Uzalo Special Thread

nosipho anaongea na mama ake mambo tofautia tofauti,wakiwa kitchen huku nosipho akiwa amevalia
nguo za mazoezi ghafla ataiona Pete ya mama ake aliyovishwa na zakes,atamuuliza mama ake kwa nn amekubali halafu mbona mapema Sana.

mangcobo atamjibu nosipho na kumwambia mapema unaona wewe je unataka Mimi nizeeke nikiwa peke yangu(single) vile vile ni maamuzi yangu nishaamua hivo.

nosipho baada ya kutoridhishwa na maneno ya mama ake ,Anaamua kusepa kuelekea jogging ambapo huko atakutana na mondli.

kisha watasalimiana na baada ya hapo mondli ataanza kumlaumu nosipho kwa nini alidanganya kwamba alikuwa ametishiwa kisu na wauni,kisha kumwambia uongo si mzuri kwa Sababu unaweza kukutia matatizoni siku moja ,na inawezekana ukapata kweli matatizo ukaja kituoni na tusikuudumie ipasavyo tukijua tu unadanganya.

halafu vilevile sijui nilishindwa vipi kujua Kama wewe na familia yako kwamba mna tabia ambazo si njema.

so nosipho baada ya kutajiwa tu familia ,anashikwa na hasira na kumwambia mondli sikiliza wewe usizani mimi ninavokufatafata kwamba nina shida Sana na wewe halafu sitaki tena nikusikie ukiitaja familia yangu,kisha nosipho anasepa zake.



zweli(mastermind) akiwa nyumbani anazungumza na Dada ake(smangele) kuhusu mipango yake kama vile kwenda kutafuta maisha Johannesburg,so smangele anamuuliza kwa hy umesema unaenda kutafuta maisha ,je unaweza kuniambia kipi ambacho utakuwa unafanya kwa ajili ya kukuingizia kipato,
zweli atajibu chochote kile na kumalizia na statement I will hustle.


zakes akiwa ofisini(panelbeaters) anatembelewa na mtoaji oda wa Italian cars aitwaye samuel ngidi
yote yamewezakana kwa kujulishwa na SBU
samuel ngidi atamwambia zakes ukitaka kufanya biashara na Mimi lazima ukubaliane na conditions zangu MF moja ya condition ni lazima mxolisi awepo na uwe unashirikiana nae
so kishingo upande zakes atakubali ,kisha wanapeana mikono na samuel ngidi anasepa.


mxolisi anaenda kuonana na zweli(mastermind) kwa ajili ya kumshawishi afanye nae tena kazi,lakini zweli atamwambia kuanzia sasa sifanyi kazi za bure,na kwa kila kazi tutakayofanya tunagawana faida. 50 kwa 50,mxolisi atamwambia hamna shida kisha anasepa.

smangele anaonekana akiwa nyumbani kwa pastor ayanda akicheki stocks za vitu jikoni lakini kabla ajamaliza anatokea ayanda akiwa na mifuko mbalimbali ya vitu toka sokoni ,kisha watasaliamana na kumuuliza smangele ameingiaje ndani,smangele atamjibu na kumwambia nilisaidiwa na mxolisi,so smangele atavaa apron,vile vile ayanda
lkn smangele atamuuliza unafanyeje ayanda,yeye atajibu nataka nipike
so smangele atamwambia kazi ya kuwapikia wajumbe wa bodi na wachungaji ni ya kwangu kwa hy acha.

mxolisi anaenda nyumbani kwao kwa zamani kuonana na mama ake mlezi(mangcobo) kwa ajili ya kumjulisha kuhusu kutaka kufanya kazi na zweli ,so mangcobo hatoafiki kabisa na kumwambia mxolisi hatuwezi kufanya kazi na wasaliti halafu vile vile kazi anayofanya zweli hata zakes anaweza kuifanya na tena Ana uzoefu nayo.
baada ya kujibiwa hivo mxolisi ataona Pete kwenye mkono wa mangcobo na kumuuliza kulikoni
kisha mangcobo atamjibu Kama unavyoona nataka kufungua ndoa
lkn mxolisi atamwambia VP kuhusu baba ,mangcobo atamjibu nimsubiri baba ako hadi lini kwanza zakes ni MTU mzuri kwangu.

smangele anaenda kuonana na ayanda kanisani kwa ajili ya kuzungumzia mawili matatu kuhusu mstakabali wa mahusiano yao lkn kabla hata mazungumzo hayajakolea zinatokea pisi Kali tatu mbele yao na kumwita pastor ayanda,smangele baada ya kuona hivo anachukia na kuondoka.


mangcobo kamwita mamlambo nyumbani kwake ,kwa ajili ya kumjulisha kwamba anataka kufunga ndoa na zakes
mamlambo atamwambia aiwezekani kufungisha ndoa kanisani kwetu ambayo inamuhusu mtu ambaye ni shetani Kama zakes.
 
Yan had raha ulivoelezea saivi hata nisipoona najua ntakutana na hii kitu yenyewe kwa urefu kabisa keep it up
 
Uko vzr aisee had raha
 

Thank you for sharing [emoji3590]
 
Ni kama nimeona live,ni simulizi tamu

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
Mwenye link tafadhali tamthilia ni Kali sana tatizo muda wa kufatilia,,Kama kuna mwenye link nitakayo kuwa nafatilia online tafadhali anipe
 
Huyu aunty yake na xulu ana majibu makavu kinomaa aseeh duh 😁😁

Mxo kashayavuruga tayari huku.
 
Napenda kuwa na mashangazi kama hawa yaani shangazi wa xulu Kamtimua zakes kama mbwa
 
Napenda kuwa na mashangazi kama hawa yaani shangazi wa xulu Kamtimua zakes kama mbwa
Unapoweka ubuyu hàpa hakikisha umeweka Kila kitu bila kubakisha.Wengine hatujaangalia Uzalo tuna mwezi Sasa!
 
Baada ya Mxolisi na Na Mastermind kuiba ile Gari BMW i8 aka Beamer walionekana Kwenye Cctv camera na mwenye Gari akampelekea Dhlomo ili awakamate

Mxolisi na Mastermind wakakamatwa na Dhlomo kwa mahojiano na akawaambia saiv hamchomoki maana nina evidence


Mastermind na Mxolisi wakiwa wanasubiri kuhojiwa wakakubaliana hamna kusema ukweli mpk tuone ushahidi tunakataa kila kitu.


Basi Dhlomo na Mondli walivotaka kuwaonesha ile cctv footage wakawa wanaona chenga tu yaani Cd imeibiwa na haipo Kwenye laptop wakawa wanashangaa tu

Kumbd Zakhele Mkhize aka Zakes alimpa rushwa askari mmoja aibe ile cd yenye evidence

Mastermind na Mxolisi wakaachiwa huru

Dhlomo akaenda kwa Manzuza kumwambia kuhusu mxolisi kuwa anaendelea na wizi wa magari

Mxolisi anatoka kituoni anarudi nyumbani anamkuta Dhlomo anaongea na Manzuza akajua ashachoma akapitiliza chumbani


Manzuza akataka maelezo kuhusu kilichotokea Mxolisi akasema wamesingiziwa na hamna ushahidi wowote Manzuza akamwambia Mxolisi achague kati ya Xulu au Mdletshe

Shangazi yake Ghabashe kaenda nyumbani kwa Xulu anamkuta Zakes na Pajamas na kwakua hawajuani Zakes anataka kumfukuza shangazi mpk aliposema yeye ni shangazi yake Xulu Zakes anashikwa na aibu anatulia


Shangazi yake Ghabashe anapinga mahusiano ya Mangcobo na Zakes na hataki ndoa ifungwe anataka Zakes atoke nyumbani kwa Xulu


Mastermind ashapata ukweli kwamba Smangele anatoka na Ayanda,anamuonya asimuumize dada yake la sivyo watazinguana


Manzuza anamualika Smangele nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha usiku na kumpa go ahead Kwenye mahusiano yake na Ayanda


Ayanda anamtambulisha rasmi Smangele kanisani kwamba ni mtu wake.Mangcobo anasikitika kwa sababu Ayanda ni mwanae na hakumwambia chochote


Zakes ameenda kanisani ili Manzuza amuone ni mtu mwema kwa Mxolisi na anamuahidi kuwa wanafanya biashara hali pale Panel beaters


Nosipho anamwambia Mondli kuwa anampenda waanze mahusiano ila Mondli anasema twende taratibu tusiharakishe mambo tuwe marafiki kwanza

Mondli anaomba ushauri kwa Dhlomo kuhusu mahusiano anasita kuwa na nosipho, Dhlomo anamwambia chukua goma acha ufala


Nosipho amechoka kumfukuzia Mondli akamfata kituoni akamchana kuwa kila mtu na hamsini zake amechoka kujitongozesha akasepa ikawa aibu kwa Mondli kila askari kituoni anamcheka



Nosipho karudi enzi zake za kuvaa mawigi na vimini Mondli anajilaumu anamfata tena nosipho ila anakataliwa


Mastermind anawakuta Zakes na Sbu ofisini wanapanga njama walivomuona wakamfukuza

Baadae walivoondoka akaenda kuweka kidude cha kurekodi sauti Kwenye ofisi ya Zakes

Mxolisi amepata order ya magari matano akamwambia Zakes ghafla Manzuza anawakuta


Zakes anajitetea kwamba Mxolisi anamsaidia kazi

Manzuza anamwambia Mxolisi Aache kujihusisha na kina Xulu,ila Mxolisi anatishia kuondoka na kwenda Johannesburg akaendelee na maisha yake kwani hawezi kuishi bila kipato

Manzuza anamruhusu tena Mxolisi kuendelea na kina Xulu


Shangazi yake Ghabashe amemuita mjomba wake xulu nyumbani kwa Mangcobo ili waendeleze kupinga ndoa ya Mangcobo na zakes


Mangcobo anatishia kuwafukuza nyumbani kwake wakiendelea kumpangia maisha


Zakes baada ya kuona mambo yanataka kuhribika anampa offer mjomba wake Xulu awaache waendelee na ndoa na atampa Rand 20000

Mengine nimesahau..........
 
Mkuu hongera sana kutujuza Kwa kirefu👍👌
Kazi nzuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…