Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Huyu hayuko serious. Hivi kuna Uzi unafurahisha Kama ule? Mimi nikiona nimekuwa bored tu naufungua huo. Kuna watu walikuwa na mamilioni mule wamefilisika Hadi wamerudi kwa wazazi 😀😀😀
Anakusalimia mjeda wako na amesema siyo vizuri kutwa kwenye mitandao.
 
Mimi Uzi wa mgogoro wa Russia na Ukraine nauchukia Sana,Kuna siku nilijaribu kufungua nakuta Ni liuzi lirefu na vitu havieleweki nikasema siwezi shoboka na mambo ya nchi za watu.

Tangu siku hiyo huo Uzi huwa naupita kwa Kasi ya 5G
Kimsingi ni Uzi ambao hata mimi siukubali kabisa kuna mwamba huwa yeye anacomment tu Slava Ukraine.
 
“Umevaa nini leo? Tupia uturingishie”
 
Huo uzi siupendi sana sana maana hata sijawahi kuuelewa na sijui watu gani humu huwa wanacomment humo na kuuweka on trending wakati wengi humu tumeonesha kutoupenda
Huo uzi ukiwa una kazi uwezi kuuelewa kabisa lakini kwa wanao tafuta kazi serikalini wanaelewa sana maana yake!
 
1. New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Huo uzi sijawahi kuuelewa kabisa kwanzia mwaka juzi umeanzaa, kwanza wananiuzi na kiingereza chao. Sijawahi kujua wanaongea nini , wanaongea kiingereza kigumu sana

2. Makapuku Forum (Hawa sijui wamepotelea wapi siku hizi)

3. Uzi wa kupeana Likes, Comment chochote upate likes

4. Kula Tunda Kimasihara (Naona ni kama mambo ya kitoto maana kwangu mm kila siku nikila tunda huwa ni mimasihara , so sijawahi kuona jipya)

5. Wazee wenzangu wa kuweka mzigo , Njooni tubashiri mechi za leo ( Hawa jamaa kila siku wanapigwa na mhindi ila hawakati tamaa)
 
Mpaka muda huu uzi wa watumishi unaongoza ukifuatiwa na wazee wa kuweka mzigo[emoji23][emoji23].
Tuendelee wazee
 
Sizipedi zote ulizozitaja,na Huwa nazipita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…