Pascal ni mnafiki.Mkuu huyu jamaa akiamua kujitoa ufahamu kuhusu yanayojiri nchini anakuwa mtu wa ajabu sana kwa pumba anazoandika humu.
@Moderator tafadhalini hii ni JF si FB au mitandao mingine ambayo matusi ni ruksa. Humu lazima staha iwepo si matusi namna hii. Hawa madogo hawajielewi kabisa, unadai demokrasia lakini huwezi kumvumilia mwenzako akitoa hoja tofauti. Ndio maana wengine tumeamua kuwanyoosha ili upinzani na mashabiki wake wabadilike na tujifunze namna ya kujenga hoja huku tukilinda maslahi ya taifa na kuwa na staha kwa viongozi wetu.
Tatizo ni kwamba watanzania hawaoni haja ya kumtetea Magu anapotukanwa na vyombo vya nje.For sure kuna tatizo kwenye mfumo wetu wa elimu. Mbona watu ni wajinga kiasi hiki?
Hakuna anaesema rais yuko sahihi, hata mleta mada ameelezea hayo yote, Someni Muelewe lengo la mleta mada,
Hawa jamaa wanapolazimisha wote tuwaze wanayoyawaza wao...una hoja nzuri sana.
..ila una tatizo dogo ktk "mtazamo" wako.
..kwa mtiririko wa hoja zako inaelekea unaamini viongozi wako serekalini tu, huko kwingine hakuna viongozi.
..sasa napenda nikukumbushe kwamba hata ktk vyama vya upinzani kuna viongozi.
..na viongozi wa upinzani wanadhalilishwa, wanatukanwa, wanabugudhiwa, wanaumizwa, na wapo waliouwawa.
..ili tuwe na "udhu" wa kuwatetea viongozi wetu wa kitaifa wanaosemwa huko nje, ni vema tukaanza kwa kuwatetea viongozi wa upinzani kutokana na madhila wanayoyapata hapa nchini.
Wale wasukuma ambao walimoiga kura jpm hadi hawakubomolewa nyumba zao na wanaofaidika na huu utawala ndo wakaongoze kampeni za kumtetea baba yao. Ila sisi hapana.Huyo anaemtete anakatawale mifugo yake na watoto wake nyumbani kwake
Wale wasukuma ambao walimoiga kura jpm hadi hawakubomolewa nyumba zao na wanaofaidika na huu utawala ndo wakaongoze kampeni za kumtetea baba yao. Ila sisi hapana.
Uzalendo kwa nchi tunao ila sio uzalendo wa kutetea upumbavu.
Kaandika au anahamasisha? Uzalendo anaounadi umevurugwa na nani? Hizi dhana za kujificha kwenye kuilinda amani na uzalendo ni chaka la kufanyia maovu na ufisadi! Simameni katika haki na acheni kumega nchi vipande kwa ukabila!Nikisoma comments za watu wengi humu najiona mtu mwenyewe akili sana! Watanzania ni nani alituloga? Mnaombeza Paskali Hivi mmesoma kwa umakini alichoandika kweli?
Ona na wewe unatutukana kisa sio wazalendo! Wewe uzalendo wako ni upi na umelifanyia nini taifa lako? Unatukana watu kisha unawadai uzalendo? Ni Tanzania tu inakopatikana hii kitu ya kuwaita wananchi malofa, vilaza, wapumbavu na vinyago kisha uwadai uzalendo wao kama fidia! Wajirekebishe na wajivue huo uungumtu kwanza ili tumwelewe mleta hoja!Watu humu vilaza sana,yaani kuna watu unaweza ukawaona wa maana kumbe hata kuelewa vizuri andiko kama hiki wameshindwa wamebaki wanatoa oovu tu..
Ona na wewe unatutukana kisa sio wazalendo! Wewe uzalendo wako ni upi na umelifanyia nini taifa lako? Unatukana watu kisha unawadai uzalendo? Ni Tanzania tu inakopatikana hii kitu ya kuwaita wananchi malofa, vilaza, wapumbavu na vinyago kisha uwadai uzalendo wao kama fidia! Wajirekebishe na wajivue huo uungumtu kwanza ili tumwelewe mleta hoja!Watu humu vilaza sana,yaani kuna watu unaweza ukawaona wa maana kumbe hata kuelewa vizuri andiko kama hiki wameshindwa wamebaki wanatoa oovu tu..
kwani hujui huyu naye mtoa uzi anatafuta uongozi ndani ya tawala hii ndo anajikosha na anajiondoa kwenye 26/4 ili asionekane mbya hahaaaaaaSijaona popote rais alipotukanwa, anaambiwa ukweli tu.
umeongea point my dia yaani kweli watu wako unawaongoza wako kwenye majanga ya kupoteza mali na hata ndugu zao walikufa wewe kama kiongozi unaongea hovyo badala ya kuwafariji unadhani hao watu watasemaje watkakuwajeMkuu Pascal Mayalla sio kwamba hatuna uzalendo tatizo ni yeye mwenyewe ndiye anajidhalilisha, unaendaje mahali ambapo watu wamepatwa na tetemeko la ardhi wamefiwa, wana uchungu wa kupoteza nyumba na mali zao halafu unakurupuka na kuwambia wafanye kazi Serikali haitatoa msaada wowote, asiyefanya kazi na asile na asipokula afe, haya ni maneno ya hovyo sana