuzuia fedha yao hadi masharti ya utu yatimie?

Hivi Mugabe anaongoza kwa wingi wa wazalendo au wizi wa kura? Akiwa na uchaguzi halali unafikiri uzalendo wa Wazimba utamsaidia kubaki kwake kwa sababu ya kuzuiwa kwa fedha ya mkoloni?
Uganda jee?

Ikiwa uchaguzi wa haki utafanyika huyu mzalendo wao atashinda? Kule Zambia jee? Tunahalalisha hadithi za kupanga panga. Hivi kati ya uonevu uliovuka mpaka na kilio cha kuzuiwa misaada kipi hasa kitachozuia uzalendo.

Yaani tunapanga panga hadithi kama tuko katika vita ya baridi katika karne hii. Ukoloni ulishamaliza hizi sentiments za kuwatusi wazungu tukiwa ndani lakini wapenzi wakubwa tukiwa nje ndio ninaouona upuuzi mkubwa zaidi.

Madikteta dunia hawana wingi wa wazalendo kwa sababu ya kuzuiwa misaada. Uzalendo wanaojaribu kutuonyesha ni uzalendo feki unaosukumwa tu na khofu ya bunduki, mizinga na roketi hakukosa kibatari na kauli zake. Firauni hakuangamizwa kwa sababu ya maendeleo bali kukosa utu, kuonea wanyonge na kujifanya Mungu mtu.

Hakuna aliepewa laana za Mungu kwa kupinga maendeleo yasio na utu bali walioangamia wengi ni wanafiki, wadhulumaji na waliosimama katika mabaya kwa wanyonge. Yesu hakusimama kuzuia maendeleo yasio na utu? Kwa nini tulidai uhuru wakati mzungu alijenga na kuhakikisha maendeleo yanakuwa japo kibaguzi na bila ya utu?

Unajuwa hata Iddi Amini nae akituaminisha anawazalendo kwa sababu za kupanga kama hizi?

Botha wa Afrika Kusini nae halkadhalika akiamini uzalendo kuzidi kila akibanwa.

Uzalendo unao "encouraged" kupindwa kwa utu, kudidimizwa kwa haki na kuzimwa kwa demokrasia ni sawa na uchifu wa kuwauza wananchi katika utumwa kwa sababu za kuwa ni shida katika tawala zao.

Na iweje tuwapigie makofi wazungu wanaouona ubaya unaotendeka lakini wakaendelea kuzisaidia kwa hali na mali tawala katili duniani?

Si ndipo tunaposimama na kuwalaumu kuwa ndio sababu ya kudumu kwa ukatili na uongozi wa ghilba barani Afrika na ukoloni mambo leo.

Hivi tunadhani misaada hii inapotolewa katika mazingira yasiojali utu, demokrasia na haki kweli ni misaada ya maslahi nasi au watoaji? Makatili wakubwa duniani walidumu kwa sababu gani kama si misaada iliokuza ubeberu, ubabe na tawala za khofu?

Wazalendo walijengwa Ujarumani katika misingi hii ya taifa langu kwanza halikosei na matokeo yake ubaguzi ukawa ni maisha ya kawaida na mauaji ya kibaguzi yakipewa daraja ya utukufu.

Uzalendo usiohoji utu, haki, usawa na heshima ya kuishi mwananchi kwa sheria na uhuru wake ni uhuni tu usio na chembe ya insaf.

Maendeleo gani yenye manufaa na wananchi ikiwa haki, uhuru na heshima ya kuishi kwa kulindwa na sheria na utu ukiwa haupo?

Yaani ukiwachie kizazi chako urithi wa kukubali aonewe, anyimwe haki na kuishi kwa muono wa mzizi mkuu ilimradi tu kuna maendeleo?
 
Naomba wana Jamii wenzangu tujadili kwa kirefu maana ya neno "UZALENDO" na ni nini maana ya kuwa MZALENDO halisi hapa Tanzania nyakati hizi.

Hivi kukubali kila kitu inachosema serikali ndio uzalendo?

Kumuunga mkono raisi kwa kila kitu anachosema na kufanya ndio uzalendo?

Kua na mawazo mbadala na serikali, wewe sio mzalendo?
 
Uzalendo ni hali ya kuithamini nchi yako na kuwa tayari kutenda kwa mapenzi ya nchi yako

Sent from my TV
 
Kuna wakati kuipenda Serikali iliyopo madarakani sio Uzalendo na kuna wakati kuichukia Serikali iliyopo madarakani ni Uzalendo.
Kuichukia au kuipenda nchi ni tofauti kabisa na kuichukia au kuipenda Serikali.
 
Uzalendo hapa kwetu ni sawa dodoki ukilitupa kwenye maji machafu,litabeba takataka zote huo ndio uzalendo sasa
 
Kumekuwa na watu wakiwaita wenzao kuwa si wazalendo. Mabishano ni makali.
TATIZO: lazima kwanza tukubaliane definition ya Uzalendo. Tukisha kubaliana definition ya uzalendo, then tutaweza kirahisi kumjua nani si mzalendo. Huu ni ukumbi wa GTs, lazima tujenge premise za kupata jibu la kisayansi.

Mfano: Is a whale a fish? Kabla ya kujibu swali hilo lazima tukubaliane characteristics (sifa???) za fish. Tukikubaliana characteristics (sifa???) hizo tu, basi ni rahisi kusema kama a whale is a fish or not!
 
Kuingia kwenye station ya redio Saa tano usiku na Rais asiseme chochote...huo ni uzalendo
bongo mufilisi
 
Maana halisi ya uzalendo ni kulipenda na kuwa tayari kulitetea taifa lako ata kupoteza maisha.

MAANA YA kiCCM
Kumsifia kiongozi wao kwa mema na mabaya ata kama ni hasara kwa taifa,(mf kukanatwa kwa ndege wakati chanzo ni yeye) … Kuwazuia wanafunzi waluopewa mimba kurudi shule, ripot feki za makinikia etv
Au zidumu fikra za n/kiti nfiyo uzalebdi wa o
 
Uzalendo ni kupenda na kuithamini mila,desturi,utamaduni,asili,taifa, lugha.-zetu
 
Mimi huu wimbo unaoimbwa na viongozi tuwe wazalendo wakati wao wenyewe wamekosa uzalendo unanikera. Tutakuwaje wazalendo wakati hata basic needs na basic social services ni za kusuasua wakati wahubiri wa uzalendo hizo needs na services wako na access nazo kwa urahisi?
 
Back
Top Bottom