Tabia ya GC imebadilika baada ya kutoka Jela,amekuwa mwizi na tapeli.Alimuibia Zweli,mastermind wallet na kuenda kuweka heshima bar.Alinywesha watu bia na kufanya vibe la kufa mtu na kuwamwagia watu pesa.Alifumwa bar na DK na habari kufikishwa kwa Master mind,alifukuzwa usiku ,utetezi wa Smangele haukufua dafu.
Thobile ndiye mmiliki mpya wa Saloon iliyokuwa ya GC.Baada ya kufukuzwa nyumbani kwa kina Zweli/Sma, GC alikwenda kujihifadhi maeneo ya Kanisa.Asubuhi wakati anajisafisha washroom walikutana na Mamlambo.GC alidanganya yupo maeneo ya choo cha kanisa akifanya maombi.Mamlambo alimwambia amalizane na maombi yake, yeye,Mamlambo yupo nje anamsubiri ana maongezi naye.Mamlambo alitaka kujua kilichompeleka lockup ni kisa gani, GC akaishia kumdanganya.Mwisho wa siku Mamlambo aliishia kutapeliwa na GC.
Terror yupo mjini akijitaja kama ni binamu wa Mumsy(mtoto wa mchungaji)toka Swaziland ,huku akimtafuta.Anakutana na Smangele na anaelekezwa nyumbani kwa mchungaji, sehemu ambayo anaishi Mumsy.Anafika mahali hapo na kumkuta Manzunza(mke wa mchungaji),Baada ya kuulizia kama hapo anaishi binamu yake,Terror anakaribishwa na Manzunza.Mumsy bila kujua anatoka chumbani na kumkuta Terror sitting room,anajikuta ana dondosha chombo alichoshika na kuvunjika.Terror anamchangamkia Mumsy akimwita binamu,Manzunza bila kujua mchezo unaoendelea, anakwenda kuchukua vifaa vya usafi kuondoa chombo kilichovunjika.Huku nyuma Terror anamchimba biti Mumsy kwamba amekuja kuchukua roho yake kumpeleka kuzimu,huku anamwambia ataua familia moja baada ya mwingine mbele yake.Anaulizi wapi pesa zake zilipo.Mummsy anajaribu kuBuy time akimwambia aje kesho,atakuta mzigo.Terror anagoma akidai anataka kumchoma kwa polisi.Manzunza anaporudi anakuwa haelewi chochote kinachoendelea kati ya wawili Hao.Baadae mchungaji anajumuika nao akitoka kwenye mizunguko yake bila na yeye kuelewa kinachojiri.Nyumbani kwa Zweli,Sma anamwambia Zweli amekutana na binamu wa Mumsy, Zweli anashtuka kwamba Mumsy yupo hatarini.
Mangcoba akiwa katika kilele cha furaha ya kuchumbiwa na Nkuzi,anatumiwa ujumbe wa ajabu ambayo haueleweki.Hamjui mtumaji,hii inapelekea kupoteza furaha kabisa,Nkuzi anajaribu kumuuliza lakini anamficha.Baadae anamwita Mxo ajaribu kumshauri kuhusu hilo jambo lakini anakuwa hajapata jibu na kumjua mtumaji wa hizo jumbe.