Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

wewe mwenyewe umetoka kusema kwamba sayansi ikishindwa ku prove kitu saivi sio kwamba hakipo, inawezekawa ikafanikiwa kuprove baadae,

kwa mantiki hiyo, uta conclude vipi Mungu hayupo kwasababu Sayansi imeshindwa ku prove Yupo ?
Sayansi haisemi Mungu yupo.

Ninyi watu wa dini na imani ndio mnasema Mungu yupo.

Sasa unataka sayansi ije iprove kitu ambacho haijakisema?

Yani kitu useme wewe halafu uthibitisho utake mimi nikupe?

Hivi ina make sense kweli?
 
nimetoka kumjibu hilo swali Infropreneur

nimemuelezea keanini hiyo cycle inajirudia, nikamwambia kama hajaelewa asome kwa hatua
 
Unathibitishaje kwamba akili ya binadamu ina limit?

Hili nalo la kuuliza. Akili ya mwanadamu ina ukomo kama ulivyo ukomo wa kamba aliyo fungiwa mbuzi. Huku ndiko tamko akili lilipotokea.

Ukiangalia maana ya tamko Akili linaonyesha wazi lina ukomo. Akili ni kizuizi kinachomfanya mwanadamu asikosee katika kutenda au katika kauli. Hapa tayari kuna ukomo kwa minajili ya maana ya akili. Wewe huwezi kujua yaliyo fichikana wala yatakayo tokea kesho kwa uhakika wake. Huu tayari ni ukomo.

Shida yenu huwa mnakimbia uhalisia kwa makusudi au kwa kutokujua.
 
Morality has nothing to do with religion.

Kuna ancient values zilizosamvmbaa ulimwengu kote zilizojulikana kama Golden rule ambazo zilikuwa zikitumika miaka ya zamani kabla ya dini.

Golden rule ni sheria ya kuwa treat watu positive the way ambavyo wewe ungependa ufanyiwe.

Baadaye dini ndio zikaja kukopi hizo values na kuziingiza kwenye vitabu vyao ili kupitisha agenda yao.
 
Complexity ni lazima iumbwe na complexity nyingine kubwa zaidi, au inaweza kutokea tu kutoka simpler complexity?
tuna relay kwenye namna moja ya ufikiri, ambapo labda ndo uwezo wa akili yetu unapoishia

nikatoa mfano kuna vitu common ambavyo wewe unaweza ukafikiri na ukavipatia majibu kwa haraka tuu

ila ukimpa labda nyani hawezi kufikia majibu hata umuue kwasababu namna yake ya ufikiri inaishia sehemu flani

kwaiyo atakua anatafuta kulitatua hilo jambo kwenye levey yake ya akili ndo maana anashindwa

na sisi binadamu ndo hivyo tuna jaribu kutatua, ila tunafanikiwa kwa yale yaliyopo ndani ya hiyo level
 
Sayansi haisemi Mungu yupo.

Ninyi watu wa dini na imani ndio mnasema Mungu yupo.

Sasa unataka sayansi ije iprove kitu ambacho haijakisema?

Yani kitu useme wewe halafu uthibitisho utake mimi nikupe?

Hivi ina make sense kweli?

Umejuaje kama Mungu hayupo ?

Kwanza Sayansi haipo katika kutoa FACTS hili kwanza weka akilini. Sababu msingi wake au misingi yake (Scientific Method) imeasisiwa na mwanadamu, kwahiyo ina mapungufu mengi.

Pili, Wanasayansi wengi wanakiri uwepo wa Mungu, ukiona wewe unapinga uwepo wa mungu, ujue hufikirii mambo kwa undani.
 
Umeandika mengi lakini hujajibu swali nililokuuliza.

Narudia.

Complexity ni lazima iumbwe na complexity nyingine kubwa zaidi, au inaweza kutokea tu kutoka simpler complexity?
 
Ulimuona wapi huyo Mungu akiumba mbingu na ardhi?

Au unafosi imani zako uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule?

Una hoja za kitoto sana. Wewe babu yako wa sita ulimuona wapi ? Au akili unakiri unayo ? Umewahi kuiona au njaa umewahi kuiona ?

Bali uwepo wa hivyo niivyo vitaja vina ishara zake anuai kwazo vinathibitisha uwepo wake.

Twende kwa hoja za kiakili, maana huwa unadai ninatumia Qur'an tu na sina hoja zaidi ya hizo. Sasa leo nataka nipite mapito unayopita uone kama hutakimbia huu uzi.

Tuendelee ....
 
Umejuaje kama Mungu hayupo ?
Kwa sababu Mungu huyo hajawahi kuwepo na hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
Kwanza Sayansi haipo katika kutoa FACTS hili kwanza weka akilini. Sababu msingi wake au misingi yake (Scientific Method) imeasisiwa na mwanadamu, kwahiyo ina mapungufu mengi.
Hiyo misingi ya Dini ime asisiwa na nani?
Pili, Wanasayansi wengi wanakiri uwepo wa Mungu, ukiona wewe unapinga uwepo wa mungu, ujue hufikirii mambo kwa undani.
Wanasayansi wengi kukiri uwepo wa Mungu, Si uthibitisho wa uwepo wa Mungu bali ni imani zao tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
 
Sasa kama akili ya binadamu ina limit utajuaje hicho unachokisema kipo, ni kweli kipo na sio kwamba hakipo na umeshindwa kujua hakipo kwasababu akili yako ina limit?
 
Uko sahihi. Hata mimi wakati fulani nimehoji kupitia uzi. Kwa binadamu nini kinafuata baada ya ufahamu? Tumeishia kwenye consciousness. Hiyo next level ndio uungu
Kwanini mwisho wa fikra zako kuwe ndio chanzo kingine ambacho hujakithibitisha?
 
Kwa sababu Mungu huyo hajawahi kuwepo na hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Hii haiwezi kuwa sababu, sababu inaonyesha uongo wa wazi. Kitu ambacho hakijawahi kuwepo huwezi kukijua mpaka ulete ushahidi wa hakika.

Hapa umeandika sentensi isiyo kuwa na maana katika lugha na kiakili pia.

Nakuuliza swali rahisi kitu ambacho hakijawahi kuwepo umeijuaje au unakijuaje ?
 
Wanasayansi wengi kukiri uwepo wa Mungu, Si uthibitisho wa uwepo wa Mungu bali ni imani zao tu zisizo na uthibitisho wowote ule.

Imani ni nini ?

Huu ni uthibitisho sababu misingi wanayotumia kutafuta ukweli ni ya kiakili na majaribio tu.
 
Una hoja za kitoto sana. Wewe babu yako wa sita ulimuona wapi ? Au akili unakiri unayo ? Umewahi kuiona au njaa umewahi kuiona ?
Unazijua nomino dhahania?

Njaa, akili, pumzi, hofu ni mfano wa nomino hizo.

Na nomino hizo hazipo katika uhalisia bali katika dhana za kufikirika tu.
Bali uwepo wa hivyo niivyo vitaja vina ishara zake anuai kwazo vinathibitisha uwepo wake.
Thibitisha njaa unayo kwa kuishika au kuionyesha.
Twende kwa hoja za kiakili, maana huwa unadai ninatumia Qur'an tu na sina hoja zaidi ya hizo. Sasa leo nataka nipite mapito unayopita uone kama hutakimbia huu uzi.

Tuendelee ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…