Ila Bandile nae fala,
Hivi hadi anafungwa sijamsikia hata scene moja akitamka maneno "nimesingiziwa" ama "ninabambikiziwa hii kesi",
Hajatumia hata nguvu kidogo kwenye wazo la kuwa anatumika kubeba kesi ya mtu mwengine
Halafu muandishi wa series katupiga hapa na kitu kizito, Bandile kashawahi kwenda jela, hivi kweli mtu aliye wahi kwenda jela si anajua kitu kinaitwa 'alibi' yani alibi ni kuwa kama ukituhumiwa jambo ukawa na ushahidi kuwa ulikuwa na watu fulani mahala fulani kuwa muda wa tukio ulikuwa nao basi unaachiwa, yeye Bandile Kakubali kiurahisi mno kesi ya mauaji, wakati kina dhlomo wangeweza kufika huko kwao kuhoji watu na kuthibitisha kuwa muda nkosinathi alipopotea yeye hakuwapo kwamashu, yani hata mtu hata aliye iba sufuria akifika mahakamani lazima atahaha kutaka kujinasua na suala lake, ila sio Bandile.
Kingine, Bandile hakutaka kesi yake mama ake ajue hivi hakukuwa na ndugu wengine wa kuwasiliana nao pengine ndugu wengine wangekuwa na mchango mkubwa kudadisi mambo na asingefungwa