Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Kuna Uzi wa kula tunda kimasihara haunivutii hata kidogo Kuna Uzi za mashoga, Kuna ule wa kutupia picha na baadhi ya news MMU Zina trend ila hata sijawahi ona Cha maana.
N.B mwisho wa siku Kila mtu na interest zake
 
Uzi wa kula tunda kimasihara.

Uzi wa jamiiforum usiku wa manane.

Uzi wa kupeana likes sijui na comments.

Uzi wa kutupia picha yeyote ya mdada mrembo.

Inshort nyuzi nyingi tu ambazo ziko on trending sijawahi zielewa [emoji16]
[emoji28][emoji28][emoji28] uko kama Mimi tu hizo ndio thread's zisizozielewa haswa
 
[emoji28] halafu kibaya zaidi kila niki-login, threads ninazokutana nazo on trending lazima ziwepo tatu au nne tajwa hapo juu daah [emoji16]
Ndio maana niliomba JF wawe na option ya mtu ku block mada asizozitaka maana sikuhizi mada za kijinga Kwa vile Zina commentiwa sana ndio zinakuwa Zina trend sana na unakuta hazina jambo la maana la ku feed ubongo. Wangeboresha app au website vile mtu anacho comments zaidi ndio awe analetewa vitu design hyo ka walivofanya Instagram page unazopenda ku visit unaletewa vitu vya aina hyo hyo.
Sasa humu nyuzi za hovyo ndio zina pop up hapo juu
 
"Hatima ya maisha yangu iko mikononi mwa kijana wa Buguruni" πŸ€” Huu uzi una trend kweli! Ila sijawahi kuulewa unahusu kitu gani hasa.

Kuna siku nilijaribu kuufungua, nikakuta watu wanatukanana! Nikabakia tu mdomo wazi.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Hii Uzi sijawahi kuuelewa Mara kwa Mara nauona juu
 
Mimi Uzi wa mgogoro wa Russia na Ukraine nauchukia Sana,Kuna siku nilijaribu kufungua nakuta Ni liuzi lirefu na vitu havieleweki nikasema siwezi shoboka na mambo ya nchi za watu.

Tangu siku hiyo huo Uzi huwa naupita kwa Kasi ya 5G
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…